Ugaidi dili mpya ya kuwaandama waislamu?

Ugaidi dili mpya ya kuwaandama waislamu?

dostum

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
215
Reaction score
111
victor-arusha.jpeg


Anaitwa Ambrose Victor Calist ambae ndie aliyekamatwa baada ya kutokea mripuko wa bomu katika Kanisa Catholic La Olasiti Mjini Arusha, Tarehe 5 May 2013. Bomu hilo la kivita liliua watu wa tano na kujeruhi 60 (sitini),ilikuwa ni siku ya ufunguzi wa Kanisa hilo.

Kukamatwa Kwa Victor kulitokana na watu kumuona akitupa kitu kilichoripuka akiwa anaendesha Pikipiki. Amefikishwa Mahakani mara moja au mbili na mpaka leo kimyaaa.Hajuulikani Victor yuko wapi, kesi yake imefikia wapi na hakuna taarifa zinazotolewa kuhusu yeye.
Ilikuwa ni Juni 15, 2013 katika viwanja vya Soweto mkoani Arusha,mripuko wa bomu ulipotokea katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na kusababisha vifo vya watu wanne na kujeruhi zaidi ya 60.

Jeshi la Polisi lilishindwa kuwakamata wahusika huku viongozi wa Chadema wakidai kuwa na ushahidi wa picha za video zinazowaonyesha maofisa wa polisi kuhusika.

Ushahidi wa Chadema kuwa afisa wa Polisi anahusika hatukuusikia tena, hatukujua nini kinaendelea.Ushahidi huo hadi leo hakuna ajuwaye Jeshi la polisi limeutumiaje katika kumkamata huyo afisa ambaye video ilimuonesha kuhusika.
Wiki iliyopita nikiwa napitia kurasa mbali mbali katika mitandao kuisoma hii habari, moja ya taarifa iliyonishangaza ni taarifa niliyoipata kupitia page ya facebook ya EATV inayosomeka :

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limetaja majina ya watuhumiwa 19 wanaodaiwa ndio kuwa ndio vinara wa mtandao wa matukio yote ya miripuko ya mabomu
​
Vile vile nalo gazeti la Mwananchi la Ijumaa,Agosti 1 mwaka huu linatueleza kuwa:
Hatimaye Polisi limewakata watu 12 likiwatuhumu kuhusika kuushambulia kwa bomu mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) uliofanyika kwenye Viwanja vya Soweto jijini hapa.
​
Katika Gazeti la Mtanzania na Waandishi Eliya Mbonea na Janeth Mushi, Arusha linasema gazeti hilo: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Lebaratusi Saba aliwataja watumiwa waliokamatwa na matukio waliyohusika nayo kama ifuatavyo:-

Kanisa la Olasiti
Aliwataja waliohusika na tukio la ulipuaji wa bomu kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasiti jijini Arusha Mei 5, mwaka 2013, kuwa ni Yusuph Huta (30), Ramadhan Waziri (28), Abdul Humud (30) na Wakala wa Mabasi ya Mohamed Trans (ambaye amefikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na bomu la Mgahawa wa Vama).

Wengine ni Jafar Lema (38), ambaye alikuwa Imamu wa Msikiti wa Quba (ambaye amefikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na bomu la Mgahawa wa Vama), Said Mohamed Temna (42), (ambaye amefikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na bomu la Mgahawa wa Vama).
Wengine ni Kassim Ramadhan (34), Abashar Omar (24), ambao ni madereva bodaboda, Abdulrahman Hassan (41), pamoja na mfanyakazi wa Benki ya Stanbic Arusha.

Wengine ni Morris Muzi (44), mkazi wa Kalinzi mkoani Kigoma, Niganya Niganya (28), mkazi wa Businde Ujiji Kigoma, Baraka Bilango(40), mkazi wa Kalinzi Kigoma na Hassan Omar (40).

Mripuko mkutano wa Chadema
Alisema Jeshi la Polisi limewanasa watuhumiwa kadhaa ambao walihusika katika tukio la uripuaji wa bomu Juni 15, mwaka jana kwenye mkutano wa kampeni za udiwani za Chadema.

