Ufisadi wa kutisha

Ufisadi wa kutisha

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
Benja%20-Majura-0ctober22-2014.jpg

Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu, Benja Majura

CAG afichua Sh. milioni 214/- zilivyolipwa waliofeli UDOM, IFM na mabilioni yanavyoliwa Tanesco

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inayoishia Juni 30, mwaka 2013, imeanika matumizi mabaya ya fedha za umma.

Ripoti hiyo imehusisha mashirika mengi ya umma yakiwamo Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta), Bodi ya Korosho, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bodi ya Pamba, mgodi wa Southern Paper Mills na Shirika la Ranchi za Taifa (Narco).

Pia, ripoti hiyo ya CAG imeeleza ukaguzi wa fedha za serikali kuu inayoonyesha fedha zilizotolewa na ambazo hazikutolewa na Hazina, Deni la Taifa, misamaha ya kodi kuwa ni asilimia kumi ya bajeti ya mwaka 2012/13 na usimamizi dhaifu wa mikataba.

Kwa mujibu wa taarifa ya CAG iliyowasilishwa jana mbele ya Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), na Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu, Benja Majura, inaonyesha udhaifu mkubwa katika usimamizi wa fedha za umma kiasi cha serikali kupata hati chafu katika hesabu zake.

TANESCO
Ilionyesha kuwa Tanesco ilinunua transfoma mbili kwa gharama ya Sh. bilioni 7.879 kwa kushindanisha wazabuni 12 kwa njia ya zabuni maalum.

Alisema baada ya zoezi la awali la kuwapendekeza washindani kumalizika na kamati kuwasilisha ripoti yake, shirika liliongeza jina la kampuni ya Shadong Taikai Power Engineering, ambayo haikuwa kwenye orodha ya awali ambayo ilipitishwa na bodi ya zabuni ya shirika kuwa mshindi wa zabuni husika.

"Kampuni hiyo haikuwa na sifa, matokeo yake baada ya miezi miwili kabla ya mkataba kuisha muda wake kampuni ililiandikia shirika barua ya kutaka kubadilisha aina ya malighafi ambayo ingetumika kutengenezea transfoma kwa mujibu wa makataba hali iliyopendekeza ongezeko la kazi na bei kwa jumla ya sh. bilioni 3.707," inaeleza taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa Tanesco ilimlipa mkandarasi Ms Consortum Sae Power Lines and Associated Structure Ltd kiasi cha Sh. 2,876,057,520 kama fidia kwa kipindi cha miezi tisa ambacho alikaa bila kufanya kazi yeyote kutokana na mgogoro wa eneo la kupitisha mradi wa laini ya umeme katika maeneo ya Kurasini na Mbagala, Dar es Salaam.

Alisema baada ya mjadala mrefu, kampuni ya MGS International (T) Ltd ililipwa kiasi cha Sh. bilioni 1.638 na kampuni ya MPS Oil kiasi cha Sh. bilioni 1.175 kama fidia ya kuchukuliwa eneo la kupitishia mradi.

Taarifa hiyo imeanisha kuwa gharama hizo zililipwa kutokana na udhaifu wa menejimenti ya Tanesco katika kufanya upembuzi yakinifu juu ya maeneo ambayo mradi ungepita.
"Tumebaini kuwa gharama za mshauri wa mradi ziliongezeka kutoka Sh. bilioni 3.659 hadi Sh. bilioni 5.485 sawa na ongezeko la Sh. 1,825,156 bila idhini ya Bodi ya zabuni," alibainisha.

Pia, taarifa hiyo imebainisha kuwa ukaguzi wa usimamizi wa mikataba Tanesco ulibaini kuwa lilipa gharama za ziada Sh. bilioni 9.5 kwa kampuni za Semco Martine AS na Rolls Royce Maritime AS.

"Malipo haya yalitokana na mapungufu ya menejimenti katika kufanya upembuzi yakinifu juu ya dosari za kimazingira katika mradi wa mafuta mazito, ilipelekea kufanyika uopya kwa utafiti ambao ulichelewesha mradi kwa miezi kumi na Tanesco kugharamia kiasi cha Sh. bilioni 9.5," taarifa ya CAG inabainisha.

BODI YA MIKOPO
Taarifa hiyo imeainisha kuwa ukaguzi katika Bodi ya HESLB ulibaini kuwa mikopo ya kiasi cha Sh. milioni 214.5 kilitolewa kwa wanafunzi walioshindwa mitihani na kutoendelea na chuo na wengine waliohairisha masomo.

