Ufunuo: Tanzania yangu ya leo na Ijayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufunuo: Tanzania yangu ya leo na Ijayo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ufunuo wa Yohana, May 15, 2011.

 1. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 35
  Mimi Yohana mfungwa wa Kristo nilipokuwa ktk kuomba niliona yafuatayo kuhusu nchi yangu Tanzania;
  1) Haya uyaonayo leo ktk siasa ya tanzania ni kivuli na mhimu sana kwa mambo makuu yajayo; maandamano na malumbano yanaamusha na kufundisha jamii iliyokosa elimu kwa ajili ya mambo yajayo..... acha yaendelee....maana watu wangu waliokosa elimu ya siasa haitahitaji kwenda chuo au shule kujua haya....acha yaendelee please( kumbuka wiki iliyopita ulipokuwa kijijini bibi yako alikuuliza swali gani kuhusu Dr. slaa na Kikwete? swali ambalo kwa hakika ulikuwa hutegemei kulipata kutoka kwake ambaye hata kusoma hajui ...na safari zingine zote hakuwahi kukuuliza... why only this time? kuna jambo linaendelea ndani ya ufahamu wa watu wangu Tanzania niliowachagua kuishi salama

  Inaendelea muda si punde..................
   
 2. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 35
  2) Baada ya haya uyaonayo atatokea Rais atakayeifanikisha nchi ya Tanzania kuwekwa ktk ramani ya dunia hii ki-uchumi, ki-siasa na ki-michezo
  Niiuliza: Ni wakati gani haya yatatokea? Si muda mrefu,
  Nikauliza tena: mwaka gani? Hakuna haja ya kujua mwaka!
  Nami nikaendelea kudadisi: Je mimi nitayaona haya mabo yakitokea? Ndiyo ktk mwanzo wake utapata nafasi ya kuyaona (kwa sasa mimi nina umri wa miaka 30 na life span ya Mtz 60-70 hivyo unaweja jua ni wakati gani yanaweza kutokea)

  Nikauliza tena: Huyo Rais atakuja na mbinu gani?
  Atatangaza hali ya hatari nchi nzima na kwamba umasikini ndiye adui yenu mkuu na kuhakikisha kila mwanadamu anafanya kazi kwa bidii mchana kutwa na hata usiku.Atahakikisha uzembe haupo na haya ndiyo atafanya;
  a) Atabainisha maeneo yanayofaa kwa kilimo na kuya dedicate kwa watu wasio na kazi mijini na ataboresha sana sera ya kilimo
  b) Atahakikiya hakuna ulevi wa watu kulala baa na baa zitapunguzwa mitaani kwa kuwafutia leseni walio ktk makazi ya watu na muda kukaa baa utapunguzwa
  c) Vijiwe vyote vya kahawa vitafungwa...wataruhusiwa kunywea nyumbani kwao baada ya kazi
  d)Magazeti ya udaku yatafungwa na kuanzishwa magezeti ya kuelimisha watu ktk masuala ya kilimo, ujasiliamali, elimu, michezo, mazingira na afya.
  e) Migodi itaanzishwa kwa ubia na sellikali ikimiliki si chini ya 50%
  Alipofika hapa nikauliza swali: Mpaka wakati huo kutakuwa madini bado yapo? Ndiyo wanayochukua sasa hivi haijafika hata 2% ya madini yote niliyoibarikia nchi yenu Tanzania.
  f) Uteuzi wa watendaji wa serikali kuu (mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi wa makampuni ya umma, wakuu wa vyuo vya umma) watapigiwa kura ya ndiyo au hapana bugeni (wakati huo bunge litakuwa nguvu mno)
  g) Rais atamsimamisha kazi kiongozi yeyote anayetajwa kwa tuhuma za rushwa na mtu au kikundi cha watu na kuamuru uchunguzi ufanyike

  inaendelea punde...........
   
 3. Onambali

  Onambali Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nabii,

  Umetabiri vema.

  Angalia thread zangu za kuwania urais mwaka 2030
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,206
  Likes Received: 3,771
  Trophy Points: 280
  Utabili mzuri sana na wenye maono mema!
   