Watuhumiwa hao ni Yusuph Huta (30), Abdul Humud (30), pia wapo Said Temba (42), ambao wamefikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na bomu la Mgahawa wa Vama na Jafar Lema (38).
Wengine ni Imamu wa Msikiti wa Quba, Sheikh Abuu Ismail, ambaye amefikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na bomu la Mgahawa wa Vama. Wengine ni Kasim Ramadhan (34), ambaye ni dereva wa bodaboda, Ramadhan Waziri (28).

Alitaja watuhumiwa wengine kuwa ni Abashar Hassan Omar (24), Abdulrahman Hassan (41), mfanyakazi wa Benki ya Stanbic Arusha, Morris John Muzi (28). Wengine ni Niganya Niganya (28), Baraka Bilango (40) na Hassan Omar (40).

Kila mtu kasoma vizuuri majina ya wahusika wa bomu la Olasiti, lakini jina la Ambrose Victor Calist limekosekana. Pia mripuko wa Soweto kamanda Lebaratus Sabas alisema kuwa waliotiwa mbaroni wanaotarajiwa kufikishwa mahakamani, hakuna ofisa wa polisi hata mmoja. Kisha Kamanda huyo akadai kwamba Chadema iligoma kutoa ushahidi huo wa picha za video.

Kama Chadema hawana ushahidi basi washitakiwe kwa kulisingizia uovu Jeshi la Polisi. Mbona hata hilo halifanyiki? Wapelekeni mahakamani wale wanaosema mumwehusika. Ili nasi tuamini kweli hamujahusika.

Huenda kuna kamchezo tu kanachezwa-chezwa, atiwe matatizoni asiyehusika. Na waliohusika wapate kujisafisha. Unadhani Polisi kama hajahusika wangekubali kuchafuliwa ?Nina uhakika kama hawajahusika wangekuwa wameshaishitaki zamani Chadema.

Nani anakubali kuchafuliwa? Nani atakubali kutiwa dosari isiyomuhusu? Wangekubali kweli kuzuliwa? Wangekuja na mambo meengi mno, “ohh Chadema tunawashtaki kwani wanaondosha uwaminifu wetu kwa raia”. Lakini sijalisikia hili.

Mbali na matukio hayo ambayo watuhimiwa wa mwanzo walipatikana lakini haijuulikani wameishia wapi, kilchpofanyika na kutafuta watuhumiwa wapya na kuwapachika mzigo.

Hao sasa wamekuwa kama chambo kwani matukio yote hayo sasa wahusika wamekuwa wao na hata yale matukio ya Bomu nyumbani kwa Katibu wa Bakwata, Kumwagiwa tindikali Sheikh Makambawa,Kumwagiwa tindikali Sheikh Mustapha, Tukio la Arusha Night Park, Bomu nyumbani kwa Sheikh Sudi n.k. Matukio yooooote hayo wao ndio wamekuwa wahusika.

Ni kama palikuwa anatafutwa ni nani tumtwike huu mzigo, lakini inavyoonekana wamewapata wa kuwatwika mizigo na kuwakumbizia yoote hayo. Hata ile mizigo ya Maofisa Polisi na mzigo wa Ambrose Victor Calist yote wamebebeshwa wao na wao ndio wahusika. Polisi na Victor siwo tena!!
Hatuingilii masuala yao lakini pia tunayo haki ya kuhoji, uko wapi ushahidi wa video na picha ambao Cahadema walikuwa nao? Yuko wapi Victor mshukiwa wa bomu la Ollasiti?

Aliyefanya uovu achukuliwe hatua lakini asitafutwe mtu asiyehusika akatwishwa mizigo si yake. Kila muovu alipwe kwa uovu wake na mwema asitafutiwe matatizo na kuingizwa katika mambo asioyajua.

Tunaelezwa kuwa Kenya baadhi ya watu walikuwa wanabambikiziwa mabomu na bunduki kisha wanauwawa bila hata ya kufikishwa mahakamani. Musione aibu kusema kuwa aliyehusika bado hatujampata hata kama itachukua miaka mingi lakini musitake kuonekana ni wafanya kazi bora kwa kuwaingiza wasio husika matatizoni.

Mtenda muovu na ahukumiwe kwa uovu wake lakini, wasiingizwe matatizoni wasiohusika. Tusiige mifumo ya wenzetu wa Kenya. Kenya imeanza kuvuruga katika suala la amani kwa sababu za kutaka kuonekana ni wapambanaji wazuri wa kinachoitwa ugaidi. Lakini kumbe wanazidi kuichafua hali ya hewa.