Taarifa hiyo imezitaja vyuo hivyo na kiwango kwenye mabano kuwa ni Algeria na Cuba (Sh. milioni 132), Chuo Kikuu cha Dodoma ( Sh. milioni 43.9), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ( Sh. milioni 28.9) na Chuo Kikuu cha nchini Urusi (Sh. milioni 9.6).

SOUTHERN PAPER MILLS
Ripoti hiyo imeeleza kuwa Mgodi wa Southern Paper Mills uliuzwa kwa kampuni ya Rai Group ya Kenya kwa bei ya Sh. bilioni 1.68 wakati na thamani yake ni Sh. bilioni 43.68.

"Kwa makubaliano yaliyokuwepo, Sh. bilioni 1.68 zingelipwa wakati wa kusaini mkataba, Sh. bilioni 5.04 zingewekwa kwenye akaunti ya Escrow ambazo mwekezaji angeweza kuzitoa baada ya miaka mitatu na Sh. bilioni 37 zingewekezwa katika kipindi cha miaka mitatu, lakini baada ya uwekezaji huo mgodi umeendelea kumilikiwa na mwekezaji huyo kwa asilimia 100.

VETA
Ripoti hiyo imeonyesha kuwa Chuo cha Ufundi Mpanda kina mashine zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni moja ambazo zimetelekezwa na kwamba menejimenti ya Veta ingepaswa kuweka mikakati ya kuhamisha mashine hizo ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu jinsi ya kuzitumia kulingana na utandawazi badala ya kuzitelekeza.

PRIDE, BENKI YA AZANIA
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa mujibu wa taarifa za msajili wa Hazina mwaka 2008, serikali inamiliki kwa asilimia 100 ya Taasisi ya Pride Tanzania, lakini uchunguzi wa CAG ulibaini kuwa taasisi hiyo ilitolewa kwenye daftari la Msajili wa Hazina bila maelezo ya kina.

Imeeleza kuwa katika Benki ya Azania inamilikiwa kwa asilimia 91 na mifuko ya Pensheni ambayo ni Mashirika ya umma na kwamba hazijawahi kuwasilisha taarifa za hesabu kwa CAG kwa ajili ya ukaguzi.

BODI YA KOROSHO
CAG alisema ukaguzi maalum wa Bodi ya Korosho ulibaini kuwa kiasi cha Sh. bilioni 1.075 kilitumiwa na Bodi hiyo kulipia matumizi mbalimbali ya ofisi ikiwamo mishahara, gharama za matengenezo, ankara za umeme na gharama nyinginezo kinyume cha sheria inayotaka fedha hizo kutumika kwa ajili ya kuendeleza zao la korosho Mtwara.

TANTRADE
CAG amebainisha kuwa katika kipindi cha Agosti na Septemba, 2012, magari 11 yaliyosadikiwa kuwa ni ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade) yalisajiliwa kwa namba binafsi na kwamba hayakupokelewa baada ya usajili na taasisi haikujulishwa.

NARCO
Ripoti hiyo ilibainisha kuwa wafanyakazi wa Narco wamekatwa kiasi cha Sh. milioni 716.238 kwa kipindi cha Juni 1992 hadi Julai 2012, makato ya kodi na mifuko ya hifadhi ya jamii, lakini hayakupelekwa kwenye mamlaka husika kama TRA, NSSF, PPF kwa usahihi na kwa wakati.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Narco haikuwa na udhibiti mzuri wa fedha kwa kuwa kiasi cha Sh. milioni 392.911 hazikupelekwa benki na kutumika kwenye matumzi mengine kinyume cha sheria.

Ukaguzi huo ulibaini kuwa thamani ya ng'ombe 380 wenye thamani ya Sh. milioni 123.806 wa mradi ambao bado hawajauzwa ilikuwa ndogo ikilinganishwa na kiasi cha deni la mkopo ambao haujarejeshwa benki na kuiweka Narco katika hatari ya kuuza mali zake zilizowekwa rehani kufidia mkopo wa benki ya CRDB.

BODI YA PAMBA
CAG alisema ukaguzi ulibaini kuwa Bodi ya Pamba ina jengo la ghorofa sita, nne zinatumika na mbili hazitumiki ambazo zingeweza kuipatia kiasi cha Sh. 260,400,000 kwa mwaka.

