Ufisadi Zanzibar (Corruption in Zanzibar)

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,016
View attachment 309363GPS data zinasoma kwamba kuna meli inayoitwa POSCO PLANTEC 13SV01, IMO No. 9708485, Call Sign 51M254, ambayo katika database ya AIS (Automatic Identification System) inaonekana kama MAPINDUZI II, iko Zanzibar kama inavyoonekana katika picha.

Hii ina maana kwamba katika database za Maritime, bado inaendelea kujitokeza kwa jina lake la asili. Sisi walipa kodi wa Zanzibar tuna haki ya kuhoji kama kweli meli ni mpya au reconditioned.

Tukumbuke kuwa IMO number haiwezi kubadilika, hata meli itakapobadilishwa jina, mmiliki au kampuni kwa sababu ni nambari inayotumika kwa sababu za kiusalama na kuondosha udanganyifu katika soko la Marine. IMO ya Mapinduzi II ambayo imechorwa ubavuni, nyuma upande wa kulia ni 9708485. Namba ile ile kama ilivyokuwa katika registration ya jina la POSCO PLANTEC 36SV01.

Tunataka kuamini kwamba ni mpya, lakini hali ya meli yenyewe na information zinazojitokeza zinaendelea kutusuta kwamba ni kinyume chake.

Serikali inapaswa kuliangalia hili kwa jicho pana hasa ikizingatiwa imetumia pesa nyingi sana (dola za Marekani milioni 30.8) na kama ikigundulika kumefanyika ufisadi, basi wahusika wachukuliwe hatua haraka kwa style ya Rais Magufuli.

Wakaguzi wa nje wa Serikali wapo (nitatoka likizoni ikibidi) na wana taaluma ya kutosha katika masuala ya procurement. Watumike hawa kufuatilia hili.

#MagufulificationIsRequired #tusimezeeubadhirifu
 
Attachments

  • 1449344081555.jpg
    1449344081555.jpg
    5.6 KB · Views: 801

Kwani magufuri ana pia uwezo wa kuingilia mambo ya zanzibar?
 
Hapa sasa ndo ukawa utaiona role yao ya kuwachangamsha watawala. Ukawa wanahitajika sana kuwafanya hawa watu active
 
Wazanzibar ni watu wa ajabu sana, wao kila kitu ni siasa za kibaguzi. Ukute watabebana kwenye hili, licha ya kujua kuwa ni hasara kwa Taifa.
 
mengine msaidie kuondoa ufisadi kwa mikono yenu rais wa jamhuri hatafanya kila kitu!! Toa taarifa za kiintelijensia ili kurahisisha kukamatwa kwa mafisadi!!!!!
 
Balozi Seif Ali Idi ndie muhusika wa hiyo meli,aje atuambie ni mpya au kongwe,ufisadi kama huu unanikumbusha enzi za rada.
 
http://www.marinetraffic.com/ais/details/ships/shipid:3532952/mmsi:677015400/imo:9708485/vessel😛OSCO_PLANTEC_13SV01
 
Wizi kila mahali alafu ubaya zaidi Zanzibar ni vigogo 100%
 
Wazanzibar ni watu wa ajabu sana, wao kila kitu ni siasa za kibaguzi. Ukute watabebana kwenye hili, licha ya kujua kuwa ni hasara kwa Taifa.

Mkuu hoja yako inasikitisha sana!
Ina maana hujui kuwa uozo uliopo Tanganyika ni matunda ya kubebana?
 
Najaribu kufuatilia kujua imeundwa mwaka gani, lakini mpaka sasa research zangu sijapata hio kitu
Kuna mtu anafanya kazi kwenye hiyo meli kasema ni ya mwaka1976
 
Balozi Seif Ali Idi ndie muhusika wa hiyo meli,aje atuambie ni mpya au kongwe,ufisadi kama huu unanikumbusha enzi za rada.
Wizara ya miundombinu ilikuwa inaongozwa na Waziri toka CUF!
 
Kwani magufuri ana pia uwezo wa kuingilia mambo ya zanzibar?

Magufulification ni process inayoweza kutumiwa popote ulimwenguni kwani Magufulifiation ni processs si mtu. Wenye kujua kunyambua maana ya muagufulification watiririke.
 
Back
Top Bottom