Baada ya kupewa misaada na Wazungu hutafuta watu na kuwabambikizia makosa ya ugaidi ili waletewe misaada zaidi na waonekane ndio anapambana na ugaidi. Tuwe tunajifunza makosa ya majirani zetu sisi tusiyarudie.

Email:rashidalmendhry@yahoo.com
0773526254
‬
 
Tuacha polisi ifanye Kazi same watu wamekamatwa na mabomu uliyaona sasa sijui mnataka safanyeniniii??
 
Ulimwengu wa sasa tulionao. walio na madaraka kwa kawaida inatafuja jamii iliyokuwa dhalili ndiyo inayoibebesha lawama na uchafu woote wakijua hawataweza kujitetea. Jiulize waislam wale wamekamatwa Na mabomu au wamekamatishwa mabomu. Swali je victor ametokomea wapi. Ni Kama kwasasa image iliyopo Ni kuwa kosa la ugaidi wanafanya waislam Tu. Kumbe chadema wanaushahidi kuwa askari nao wanausika.
 
Kwa hiyo ulitaka Victor ahukumiwe kwa kutupa bomu ndio uone ni haki?, mbona hata baada ya Victor kukamatwa bado mabomu yameendelea kurushwa?.

Iko hivi, linapotokea tukio poisi huwa wanakamata mtu wanaemuhisi (suspect) kwa ajili ya upelelezi zaidi. Hata wewe siku ukisikia kuna mtu kauawa nenda eneo la tukio halafu ujifanye kuonesha wasiwasi uone kama polisi hawatakusomba.

Haya mambo tuwaachie polisi, tukijifanya kutetea watu kwa mgongo wa udini basi nchi hii mtu akikamatwa aulizwe dini, akiwa ni mwislam aachiwe, akiwa ni mkristu aachiwe, akiwa ni mpagani afungwe. Acha kuingilia polisi, ama kama unajiamini nenda kawasaidie kuwapa ujuzi ili Victor afungwe
 
Ulishawahi kujiuliza kwanini vikundi vingi vya ugaidi vina majina ya kiarabu?

Anyway, usiwe na wasiwasi, hawa wanaofanya hivyo wanatimiza utabiri wa Yesu. Yataendelea kutokea na lazima unabii utimie
 
Kama chadema wamebundi na uahahidi wa ulipuaji Bomu kwenyemkutano wao na hadi Sasa wamekula gundi huku wengine wakitwishwa mzigo. Kwamantiki hiyo chadema wanafurahia wamaokamatwa waendelee kukamatwa tu.
 
Tunataka tujue kesi ya victor imepotelea wapi
tunataka kujua kwanini kwann matukio haya wanakamatwa waislam peke Yao. Je Ni vita dhidi ya haki au dhidi ya waislam
kwanini kesi hiyo hiyo kiongozi wa kikrito anaachiwa Na wa kiislam ananyimwa dhamana. Mfano kesi ya uchichezi mwanza. Mchungaji kapewa dhamana ustadh kanyimwa dhamana.
tunakumbuka lilipotokea tukio lile la bomu arusha, serikali ikatangaza imekamata waarabu mpakani, lkn mpaka huo huo wazungu hawakukamatwa.
sheikh ponda yeye ndiye aliyejeruhiwa kapigwa risasi, aliyempiga risasi Yuko huru, aliyepigwa ana kesi ambayo ushahidi wake haukamiliki.

hatutaki kuiingilia mahakama lkn navyo vyombo vya sheria visifanye kazi hata kipofu akaona kuwa vinargemea upande mmoja. Tunakumbuka mahakama ilivyotoa hukumu kuwa Ni makosa kwa kiislam kusema yesu si mungu

yako mengi yanoyotufanya tuwe Na wasiwasi kuwa taasisi nyingi za serikali zinaendeahwa Kama vigango.

mifano mingi kina lukuvi nao wanaonyesha chuki Na ubaguzi kweupe kanisani





Kwa hiyo ulitaka Victor ahukumiwe kwa kutupa bomu ndio uone ni haki?, mbona hata baada ya Victor kukamatwa bado mabomu yameendelea kurushwa?.

Iko hivi, linapotokea tukio poisi huwa wanakamata mtu wanaemuhisi (suspect) kwa ajili ya upelelezi zaidi. Hata wewe siku ukisikia kuna mtu kauawa nenda eneo la tukio halafu ujifanye kuonesha wasiwasi uone kama polisi hawatakusomba.