CHANZO: NIPASHE
 
Nchi inatafunwa na mchwa CCM, dawa ni kuwamwagia mafuta ya taa na .....
 
Ingekua vizuri kama angeandika na majina ya wahusika halafu tuone serikali itachukua hatua gani...
 
Taifa liko hatarini,ni sawa na kuwa katika mazingira ya kivita

Ninalaani vikali hatua ya IMF kukubali kuikopesha Serikali ya Tanzania ili kugharamia pengo la bajeti ya serikali baada ya wahisani kugomea kutoa msaada.Huu ni unafiki na kutangaza uadui kwa Taifa.No wonder Comrade Hugo Chavez aliwafukuza kutoka Venezuela

Marekani ni mwanachama mwenye hisa kubwa IMF .Marekani wana Sheria inayolinda wapuliza filimbi wanaofichua ufisadi serikalini (Whistle Blower Protection Act) .

David Kafulila ni Whistle Blower kwenye kashfa ya wizi wa fedha za watanzania kutoka ESCROW.Inasikitisha IMF wanasimama na Mafisadi

Eti Hatimaye Serikali imeamua kuomba msaada kutoka Shirika la Fedha Duniani(IMF) kuwakopesha fedha zaidi ili kutekeleza bajeti yake ya mwaka 2014/15 kuziba pengo la nchi wahisani kugomea kutoa fedha takribani Sh.Trilioni 1 hadi pale ambapo ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za serikali(CAG) atakapotoa Ripoti yake baada ya Kashfa ya IPTL iliyohusisha Uchotaji wa Shilingi Bilioni 200 kutoka akaunti ya ESCROW kwa Idhini ya viongozi na watendaji wa taasisi kuu za Serikali.Wahisani wanaamini hili suala ambalo lilihusisha wizi wa fedha za umma linaenda kinyume kabisa na misimamo na ustaarabu wa kisera wa nchi hizo.

Sasa tumefikia pale nilikosema.Kama wanajua wako Clean kwanini CAG asitoe ripoti?Kwanini wameanza michakato ya kukopa badala ya kusubiri ripoti?

Sasa hizo adjustment za IMF ni kama Structural Adjustment Program(SAP) nyingine sio?SAP iliyosababisha uuzaji wa benki ya NBC kwa Bei ya kutupwa na kuua viwanda vya Tanzania .Leo tuna magofu

SAP iliyosababisha Serikali kuacha kutoa huduma kama elimu,afya n.k kwa raia wake.

Nchi imeelemewa na mzigo wa madeni hadi sasa.Wanakopa kwa ajili ya kutumia.Mafusadi waliokwapua fedha za ESCROW wanatuingiza kwenye Mkopo wa Riba.Tunawagharamia sisi ili watoto na wadogo zetu wakose Elimu bure,Afya na wazee wafe mapema kwa kukosa pensheni huku wafanyakazi wakikatwa kodi hadi asilimia 30 ya mshahara wao.

Serikali inakopa wakati hadi mwezi Juni mwaka huu ripoti ndani ya kamati ya Bunge ilionyesha tunadaiwa Sh.Trilioni 29.2 na kwamba Trilioni 8.2 zilikopwa kwa muda wa miezi 7 tu.Ikumbukwe Rais Mkapa aliacha Deni la Trilioni 10 .

Kiwango cha Trilioni 29.2 kilikua kikubwa maana kila Mtanzania angekua anadaiwa sh.600,000.

Sasa mzigo huu unaongezeka zaidi ili kuhudumia bajeti ya sh.Trilioni 19.

Mwanadada Mchumi maahiri wa Zambia Dr.Dambisa Moyo kwenye kitabu chake cha "Dead Aid" alionyesha jinsi ambavyo nchi za Afrika zinavyokopa kutoka Benki ya Dunia na IMF na kuishia kutanua huku wananchi wakibena mizigo mikubwa ya madeni hayo

IMF chombo cha kigaidi,ndio nathubutu kusema Ugaidi wa Uchumi duniani na siku zote kinatumika kuangamiza uchumi wa nchi zinazoendelea kwa kushirikiana na viongozi mafisadi (Ingawa wanajifanya wapinga ufisadi) .

Ni aibu sana wahisani Tanzania wanagomea kuchangia bajeti kutokana na Ufisadi lakini IMF wanakubali .

