Uganga/ndumba kwenye biashara upo? COCO case study!

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,160
1,719
Wadau hili swala mnalioneje? Huwa napenda sana ku analyse biashara tofauti kila mahali niendapo, kuna swala linanishangaza mara nyingi. Unakuta kuna sehemu mbili ziko eneo moja lakini mmoja anabiashara sana kuliko mwenzake wakati logical reasoning inaonyesha mwenzake ambaye hana wateja ana vigezo zaidi vya ubora! Mfano hebu tuangalie pale coco beach. Ukiingia upande wa kushoto kule kwenye karaoke juma5 panajaza mpaka pakukaa hakuna lakini kuanzia hapa kati kwenye pool table kuja ndani hazina lounge na huku kwingine japo kuna mazingira mazuri zaidi, choo kizuri, chakula kizuri zaidi, mziki mzuri nakadhalika ila HAPAJAI kama upande ule wenye kitimoto! NINI SIRI? Na "usomi" wangu wote wa business management na practice nashindwa pata jibu mpaka nabaki kufikiri vitu nisivyoamini kama uganga kwa sababu logical reasoning inagoma. Wadau hili mnaonaje?
 
Kitimoto hiyo ni kawaida........na uchawi haupatani na mdudu........hiyo ni nachurale........

huko kwingine inaweza kuwa kauli labda........usafi.......huduma bora........mazingira safi.......lolote laweza sababisha........
 
Preta umeshawahi hudhuria hayo maeneo mara kadhaa?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom