McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 889
- 2,863
Serikali ya Uganda, kupitia Tume ya Mawasiliano ya Uganda (UCC), imetangaza kusimamisha kwa muda huduma za intaneti kwa umma na usajili wa laini mpya za simu nchini humo, ili kuzuia usambazawaji wa taarifa potofu, vitendo vinayoweza kuchochea vurugu au kuhatarisha usalama wa taifa.
Kwa mujibu wa agizo hilo, waendeshaji wote wa mitandao ya simu na watoa huduma za intaneti wametakiwa kusitisha huduma hizo kuanzia Januari 13, 2026 saa 12 jioni hadi itakapotolewa taarifa nyingine ya kurejesha huduma.
Huduma zilizosimamishwa ni pamoja na upatikanaji wa intaneti kwa umma, uuzaji na usajili wa SIM kadi mpya pamoja na huduma za data roaming kwa nchi wanachama wa One Network Area.
Hata hivyo, huduma muhimu kama mifumo ya afya, benki, ATM, malipo ya kodi, mifumo ya serikali, umeme, maji, mafuta, usafiri na usalama wa mitandao zimeruhusiwa kuendelea kufanya kazi kupitia intaneti isiyo ya simu.
UCC imesisitiza kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii, programu za ujumbe na VPN za simu yakipigwa marufuku kabisa.
Soource: Uganda Communications Commision