madaili
Member
- Mar 6, 2014
- 32
- 27
Jamaa alienda kuhudhuria mkutano, katikati ya mkutano mkewe alimpigia simu lakini akakata na kumtumia meseji kuwa yupo mkutanoni atampigia baada ya mkutano kuisha. Mkutano ulipoisha aligundua kuwa simu yake imeishiwa chaji na imezima, akaamua kumuazima simu jamaa aliyekuwa amejuana naye kwenye mkutano huo, lakini alipoingiza namba ya simu ya mkewe akakuta jamaa kumbe tayari ana namba ya mkewe, lakini jina ambalo jamaa huyo amesevu ni [Mlupo toka Facebook], ngumi zikarushwa na wote wakavunja meno ya sebuleni wakapelekwa hospitali kwa matibabu.
Mkewe baada ya kufika hospitali aligundua simu yake imeisha chaji imezima, akaamua kumuazima simu mwanamke aliyekuwa mapokezi anamsubiria ndugu yake, alipoingiza namba akakuta simu ya bwana wake tayari ipo na mwanamke huyo amesevu kama [Buzi lililonona], ngumi zikapigwa na baada ya kuamuliwa wakapelekwa kwenye chumba cha matibabu, ndani ya chumba cha matibabu humo namo kulikuwa hakutoshi...