Ufugaji wa Kware kwa ajili ya Nyama

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,912
Watu wengi wakisikia Kware moja kwa moja picha inayo kuja ni ya mayai kwamba yanatibu mara ukimwi mara Kisukari.

Ila ukweli ni kwamba wengi hawakwenda mbele zaidi kwenye matumizi mengine kama nyama au mayai kukaanga.

Kware wanaweza tumika kama mboga au kitoea na wakawa mbadala wa vitu kama samaki au nyma ya Ng'ombe au kuku.

Ndani ya Familia wakishika kware 4 wakachinja siku inaisha, inapikwa tu Ugari then kware wanakaangwa na maisha yanasonga mbele.

Hawa ndege wengi hawakufikia kula nyama yake, kware wana nyama tamu sana asikuambie mtu.

Kware ukitaka kuwafuga kwa ajili ya nyama ni kufuga wengi sana, sio kware 50.

Kuna Breeds kwa ajili ya nyama.
1. Giant Quils au Goliath kama wanavyo waita.
Hawa hifikia gram 500.

2. Kuna Jumbo Quils
Hawa hufikia gram 300

3. Kuna hawa wa kawaida ambao ndo wale tulio wafuga enzi zile hawa hufikia gram 200 au 250.

Ukiweza kupata Giant quils basi unaweza fanya kazi kubwa sana.

Shida kuu ni kufutana kama nyumbu na anavyo tumbukia mmoja basi wote wanatumbukia.

Nyakati hizi ubunifu unahitajika sana kuliko kufuatana fuatana kama kumbikumbi, tunahitaji kuumiza sana vichwa na kuwaza beyond.
FB_IMG_1589989765048.jpeg
FB_IMG_1589568826723.jpeg
FB_IMG_1589568761218.jpeg
FB_IMG_1588057833911.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawaruki hao? Kama wanaruka vipi watarudi jioni au ndio ntolee?
 
Hawa ndio mh aliwapima korona? Picha za walio hai wanaonekana waduchu ila walinyonyolewa wanaonekana wakubwa
 
Hawa ndio mh aliwapima korona? Picha za walio hai wanaonekana waduchu ila walinyonyolewa wanaonekana wakubwa
 
Mkuu una tengeneza soko, na pia huwezi kuwa na soko bila mzigo, ujue vitu kama hivi haviuliziwi kwa sababu havipo au havipatikani, ila ukaanza wewe kuchinja na kupack na kuuza utauza sana na hawatatosha, mimi nilishindwa kwenye Oda ya Nyama yake nikaacha kwa muda make nilianza kuchinja nikiwa na kware 180 nikakuta sitaweza na wataisha hadi wa mbegu.

So create awareness,
Soko lake likoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom