Uganda wamejaribu, Rais Samia unaweza washitaki hao Mawaziri wezi

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Serikali ya Rais Museven imeweza angalau kumfikisha waziri mahakamani kwa wizi.

Kwa mbiringe zinazoendelea bungeni na nje ya bunge kwa ripoti ya CAG na kashifa za wizi wa mali za umma namuomba rais Samia afumbe macho sasa.

Namuomba asiwaangalie usoni hao wezi awafikishe mahakamani tu maana hatakuwa wa kwanza kufanya hivyo.

Asisubiri wananchi tuichoke hii serikali yake mapema.
Screenshot_20230407-081751_Instagram.jpg
 
Ungetakiwa uandike Uganda wameweza, sio wamejaribu.

Huyu wa kwetu nguvu zake zinaishia kwenye kuteua na kutengua, hayo ya mahakamani hayawezi kabisa..

Ndio maana hujisifu kwa kushika kwake "kalamu nyekundu", ndio maana wezi nao hata hawamuogopi tena sababu wanajua adhabu ya juu kwao ni "kalamu nyekundu".
 
Serikali ya Rais Museven imeweza angalau kumfikisha waziri mahakamani kwa wizi.

Kwa mbiringe zinazoendelea bungeni na nje ya bunge kwa ripoti ya CAG na kashifa za wizi wa mali za umma namuomba rais Samia afumbe macho sasa.

Namuomba asiwaangalie usoni hao wezi awafikishe mahakamani tu maana hatakuwa wa kwanza kufanya hivyo.

Asisubiri wananchi tuichoke hii serikali yake mapema.View attachment 2579251
Ukiangalia taarifa ya CAG hakuna sehemu unaweza mpata Waziri Kwa sababu sio afisa masuhuli Bali Kiongozi wa sera tuu so hakuna ushahidi wa Moja kwa Moja wa Waziri yeyote kuhusika isipokuwa watendaji kuanzia Karibu Mkuu na maofisa wake wa chini.

Huko Uganda huyo alihusika directly na wizi.
 
Ungetakiwa uandike Uganda wameweza, sio wamejaribu.

Huyu wa kwetu nguvu zake zinaishia kwenye kuteua na kutengua, hayo ya mahakamani hayawezi kabisa..

Ndio maana hujisifu kwa kushika kwake "kalamu nyekundu", ndio maana wezi nao hata hawamuogopi tena sababu wanajua adhabu ya juu kwao ni "kalamu nyekundu".

Kikwete ndio mshauri wake mkuu anashindwa nini kumuongoza kuwashtaki mawaziri wezi [ wamenunua nyumba Dubai] ili hali yeye enzi ya utawala wake aliwafikisha mahakamani mawaziri wa fedha wa enzi hizo Dan Yona na Basil Mramba na kuwashtaki kwa ubadhirifu na hatimaye kufungwa jela!
 
Serikali ya Rais Museven imeweza angalau kumfikisha waziri mahakamani kwa wizi.

Kwa mbiringe zinazoendelea bungeni na nje ya bunge kwa ripoti ya CAG na kashifa za wizi wa mali za umma namuomba rais Samia afumbe macho sasa.

Namuomba asiwaangalie usoni hao wezi awafikishe mahakamani tu maana hatakuwa wa kwanza kufanya hivyo.

Asisubiri wananchi tuichoke hii serikali yake mapema.View attachment 2579251
Huyu hawezi hata iweje labda kama ameshachoka kulamba asali iliyoachwa kwenye kibuyu
 
Back
Top Bottom