 5. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 35
  3) Elimu ya ujasiliamali itatolewa kwa wingi zaidi kuanzia vijijini hadi mjini, runinga zitarusha program maalumu kwa wajasiliamali na utumishi bora wa serikali, miziki na maigizo yasiyo na tija itapewa masaa machache kabisa ktk kila runinga irushayo matangazo Tanzania.
  4) Uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo vya kuprocess bidhaa za kilimo utaongezeka ktk kila kijiji na watu watakula chakula chenye ubora na afya zao zitaimprove kuanzia vijijini hadi mijini ...chukula kitakuwepo cha kutosha
  5) Tuta export bidhaa za vyakula ktk nchi jirani zitakazokuwa wakati huo na njaa kubwa kwa bei kubwa sana na uchumi wa nchi utaongezeka kwa 45% kila mwaka. Alipofika hapa nikauliza: Huyu Rais atakwa madarakani kwa miaka mingapi?Atakaa miaka 15. Nikauliza tena: mbona katiba yetu inasema ni miaka max 10? Wananchi watamwongezea muda kutokana na aliyoyafanya
  6) Ataanzisha sports academy maeneo kati ya Morogoro na dodoma itakayochukua wanafunzi 1000 kwa mwaka kuanzia watoto wa miaka 3 hadi 19. itakuwa na viwanja vya mpira vya wazi std 18 wakicheza usiku na mchana. na mtawin w/cup
  7) Umeme utakuwa wa uhakika, atatumia makaa ya mawe kwa kujenga megafactory ya kufua umeme haikuwa kutokea ktk Africa na mtauza

  more tu come........
   
 6. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  haya mi napita mkuuuuu!!!!!!!!!!
   
 7. Tympa

  Tympa Member

  #7
  May 15, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Utabiri huu uliousema, hata mimi nilikuwa nafikiria kufanya hayo mambo(isipokuwa kuwin wcup) endapo baadaye nitakuwa raisi wa hii nchi.
   
 8. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 35
  Watu watajawa na furaha, watapendana, watatambuliwa kwa upendo wao kimataifa, watapenda na kujivunia utaifa wao, watategemewa africa na duniani kwa kuleta amani na haya ndiyo matokeo yake:-

  1) Viwanda vya magari, mitambo, mashine mbalimali vitabuniwa na watanzania na kutengenezwa kupitia vitengo vya utafiti wa sanyansi na vyuo vikuu ( mtaona gari brand yaTZ)
  2) Afya zao bora kutokana na upatikanaji wa chakula kilichotengenezwa kwa ubora na kwa wingi watafikiria na kubuni mipango kabambe ya kukuza uchumi wa nchi yao
  3) Rushwa mtaisikia kwa majirani zenu tu
  4) Umalaya hautakuwepo tena, watu watajali kazi kazi tu wadada/kaka wamiliki wa makampuni yanayowekeza hadi nchi jirani wataongezeka sana
  5) Miundo mbinu itaboreshwa sana hakuna ajali za mara kwa mara wala foleni, Barabara kutoka dar hadi morogoro itakuwa na njia 8 (4 zinakuja na 4 zinaenda) moro dodoma 6, moro mbeya 4, chalinze Arusha 4. dodoma mwanza 4 na nyingine zitakuwa rami zote.
  6) mji wa Dar utabakia mji wa biashara na wizara zote na office za siasa zote makao makuu yatahamia Dodoma hata Ikulu. barabara zitapanuliwa na kuweka flyover kila janction kiasi kwamba mtu anaweza kudrive kwa spidi ya 120km/h akitokea kimara hadi akiba na spidi ya 60 akifika posta bila kusimamama
  7) Mshahara kima cha chini kitakuwa $1800 na per capital income itafika $12,000 ktk utawala wake na itazidi kuongezeka ktk tawala zitakazofata baada yake.

  Niliuza swali: Majirani zetu si watavamia ajira zet zikiwa na mshahara mnono kuliko za kwao? Aha! yes, kwanza kabisa akiingia tu atatoa vitambulisho kwa kila raia na kila mwajili atatakiwa apate copy ya kitambulisho cha mtu anayetaka kumwajili na selikali atapitia kuhakiki.

  Na hayo ni machache ktk mengi mazuri niliyoona
  Nilijisikia faraja sana na ninaamini itakuwa
   
 9. Tajy

  Tajy JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenena
   
 10. Onambali

  Onambali Member

  #10
  May 15, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ee Baba wa Mbinguni,

  Naomba iwe hivyo kama mnenaji huyu alivyosema.

  Sema tu Ee Bwana maana mimi mtumishi wako (Onambali) nitakusikia. Pasipo maono watu huangamia. Ee Mungu uliyefunua matumizi sambamba ya kitabu cha Ufunuo wa Yohana kupitia kwa huyu mtu aliyejiita Ufunuo wa Yohana, naomba umjalie aione nchi saswa na haya anayosema.

  Hayo ndiyo nitakyoyafanya Ee Bwana Mungu kwa uwezo wako, itakapotimia hapo mwaka 2030, utakaponipa hekima ya kuongoza taifa lako hili la Tz
   
Loading...