Uganda yapiga marufuku uvutaji Sigara hadharani

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,296
151001140159_cigarette_butts_640x360_ap.jpg

Sheria kali dhidi ya uvutaji sigara na uuzaji wa tumbaku imeanza kufanya kazi nchini Uganda

Watu wanaowasha sigara kwenye baa,migahawa na hoteli watalipa faini ya dola 60 au kifungo cha mpaka miezi miwili.

Wavuta sigara wanapaswa kuwa umbali wa mita 50 kutoka kwenye maeneo ya hadhara, kama vile Shule,Hospitali na kwenye maeneo ya usafiri wa umma

Sheria mpya zinawabana pia wauzaji wa sigara za kilektroniki, na shisha ambazo zimekuwa maarufu sana kwenye kumbi za burudani za usiku jijini Kampala.

Zaidi ya hayo katika hatua za kupambana na uvutaji sigara, Serikali imepiga marufuku uuzwaji wa sigara moja moja na kuweka makali zaidi kwenye matangazo na uuzaji wa tumbaku kwa walio chini ya miaka 21.
 
Maeneo ya kazi wanatakiwa wajengewe eneo la kuvitia sigara, yaani kama vile chooni palivo kwamba mtu akitaka kuvuta anakwenda huko kuvuta kama vile anavyokwenda chooni akihisi haja
 
Huu ni mfano wa kuiga kutoka Uganda, yaani wavutaji wamekuwa kero, unakuta mtu anavuta sigara halafu anakupulizia moshi kana kwamba na wewe ni mvutaji mwenzake, tena kuna madereva na makonda wanaovuta sigara ndani ya gari huku abiria wakiwa ndani.
 
Sasa apo itakuwa aina radha tena. Maana raha ya cigarettes uvute mbele za watu
 
Hii itasaidia kupunguza uvutaji - kiafya ni vema japo wakulima na industry ya tumbaku hawatafurahia hatua hizi.
 
Hongera sana Uganda kwa maamuzi yao ya busara kulinda afya za wananchi wake wasiovuta sigara. Mfano mzuri wa kuigwa na nchi za Afrika . Nchi kama USA wanatumia mpango huu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom