Corticopontine
JF-Expert Member
- Sep 20, 2019
- 665
- 1,278
Ahsante sana kwa somoUgaidi au kwa Kiingereza terrorism lina utata sana katika tafsiri. Mpaka sasa kuna tafsiri zaidi ya 1000 za ugaidi duniani.
Wakati mwingine tafsiri ya ugaidi inatokana na matakwa ya mtu, kikundi au nchi husika.
Kwa mfano mtu mmoja anaweza akatafsiriwa kuwa ni gaidi kulingana na mtazamo wa watu fulani. Lakini mtu huyo huyo akatafsiriwa na watu wengine kama mkombozi wa jamii ya watu fulani wenye malengo na mtazamo unaofanana.
Wakati wa utawala wa kibaguzi wa Makaburu wa Afrika Kusini, walimtafsiri Nelson Mandela kama gaidi, wakati kwa upande wa Waafrika alikuwa ni mkombozi/mpigania uhuru.
Kwasababu wao ndo waliongoza Kwa ugaidi ....kama ambavyo zamani mshamba Ni msukumaZamani kidogo gaidi ilikuwa lazima awe mwarabu au muislsm
Hiyo ya mshamba kuwa msukuma ni mpaka leoKwasababu wao ndo waliongoza Kwa ugaidi ....kama ambavyo zamani mshamba Ni msukuma
Zamani kidogo gaidi ilikuwa lazima awe mwarabu au muislsm
Bila kusahau midevuZamani kidogo gaidi ilikuwa lazima awe mwarabu au muislsm
Jadili mada siyo mtu. Mtu atatiwa hatiani kwa hoja ambazo mleta mada kailetaHabari wana jamvi ?
Nimekuja kuuliza wajuzi juu ya neno hili. Maana siku mbili hizi limekuwa gumzo sana na kuonekana ya kuwa kuna mtu kama ameonewa kuitwa au kutuhumiwa kwa ugaidi.
Nataka nijue wanao pinga hilo wanazingatia maana ya ugaidi au ? Kwanini huyo aliyetuhumiwa juu ya ugaidi aonekane amedhulumiwa ?
Nini maana ya UGAIDI ?
Chanzo cha ugaidi ni nini?Ugaidi kwa maana nyepesi ni kitendo kinacholenga kusababisha hofu kwa raia, serikali au jamii ya kimataifa na vyombo vyake.
Sheria yakudhibiti na kupambana na ugaidi Tanzania imetoa maana pana ya ugaidi katika kifungu cha nne.
Kosa la ugaidi linajumuisha watendaji, wasaidizi na wadhamini wanaosaidia magaidi. Kifungu cha 4 mpaka 10 vinachambua kwa undani mambo yanayopelekea jinai ya ugaidi.
Baadhi ya mambo yanayoweza kuangukia katika ugaidi ni kama ifuatavyo;
I. Kufanya kitendo au shambulio linaloweza kuleta uharibifu mkubwa kwa nchi au taasisi za kimataifa
II. Kwa kutumia nguvu kuilazimisha serikali kufanya Jambo fulani kwa nguvu bila matakwa ya serikali yenyewe
III. Kutumia silaha au milipuko kwa lenga la kutisha umma wa watanzania.
IV. Kuteka viongozi wakuu wa kiserikali kwa shinikizo fulani
V. Kula njama, kusaidia, kuwezesha magaidi kufanya ugaidi.
VII. Kumiliki vifaa au dhana, namba, michoro au ramani ya eneo lililolindwa na kutumia vifaa hivyo kwa lengo la ugaidi etc
Kosa la ugaidi linafanana sana na kosa la uhaini ambapo kwa pamoja makosa haya adhabu yake ni kifo au kifungo cha miaka kadhaa kutokana na namna ya ushiriki katika uhalifu huu.