Uganda Cranes yaiangamiza Misri 1-0

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
cranes.jpg


Kikosi cha timu ya taifa ya Uganda maarufu kama Uganda Cranes. Picha/MAKTABA
Na GEOFFREY ANENE

Imepakiwa - Thursday, August 31 2017 at 17:38
Kwa Mukhtasari

Uganda huenda ikawa timu ya kwanza kutoka eneo la Afrika ya Mashariki (Cecafa) kushiriki Kombe la Dunia tangu lianzishwe mwaka 1930 baada ya kuchukua uongozi wa kundi E kwa kuzaba Misri 1-0 jijini Kampala, Alhamisi.

UGANDA huenda ikawa timu ya kwanza kutoka eneo la Afrika ya Mashariki (Cecafa) kushiriki Kombe la Dunia tangu lianzishwe mwaka 1930 baada ya kuchukua uongozi wa kundi E kwa kuzaba Misri 1-0 jijini Kampala, Alhamisi.

Ni mara ya kwanza kabisa Uganda imepata ushindi dhidi ya Misri tangu kabiliano lao la kwanza mwaka 1962. Uganda ilikuwa imepoteza mechi tisa mfululizo dhidi ya Misri kabla ya bao la Emmanuel Okwi kuipa Cranes ushindi huo wa kihistoria.

Cranes, ambayo ilirejea katika Kombe la Afrika mwaka 2017 baada ya kuwa nje tangu mwaka 1978, ilizima Pharaohs kupitia bao la Okwi lililopatikana dakika ya 51.

Beki wa Gor Mahia Godfrey Walusimbi pamoja na kiungo wa zamani wa Gor Mahia, Khalid Aucho na mchezaji bora wa mwaka wa Afrika mwaka 2016 anayecheza barani humu Denis Onyango ni baadhi ya vifaa Uganda ilitumia kudhalilisha Wamisri. Nayo Misri ilikuwa na magwiji kama Mohamed Salah (Liverpool, Uingereza), Mohamed Elneny (Arsenal) na kipa Essam El Hadary aliyegonga umri miaka 44 Januari 15 mwaka 2017.

Mataifa haya yatarudiana Septemba 5 nchini Misri. Uganda itajiweka pazuri zaidi kufuzu ikipata ushindi mjini Alexandria.

Uganda inanolewa na Mganda Moses Basena nayo Misri iko chini ya raia wa Argentina, Hector Cuper.
Waganda wanashikilia nafasi ya 73 duniani. Misri ni ya 25. Mataifa mengine kutoka Cecafa – Kenya (82 duniani), Rwanda (119), Tanzania (120), Ethiopia (120), Burundi (132), Sudan Kusini (148), Sudan (152), Djibouti (192), Eritrea (206) na Somalia (206) yaliondolewa katika mbio za kufika Urusi mwaka 2018.
Mechi kati ya washiriki wengine wa kundi hii Black Stars ya Ghana na Red Devils ya Congo Brazzaville ni Ijumaa.

JEDWALI LA KUNDI E
Timu P W D L GD Pts
Uganda 3 2 1 0 +2 7
Misri 3 2 0 1 +2 6
Ghana 2 0 1 1 -2 1
Congo 2 0 0 2 -2 0
 
Back
Top Bottom