kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,686
KWANZA kabisa namshukuru Mungu, muumba wa mbingu na ardhi kwa kunijaalia uhai, afya njema pamoja na nguvu za kutosha kiasi cha kuniwezesha kutimiza majukumu yangu ya kila siku.
Wiki iliyopita nilielezea kuhusu namna unavyoweza kuishi ukiwa umeishiwa, ni matumainiyangu kwamba mlijifunza mengi.
Wiki hii nitazungumzia mada inayohusu ufujaji wa pesa, tabia ambayo imekithiri kwa baadhi ya watu katika jamii yetu.
Siku zote matumizi ya pesa hayawezi kuwa sawa baina ya mtu na mtu ama familia na familia. Si rahisi mtu anayepokea mshahara wa shilingi milioni moja akawa na matumizi sawa na mtu anayepokea laki moja. Lazima kutakuwa na tofauti.
Lakini je, mwenye kipato kikubwa anapokuwa na matumizi makubwa ni sahihi mwenye kipato kidogo kusema mtu huyo anafuja pesa? Kama sio, kufuja pesa ni kupi?
Kufuja pesa ni kutumia pesa bila mpangilio tena wakati mwingine katika mambo ambayo hayana maana.
Ifahamike kwamba ufujaji wa pesa hauko katika anasa tu kama vile ulevi, kuhonga na mambo mengine kama hayo, bali pia katika mambo ambayo kimsingi hata yakikosekana katika maisha ya binadamu hayawezi kuleta athari.
Tafiti mbalimbali zimedhihirisha kwamba wengi ambao hutumia pesa ovyo ni athari za malezi waliyoyapata kutoka kwa wazazi wao tangu utotoni. Mzazi ndiye anayeweza kumfundisha mtoto kuwa ama kutokuwa na nidhamu katika pesa.
Unaweza kukuta watu wawili wanafanya kazi moja na wanalipwa mshahara sawa, lakini mmoja akawa na matumizi ya ovyo na kujikuta akiumaliza ndani ya siku chache na kulazimika kuanza kukopa ili kuweza kusogeza siku.
Kama nilivyoeleza hapo awali kwamba matumizi baina ya mtu na mtu hata siku moja hayawezi kuwa sawa, lakini ni ukweli usiofichika kwamba wapo wanaosifika kwa utumiaji mbaya wa fedha, athari ambayo inatokana na malezi kutoka kwa wazazi wao.
Ndiyo maana linapozungumziwa suala la utumiaji mbovu wa fedha kwa mtu fulani lazima historia itahusishwa katika hilo. Upo uwezekano mkubwa kwamba enzi za utoto wake wazazi wake walikuwa wakimpa pesa nyingi bila kujali mahitaji yake na kulazimika kuzitumia ovyo huku wazazi wakionesha kutojali. Katika mazingira kama hayo ni wazi kwamba athari hii itakuja kuonekana ukubwani.
Kitendo cha baadhi ya wazazi kuwapatia watoto wao fedha nyingi kama sehemu ya matumizi yao ya kila siku ni kuwalazimisha wazitumie kwa fujo kwani watakuwa wanajua kesho watapewa nyingine.
Mtoto kuanzia utotoni anatakiwa ajue ugumu wa kupata pesa, ajue kwamba bila kusoma, kufanya kazi ama kujishughulisha kwa namna yoyote hawezi kupata pesa. Unapompatia fedha mwanao kila anapohitaji bila kuhoji juu ya matumizi yake ni kumfanya aone kwamba hakuna ugumu wowote kupata pesa mazingira ambayo kisaikolojia yanaweza kumuathiri.
Hata kama pesa ipo lakini si wakati wa kumzoesha mtoto utumiaji wa ovyo wa pesa. Mpatie mahitaji yake muhimu lakini usimpe pesa nyingi kiasi cha kumlazimisha atumie atakavyo kwa sababu zipo.
Ninachosisitiza ni utumiaji mzuri wa pesa na wala sisemi uwe bahili, mgumu wa kutoa, mgumu wa kusaidia, hapana! Tena kwa kuitumia pesa yako katika kuwasaidia ambao hawajiwezi hata Mungu anakujaalia urahisi katika kupata pesa tofauti kabisa na unapoitumia pesa unayoipata katika starehe zisizo na msingi.
Lazima nidhamu itumike katika kutumia kila shilingi unayoipata laa sivyo mwisho wa siku tunaweza kujutia pesa ambazo tumezitumia ovyo kwa kufurahisha nafsi zetu ama kujipatia umaarufu.
Kwa kuzingatia hilo ndio maana katika umri mdogo mtoto anatakiwa kufundishwa nidhamu ya pesa, utumiaji makini wa pesa.
Kushindwa kwa mzazi kufanya hivyo ni kumtengenezea mtoto mazingira ya kuja kushindwa kutumia vizuri pesa zake ambazo atakuwa akipata.
Kwa hiyo kama hutakuwa makini na kila shilingi unayoipata leo, fahamu kufanikiwa katika maisha yako ni kitendawili.
GPL