Ugaidi Tanzania Unafanikiwa

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
100,026
122,645
Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni ugaidi (terrorism).

Lengo la ugaidi ni kuwatia watu hofu na kufikisha ujumbe kwa wengi kwa njia ya hofu.

Matukio yanayoongelewa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao yote ya kijamii mpaka nchi za nje kwa sasa ni hayo, kuanzia watu kutekwa, kutolewa bastola hadharani, mauaji ya Kusini huko, watu kukutwa kwenye viroba, kupotea kwa watu na mengi mengineyo, yote yanaashiria ugaidi.

Magaidi hujitokeza na kusema sisi ndiyo tuliyoyafanya hayo ili waogopwe au matakwa yao yatimizwe au hukaa kimya na kuwachochea kivingine kwa lengo hilo hilo.

Matukio ya ugaidi yanapotokea pia hujitokeza wengine ambao hutumia fursa hiyo kufikisha ujumbe wao kwa njia tofauti.

Kwa yanayotokea Tanzania, ukweli ni kuwa, kuna wanaofanya huo ugaidi wa kutisha na kuna wanaotumia huo gaidi kama ni fursa kwao kufikisha ujumbe wao ama kwa kuongezea ugaidi mwingine au kwa kuendeleza hofu kwenye jamii na vyombo husika.

Watanzania tunachotakiwa kufanya ni kukaa kimya na kufunga hii mijadala yote na kuwacha kuripoti matukio yote ya kigaidi ili kushindana na ugaidi.

Gaidi kama matukio yake hayaongelewi kazi yake inakuwa haijafanikiwa.

Au leta mawazo yako ni njia gani zitumike kutatuwa hili tatizo "linalotukabili".

Kwa muono wangu, kila tunapoyaongea na kuyasambaza ndiyo furaha ya magaidi na ndiyo lengo lao, wengi wajawe na hofu.

Kwanini? Mie sijuwi.
 
Nashindwa kuelewa kwa nini serikali tukufu ya CCM iko kimya_ hata wabunge wake wanapokuwa wanakabiliwa na matishio ya kutekwa?

Watanzania hatuwezi tukakaa kimya eti tuwakomeshe magaidi kwa kimya chetu!!!.
FaizaFoxy Ndugu yangu nitaumia kiasi gani nikisikia umetekwa na kuteswa?
Je moyo Wangu utahimili kukaa kimya kweli?
Nitafanya niwezalo . Nikishindwa kulipa kisasi basi nitaandika.
Kamwe sitokaa kimya.
Kuna watekaji walitajwa kwa majina na miongoni mwao ni Ramadhan Igwondu, je alichukuliwa hatua gani?
Serikali yetu ya Leo imekuwa Crime Organiser ndio maana iko kimya na hata kwa maswali mazito inakuja na majibu mepesi.
 
dah! hapa ndio umetutisha zaidi. magaidi kwa lengo gani. siasa, dini au pesa? magaidi wasiodai kitu ni wa aina gani!

Terrorism maana yake ni vitisho, hata nyumbani unapomkemea mwanao ni vitisho "terror".

Inabidi ubadili njia na uanze kumlea bila kutishana.

Chini hapo nimesema, sijuwi. Ni mjadala.
 
Nashindwa kuelewa kwa nini serikali tukufu ya CCM iko kimya_ hata wabunge wake wanapokuwa wanakabiliwa na matishio ya kutekwa?

Watanzania hatuwezi tukakaa kimya eti tuwakomeshe magaidi kwa kimya chetu!!!.
FaizaFoxy Ndugu yangu nitaumia kiasi gani nikisikia umetekwa na kuteswa?
Je moyo Wangu utahimili kukaa kimya kweli?
Nitafanya niwezalo . Nikishindwa kulipa kisasi basi nitaandika.
Kamwe sitokaa kimya.
Kuna watekaji walitajwa kwa majina na miongoni mwao ni Ramadhan Igwondu, je alichukuliwa hatua gani?
Serikali yetu ya Leo imekuwa Crime Organiser ndio maana iko kimya na hata kwa maswali mazito inakuja na majibu mepesi.

Kuna kitu kinaitwa moles kwenye intelijensia.
 
Huo ni mpango wa kushindwa malengo fulani .wahusika wanafanya hayo kutisha wengine badae wanaotishwa watajibu hapo utamu utakuja.naamini kilichotokea msaanii kutekwa na Rc kuahidi kupatikana basi hakuna shaka gov.inajua .bashite ni mjuaji ktk hili na yuko kwa nguvu ya baba J. Iko siku watajutia na damu na maumivu ya hao wote yatakua juu yao na familia zao.kwani mchuma janga hula na wa kwao.
 
Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni ugaidi (terrorism).

Lengo la ugaidi ni kuwatia watu hofu na kufikisha ujumbe kwa wengi kwa njia ya hofu.

Matukio yanayoongelewa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao yote ya kijamii mpaka nchi za nje kwa sasa ni hayo, kuanzia watu kutekwa, kutolewa bastola hadharani, mauaji ya Kusini huko, watu kukutwa kwenye viroba, kupotea kwa watu na mengi mengineyo, yote yanaashiria ugaidi.

Magaidi hujitokeza na kusema sisi ndiyo tuliyoyafanya hayo ili waogopwe au matakwa yao yatimizwe au hukaa kimya na kuwachochea kivingine kwa lengo hilo hilo.

Matukio ya ugaidi yanapotokea pia hujitokeza wengine ambao hutumia fursa hiyo kufikisha ujumbe wao kwa njia tofauti.

Kwa yanayotokea Tanzania, ukweli ni kuwa, kuna wanaofanya huo ugaidi wa kutisha na kuna wanaotumia huo gaidi kama ni fursa kwao kufikisha ujumbe wao ama kwa kuongezea ugaidi mwingine au kwa kuendeleza hofu kwenye jamii na vyombo husika.

Watanzania tunachotakiwa kufanya ni kukaa kimya na kufunga hii mijadala yote na kuwacha kuripoti matukio yote ya kigaidi ili kushindana na ugaidi.

Gaidi kama matukio yake hayaongelewi kazi yake inakuwa haijafanikiwa.

Kila tunapoyaongea na kuyasambaza ndiyo furaha ya magaidi na ndiyo lengo lao, wengi wajawe na hofu.

Kwanini? Mie sijuwi.
Sa ndugu yako mfano akitekwa inaama ukae kimiya usitangaze sababu utakuwa una promote ugaidi sister???,,au,,,,,,ivi inawezekana Dola ikafanya ugaidi au matukio ya kigaidi,,,au ili neno gaidi ni kwasisi waislam tu duniani
 
Back
Top Bottom