Uganga na Siasa Tanzania - Is it TRUE?

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
0
Nimesoma kwenye gazeti la Alasiri la jana, 08/12/2007 (www.ippmedia.co.tz) na kukuta article attached below. Jamani sisemi kwamba naamini au ni kweli lakini kikubwa ni kwamba panapofuka moshi lazima pawe na moto japo ni cheche tu!!! Kama mambo ni ukweli then kweli JK anayo kazi kubwa hapo manake jamaa labda wanatumia mamboz kumpumbaza.....ha ha haaaaaa

Mganga awaumbua vigogo
2007-12-08 15:32:47 Na Mwandishi Wetu, Jijini


Kama wahenga wasemavyo kwamba mfa maji haachi tapatapa basi ndivyo hali ilivyo hivi sasa kwa baadhi ya waheshimiwa, ambao inadaiwa mashangingi yao yamekuwa yakipigana vikumbo kwa mtalaam mmoja wa mambo ya jadi.

Lengo za ruti hizo za usiku usiku za vigogo, mganga huyo maarufu Jijini anasema ni kutaka awatengeneze ili wanusurike na panga kali la Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake, mganga huyo amejisifu akisema `ameshawapiga tafu` vigogo kibao nchini .

Amesema kwa jinsi waheshimiwa wengi wanavyomtembelea hivi sasa utadhani ni wakati wa kampeni za uchaguzi.

``Kijana... ninachokueleza ni kwamba hivi sasa, mambo yamekuwa mazuri kwa upande wangu. Yaani ni kama inavyokuwa wakati wa kipindi cha uchaguzi ambapo viongozi wengi wa kisiasa huja kunisalimia...kufa kufaana bwana,`` akatamba.

``Juzi pekee waliletana wawili ... wote walikuja kwangu usiku na hofu yao ni moja tu, kwamba niwasaidie ili mzee (Rais JK) asije akawaengua kwenye nafasi walizo nazo,`` akaongeza.

Hata hivyo alipotakiwa kuwataja waheshimiwa hao, mganga huyo amegoma akisema masharti ya tiba yake hayamruhusu kufanya hivyo.

``Kwani nyie kazi yenu haina masharti na maadili? Basi hata mimi siwezi kukutajia hao watu...kwanza tunaheshimiana mno kwa kuwa wengi ni wateja wangu wa siku nyingi,`` akasema mganga huyo.

Alipoulizwa kwa nini basi ameamua kuwaumbua wateja wake, mganga huyo akasema haoni ubaya wa kufanya hivyo kwa kuwa hakuwataja kwa majina.

``Mimi sijawataja kwa majina....lakini hata ningewataja, si wanakuja kwangu kwa hiari yao?, Sasa wanahofia nini kujulikana?`` akasema mganga huyo.

Amesema ruti za kwenda kwake ziliongezeka baada ya kuwepo kwa fununu kwamba Rais Kikwete angepangua safu ya watendaji wakuu Serikalini.

SOURCE: Alasiri
 

Choveki

JF-Expert Member
Apr 16, 2006
449
250
Je mmesahau yule aliyekuwa ameangusha hirizi na majina ya wabaya wake(wagombea wenzake urais) wakati wa kampeni ya urais kule Tabora?

Sijui kama yupo ambaye haendi kwa hao wataalam. Kwa upande mwingine siyo viongozi wa kitanzania tu, waafrika au wa asia tu hata wazungu nasikia wapo ambao huwa wanapenda sana mambo hayo ya kwenda kuganga na kuganguliwa kabla hawajaanza shughuli yeyote nzito.
Tetesi ni kuwa hata yule Ronald Reagan wa Marekani miaka ileee alikuwa hajambo katuka hayo maswala.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom