Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 361,076
- 831,698
Tunaishi nyakati ngumu kisiasa... Zilizojaa hofu.. Za kutia shaka na zenye kuleta woga na wasiwasi mkuu... Sononi zimetamalaki nyusoni mwa wengi... Ni hofu.. Hofu.. Hofu....
Kila zama na vitabu vyake... Usemi huu una maana kubwa kuliko tunavyodhani... Kuna zama za vita ya mungu maji ma mungu tufani.. Kuna zama za vita kati ya Mungu moto na mungu hewa.. Kuna vita ya kusi na kaskazi, mashariki na magharibi... Ardhi na mbingu... Vyovyote iwavyo vita zote hizi sababu ni moja.. Kuzimu kunataka kushiba
Chakula cha kuzimu ni damu lakini hapo katikati kuna kizazi cha viumbe vyenye kula nyama... Hivi vinaitwa najisi ya udongo.. Kuna najisi ya ya maji pia.. Kazi yao ni kuharibu... Kuishibisha ardhi miili ya vifo vya kisasi.. Roho zilizolazimishwa kuachana na miili yao
Yanayotokea sasa hayana budi kutokea... Ni zama za vita ya kiroho.... Roho dhidi ya roho... Ni vita mbaya kuliko zote tofauti na vita ya tufani na moto... Vita ya maji na majanga mengine ya asili.... Lakini hivi vita vya roho moja iondoke moja ibaki... Tunaishibisha ardhi visasi
Tumepitia vipindi vya tawala mbalimbali kiuongozi... Kila kipindi kimekuwa na majanga yake katika ulimwengu wa roho.. Majanga ambayo ni matokeo ya vita ya kiroho ili kuzimu kushibe kuneemeke nakuweze kuzaliana na kuongezeka kwa kiwango kile kile cha neema na kuongezeka katika dunia ya binadamu
Ulimwengu unaendeshwa na nguvu roho... Huu ndio msingi wa uhai wa maisha yetu... Tuyaonayo kwa macho ni matokeo ya kile kilichotendeka katika ulimwengu usioonekana
Engine roho inayoendesha dunia ina pande mbili hasi na chanya... Ni lazima hizi pande mbili zipate kiwango sawa cha nguvu ya uvutano ili ulimwengu uweze kuishika.. Ni kama piston kwenye gari... Mjadala wangu unajikita kwenye nguvu hasi... Lakini nitaacha kuzungumzia sehemu nyingine ya dunia.. Nitazungumzia kipande kidogo cha sehemu ya dunia.. Kipande hicho kinajulikana kama nchi ya Tanganyika/Tanzania
Kufupisha mada na kutokana na makisio ya umri wa wengi humu jamvini nitajadili kuanzia kipindi cha mzee Benjamin Mkapa.... Huyu akiwa na haiba yenye wajihi wa uwalazi ukipenda ita kipara.... Muktadha wa maono ya nguvu yake kiroho kuzimu kukachagua karamu ya chakula cha kafara na huduma katika madhabahu za roho kupitia ajali na majanga ya kiasili... Kiroho inaitwa ni vita ya pande nane za dunia ikizihusisha nguvu zote.. Ni kipindi hiki kuzimu kulikaribia kuvimbiwa lakini bahati mbaya kuzimu hakushibi....
Tukamaliza na Mzee Mkapa.. Tukaja na kaka mkubwa Jakaya Mrisho kikwete... Huyu kapokea kijiti chenye vita ya pande nane za dunia lakini iliyokuwa inaishiwa nguvu na kubaki na vita ya ardhini tu... Hii ni vita ya roho yenye kuhitaji damu na nyama kwa wakati mmoja kupitia uvumbuzi wa kibinadamu.... Vyuma kupitia ajali mbalimbali vimekula na kunywa damu nyingi sana.... Mtakumbuka kipindi kuelekea mwishoni mwa utawala wake... Zile ajali zilikuwa ni karamu ya ushindi na kufunga ukurasa wa vita ya pande nane za dunia
Tuko kwenye nyakati za vita ya damu na nyama.... Kuzimu hakushibi kama wewe usivyoshiba... Kuzimu hakutosheki kama wewe usivyotosheka.... Lakini vita ya zama hizi ni mbaya ni ile ya roho juu ya roho ni vita ya kisasi katili chenye kumea visasi vya kiroho... Ardhi na maji vinashibishwa najisi ya laana za roho zilizotenganishwa na mili yao kwa mateso makubwa...
Kwa mtazamo na jicho la kibinadamu kuna watu watatupiwa lawama... Kiroho ni tofauti... Hatuna budi kuziishi hizi nyakati... Ili kuzimu kuweze kuishi.... Siku hizi hakuna ajali nyingi zinazoondoka na maisha mengi kwa maramoja. Siku hizi hakuna hakuna majanga mengi ya kiasili yanayoondoka na roho nyingi
Kuzimu kunanyonya taratibu kila kinachodonyolewa... Wanaopotea ni wengi sana.. Na wakipotea hawarudi... Lakini pia hukutana na mwisho wao kwa mateso makali.. Ni zama tunazoziishi... Na tunaongozwa na nguvuroho tusiyoweza kuizuia....
Ninapoangalia chaguzi ndogo tu za marudio na damu inayomwagika... Na wale wengine wote wanaopotea wasionekane tena... Na wale wote wanaookotwa tayari wakiwa ni wafu na wale wote wanaotupwa baharini na nyikani... Unapata jibu menu ya kuzimu imegeukia wapi..
Hofu iliyopo ni kwamba binadamu hawezi kula nyama ya binadamu mwenzie lakini kwa ukatili unaoendelea ni sawa na picha husika kwenye hii mada RISE OF THE ROTTEN
Jr
....!!!