Ufisadi waitikisa Wizara ya Kilimo

Jan 23, 2011
62
13
Ufisadi waitikisa Wizara ya Kilimo
• Wabunge washtukia mabilioni ya matrekta kuchezewa

na Bakari Kimwanga


amka2.gif
UFISADI ndani ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika umeendelea kuidhohofisha serikali ya Rais Jakaya Kikwete ambayo bado inaandamwa na tuhuma nyingi za ufisadi.
Jana wabunge wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) walieleza kuwapo kwa ufisadi mkubwa katika wizara hiyo nyeti kwa maendeleo ya nchi hasa katika eneo la ugawaji wa pembejeo za kilimo na ununuzi wa matrekta madogo aina ya Power Tiller.
Ufisadi mkubwa ndani ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ulielezwa jana katika kikao cha pamoja kilichofanyika ofisi ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam, kati ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na wataalamu wa wizara hiyo chini ya katibu wao mkuu, Mohamed Muya.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, John Cheyo, alisema kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wizara ya Kilimo imekuwa ikipata hati chafu kwa miaka miwili mfululizo hali inayopelekea kujenga shaka kwa watendaji wa wizara hiyo.
Alisema kwa mujibu wa ripoti hiyo ya CAG imebainika zaidi ya sh milioni 135 za vocha za pembejeo za kilimo zimeliwa na kutowafikia walengwa hali inayoonyesha dhahiri kutokuwepo kwa uaminifu kwa waliokabidhiwa kusimamia ugawaji huo kwa mujibu wa sheria.
Wajumbe wa kamati hiyo walibainisha kuwa kuna ufisadi umefanyika katika mradi wa matrekta madogo Power-Tiller uliogharimu bilioni 13.
“Leo zimetengwa bilioni 13 ili kununua PowerTiller kama zingekuwa fedha zako za mfukoni ungefanya matumizi haya, lakini bado kuna mchezo mchafu unaofanywa na watu waliopewa kusimamia tenda hizi …sasa basi hatuhitaji tena kamati yetu kusikia PowerTiler kwani haziwanufaishi wakulima wa kawaida.”
“Kamati hii inaona huu umekuwa ni mradi na dili kwa wakuu wa wilaya, makatibu tarafa na hata watendaji wa vijiji na kuacha wakulima wa chini vijijini wakiendelea kuteseka huku wizara inaangalia bila kuchukua hatua za kisheria, hivyo kamati yetu tunasema sasa vitendo vya wizi basi,” alisema Cheyo.
Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ali Kessy Mohamed, alisema toka serikali ilipoanzisha mradi wa kununua powertiller nje ya nchi kumekuwa hakuna manufaa kwa wakulima na hazifai kwa matumizi wala kubebea abiria na mizigo.
Alisema kwa mujibu wa ripoti hiyo inaonyesha baadhi ya maofisa wa Wizara ya Kilimo waliingia mkataba na moja ya kampuni ambayo ilionyesha kutengeneza powetiller lakini zikiwa chini ya kiwango na kutofaa kwa matumizi ya kilimo nchini.
“Tunahitaji kujua hapa inaonyesha kampuni ya Confee ambayo haijasajiliwa na hata ilipofuatiliwa nchini Afrika ya Kusini nako haijasajiliwa, je ofisa aliyeingia mkataba huu hadi sasa amechuliwa hatua gani na wizara hii?” alihoji mjumbe huyo.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Zainabu Vullu, kitendo cha halmashauri nchini kununua powertiller huku tayari kukiwa na bajeti maalum iliyotengwa na wizara kwa ajili hiyo, kinaonyesha kuwapo kwa ufisadi.
“Tunahitaji kufahamu, je halmashauri kutenga fedha na kununua powertiller ni fedha zao au ndio hizi za wizara na kama ndio hivyo hakika haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma, lakini bado hadi sasa hakuna tija kwa powertiller zaidi ya kutumia njia ya wanyama kazi katika ulimaji wa mazao nchini,” alisema Vullu.
Akijibu maswali hayo huku akijikanganya katika majibu yake ya msingi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mohamed Muya, alisema pamoja na kuwepo hali hiyo bado wizara yake inajitahidi kutumia njia mbalimbali ili kuweza kukabiliana na hali hiyo.
Alisema mmoja kati ya maofisa wa wizara hiyo walioingia mkataba na moja ya kampuni za kuingiza powertiller nchini hivi sasa amestaafu kazi kwamba suala hilo watalifikisha mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
Hata hivyo, majibu hayo yalipingwa waziwazi na wajumbe wa kamati hiyo na kusema kuwa katibu huyo amekuwa akifanya kazi kwa kubahatisha hali inayojenga mashaka kwamba hamsaidia vizuri Rais Kikwete.
Kutokana na ufisadi huo, kamati hiyo iliitaka wizara kusitisha uagizaji wa powertiller na ihakikishe inafuata maagizo ya kamati hiyo na kuwa na hati safi katika mahesabu yake.
Katika hatua nyingine kamati hiyo iliitaka wizara kurejesha fedha za upimaji wa ardhi kwa ajili ya mashamba ya kilimo zipatazo sh milioni 800, walizotoa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. souse Tanzania daima.Usually
when people are sad they don't do anything they just CRY over their
condition but when they gel Angry they bring about a change" (MALCOLM X)

.
 
Fedha zilizotumika kununulia powertiler katika halmashauri ni tofauti na hizo zilizotengwa na wizara. Katika Wilaya niliyopo ilibidi realocation ifanyike ili kukidhi agizo la Mheshimiwa sana... PINDA! Halafu watumishi wa Halmashauri kwa matatizo hayohayo wameadhibiwa na kamati ya mahesabu ya serikali za mitaa (LAAC). Lakini sijaona adhabu yoyote waliopewa watumishi wa Wizara husika??? Kulikoni???
 
Back
Top Bottom