Uganda:Spika asema waliokeketwa hawafai

Uganda:Spika asema waliokeketwa hawafai

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
141203100911_uganda_speaker_512x288_bbc.jpg
Spika wa Bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga awashauri wanaume kutowaoa wanawake waliokeketwa

Spika wa Bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga amewashauri wanaume kutowaoa wanawake waliokeketwa akiwataja kuwa mzigo ambao hauwezi kuijenga jamii.

Kulingana na gazeti la daily Monitor,Spika Kadaga alitoa wito huo wakati wa sherehe ya kitamaduni ambayo inapinga ukeketaji ilioandaliwa na mfuko wa umoja wa mataifa unaosimamia idadi ya watu na wahisani wengine.

''Mwanamke ambaye amekeketwa hana thamani yoyote. Achaneni na wanawake waliokwenda kukeketwa na badala yake chagueni wanawake ambao hawakukeketwa na ambao wanaweza kuimarisha jamii'',alisema Bi Kadaga.

Utamaduni huo unaojulikana kama upashaji tohara wanawake umekithiri miongoni mwa tamaduni nyingi na bara la Afrika kwa jumla na hutumiwa kumuandaa mwanamke anayeolewa ama hata kuonyesha kwamba ,mwanamke amebalehe.

Nchini Uganda ,utamaduni huo hufanyika mashariki mwa Uganda katika makabila matatu ikiwemo lile la Pokot,Sabiny na Tepeth hususan katika wilaya za Kampchorwa,Kween na Bukwo.

Bi Kadaga ambaye aliyeandamana na waziri wa maswala ya kijinsia Rukia Nakadama wote walitia sahihi ya kumaliza ukeketaji nchini Uganda.

Pia aliwaonya wazazi katika eneo hilo kukoma kuwalazimisha wanao katika ndoa za mapema na badala yake kuwataka kuwapeleka shule.

Baadhi ya wanawake waliokuwa wakitekeleza tendo hilo waliiomba serikali kulisaidia kundi la watu ambao wamewacha kuwapasha tohara wanawake.

Source:http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/12/141203_uganda_spika_ukeketaji
 
mbona yeye amekeketwa? asiwadanganye wengine bure!
 
Sasa anawahukumu victims ...wengi wanakeketwa bila ridhaa zao...hiyo tayari ni pigo kwao...yeye anawaongezea pigo lingine la wanaume kuwasusa...
 
Kwani siku hizi kuna wanaume wambeya. Hata kama wamemwambia hivyo angechuja maana asije shangaa siku moja akaporwa mume na mdada wa hivyo. Sijui inakuwaje lakini kuna makabila yanayokeketa yana watoto wengi kuliko inavyosemwa na wanaharakati.
 
Sijaipata point hapo...wewe unaona ukeketaji poa?

Maana wenyewe wanasema wanakeketa wanawake ili kuwapunguzia hamu ya ngono...je ni haki? Ili iweje? Ili mume aoe wake 6 ambao watatulia wanasubiri mgao kwa kuwa hawana mihemko?

Inakuwaje sasa wakiolewa na mume asiye na wake wengi...wataweza kutunza ndoa zao na hawana hamu?

Ukeketaji si swala la kushadadia...ingawa alichosema huyu speaker pia si sahihi maana imeonyesha amekosa huruma kwa victims
 
Shida yangu ni sababu zinazotolewa na wanaharakati katika kupinga suala hili. Kwa mfano wanasema wanaokeketwa wanapata shida wakati wa uzazi, makabila yanayofanya hivyo yanaona shida ya uzazi iko hata kwa makabila mengine.

Wangeweza kusema kuwa kukeketa ni aina nyingine ya kupenda nafsi maana wanaofanyiwa hivyo hawajafikia umri wa kutia maamuzi kama vile kuolewa (Matrimonial concert) kisheria. Hasa kwa vile kwa takwimu za Tz watu wengi ni waumini mahali fulani na dini zinapinga ubinafsi
 
Back
Top Bottom