Haya mambo tuwaachie polisi, tukijifanya kutetea watu kwa mgongo wa udini basi nchi hii mtu akikamatwa aulizwe dini, akiwa ni mwislam aachiwe, akiwa ni mkristu aachiwe, akiwa ni mpagani afungwe. Acha kuingilia polisi, ama kama unajiamini nenda kawasaidie kuwapa ujuzi ili Victor afungwe
 
Uchambuzi makini sana na wa mantiki.
Haya masuala yanafanyika na kuna shaka wahusika ni watu wa dola kwa lengo maalum.
Sio kumtetea mtu kwa dini.kama mhalifu akamatwe apelekwe mahakamani tena sio ubabaishaji wa kumpeleka kisutu hali mnajua mahakama hio haina uwezo wa kusikiliza hizo kesi
Huu ni ukiukwaji wa haki za watu.
Kuna jambo sio bure..mfano shekh Farid kwa nini achukuliwe znz na kuja kushtakiwa Dar?
Inawezekana maofisa wetu waitwao kikosi cha kupambana na ugaidi baada ya kufuzu mafunzo mahiri wayapatayo kutoka marekani wamefaulu vyema na kutunukiwa vyetu rasmi vya kikosi cha kupambana na uislam....tuwe makini nchi imeinguliwa tayari..ni adui wa umoja wa watanzania bila ya kujali dini zao.
 
Siwapendi Makafiri mimi... Basi tu!!!
Wewe ni Gaidi.
Huu ndio Ugaidi unaopigwa
vita.
Huyo kafiri amekukosea nini hadi unamchukia bila sababu yoyote ?
Wewe ni mtu wa Dini, kwanini unamchukia kiumbe wa Mungu hali ya kuwa wote mmeumbwa na Mungu ?
Hivi dini yako ndiyo inayokufundisha umchukie mtu ambaye haamimi unacho amini ?
Mbona huyo Kafiri hakuchukii wewe, hatumsikii akikusema vibaya.
Hao Magaidi hii ndio misimamo yao, sio tu wanawachukia wanaowaita Makafiri, bali wanawaua kabisa ili wabaki wao, ambao wanajiona ni wema ktk macho yao wenyewe.
Kumchukia mtu ni sawa na kumuua.
Ninyi ndio mnaochafua Imani za watu.
Ninyi ndio mnaosababisha hao makafiri wasiwaamini hata chembe hata wale waaminifu, kwani baadhi yenu mnaonesha chuki kwao bila sababu.

Ni wajibu wako kumsaidia huyo kafiri ili asiwe kafiri na sio kumchukia.

Wengine hawajawahi kuijua hiyo imani yako, wafundishe kama ni nzuri ili waifuate.

Chuki ya bila sababu kwa hao mnaowaita Makafiri ndio mzizi na chanzo kikuu cha kuwatendea mabaya na kujikuta baada ya kuitwa watu wema mnakuwa wabaya.

Hivyo vikundi vya Kigaidi vinavyoota kama uyoga ukivihoji vinasema vinataka kuwaua Makafiri wote ili wabaki watu safi.

Nakuambia ukweli ndugu yangu mpendwa,
kama una Imani, inayo kuhamasisha kuwachukia watu walioumbwa na Mungu kwa kuwaita Makafiri, na kuwatendea mabaya, ubaya wowote ule,
Tambua kuwa hiyo Imani sio ya Mungu wa Mbinguni,
ni ya mungu wa Kuzimu, Shetani, Ibilisi mkuu, Lucifa.

Mungu wa Mbinguni anawapenda watu wake wote, ndio maana amewaumba. Asingewahitaji asinge waumba, au ange amua kuwaua mwenyewe. Kama alivyowaua watu wa enzi za Nuhu. au wale wa Sodoma na Gomora wa enzi za Lutu.

Mungu aliyeumba Mbingu na Nchi anasisitiza kila kukicha kuwa,

Mpende Jirani Yako Kama Nafsi Yako.

Haijalishi anafanana na wewe au la, haijalishi amekukosea au la, haijalishi vyovyote vile inavyokuwa, haijalishi.

Jitafakari.
Chukua Hatua Bora.
 
Back
Top Bottom