Ugawaji majimbo wa NEC

MrFroasty

JF-Expert Member
Jun 23, 2009
1,195
592
Wana JF na wadanganyika kwa ujumla,

Ningelipenda nikakupeni kidokezo juu ya ugawaji majimbo, mimi binafsi yangu ni mzanzibari na katika historia yetu huko visiwani tushashuhudia ugawaji majimbo mara karibuni 2.

Mara zote hizo 2 ugawaji majimbo hufanywa na serekali ya iliyoko madarakani kukimbia wapinzani kupata viti kwenye vyombo vya sheria.

Ningelipenda nanyi musitizame au kuhangaika kwenda mbali duniani, musome historia hiyo ya Zanzibar.Mara ya mwisho tukiachilia mbali huko kwenye historia ya 60's, ni hapo baada ya uchaguzi wa 1995.Serekali ya CCM iligawa majimbo kama ni technique ya kukimbia majimbo au concentration ya wapinzani.

Kwa hiyo kuweni makini...na ikiwezekana wadanganyika muandamane kupinga suala hili.
 
Chama hiki ambacho serikali yake iko madarakani kina jali sifa za ushindi katika uchaguzi- kikisikia CCM imeshinda kwa kishindo ndio wanajisikia vizuri hawajali kabisa wameifanyia nini nchi yetu ambayo kwa muda mrefu imekuwa inaitwa changa toka mie nazaliwa.

Shameon them, what do they take us for?

Ningependa ingekuwa majimbo yote mapya (kama ilivyo kwa vyama vipya) yasiruhisiwe kuhusika kwenye uchaguzi wa mwaka huu!!
 
Nadhani iliwahi kuulizwa hapa JF kwamba lengo la kuongeza majimbo ni nini? Nawasikia wakidai ongezeko la watu kuwa kigezo kikubwa, which is illogical.

China wana wabunge wangapi?
 
Hapa Mkullo inamgusa, jamaa hawamtaki kilosa mpaka kaomba amegewe jimbo upande anaona anaweza shinda
 
Back
Top Bottom