Ni kwa sababu wanajua wataweka masharti ya kiuchumi yatakayonufaisha na kuwa na ushawishi wa kisiasa nchini na kupoka uhuru wa kijamii,kisiasa na kiuchumi wakisaidiwa na viongozi wezi na wavivu wa kufikiri.

Wezi wanaiba kisha serikali inakopa ili sisi tuje tulipe? Tutafanya Mobilization kwa Watanzania. Serikali hii ifike Mwisho.

IMF wanafurahi maana hawajawahi kuwa na nia njema na Afrika.

No,hatutakubaliana na Upuuzi huu wa watawala wetu hata Kidogo.

Pia serikali kudai kuwa itakopa kutoka Commercial Banks ni upuuzi mwingine. Benki za Biashara zinakopesha kwa Riba kubwa tena nyingi ziko owned na makaburu na raia wa Kigeni.

Pia miradi ya maendeleo itasimama.Taaluma yangu ya Uchumi sijawahi kusoma mahali popote kuwa serikali inaweza kufanya maamuzi ya kijinga namna hii ikaendelea kuwa na uhalali wa kisiasa na kijamii kuwa madarakani mbele ya watu wanaojitambua.
 
Kwa jinsi hii nchi imegawanyika
 
southern paper mills ni mgodi au kiwanda?
 
TANESCO kuna nini?kila siku ufisadi!ni bora hili shirika wapewe ABB Sweden baada ya miaka 3 serikali itakua inapata gawiwo
 
Kwa Tanzania hii siyo habari, habari ni shirika kutobatuliwa na mchwa, mchwa kubatua fedha za serikali siyo habari kabisa.
 
Hesabu za Chadema zimekaguliwa?
Kwa mawazo haya je tutafika kweli?
CDM inakusanya kodi za wananch? na kama wanapewa ruzuku,nani controller wa ruzuku?
kwa nini controller wa ruzuku asisitishe kuwapa ruzuku endapo wanazitumia vibaya?
Ebu tutumie ubongo kufikiri kama kweli ni GT.
 
Hapa wale wa lumumba hutawaona wala hutawasikia na mwingine ni kama huyo anauliza hesabu za Chadema as if hesabu za Chadema ni miongoni mwa kilichoandikwa hapo juu BAK uko wapi aise hebu soma hapa
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
please kama unauchungu na nchi hii naomba usiwe unasoma mambo yanavyo endelea .....
 
Mi nashaur tushike mapanga,mundu,shoka,kisu,mawe,bunduki,sime,acid.....tuvamie ofsi za wapumbavu hawa...tunaanzia gar lake,mpk tunafyeka yeye. It dangerous to feel freedom while u r slave.
 
Benja%20-Majura-0ctober22-2014.jpg

Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu, Benja Majura

  • CAG afichua Sh. milioni 214/- zilivyolipwa waliofeli UDOM, IFM na mabilioni yanavyoliwa Tanesco

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inayoishia Juni 30, mwaka 2013, imeanika matumizi mabaya ya fedha za umma.

Ripoti hiyo imehusisha mashirika mengi ya umma yakiwamo Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta), Bodi ya Korosho, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bodi ya Pamba, mgodi wa Southern Paper Mills na Shirika la Ranchi za Taifa (Narco).

Pia, ripoti hiyo ya CAG imeeleza ukaguzi wa fedha za serikali kuu inayoonyesha fedha zilizotolewa na ambazo hazikutolewa na Hazina, Deni la Taifa, misamaha ya kodi kuwa ni asilimia kumi ya bajeti ya mwaka 2012/13 na usimamizi dhaifu wa mikataba.

Kwa mujibu wa taarifa ya CAG iliyowasilishwa jana mbele ya Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), na Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu, Benja Majura, inaonyesha udhaifu mkubwa katika usimamizi wa fedha za umma kiasi cha serikali kupata hati chafu katika hesabu zake.

TANESCO
Ilionyesha kuwa Tanesco ilinunua transfoma mbili kwa gharama ya Sh. bilioni 7.879 kwa kushindanisha wazabuni 12 kwa njia ya zabuni maalum.

Alisema baada ya zoezi la awali la kuwapendekeza washindani kumalizika na kamati kuwasilisha ripoti yake, shirika liliongeza jina la kampuni ya Shadong Taikai Power Engineering, ambayo haikuwa kwenye orodha ya awali ambayo ilipitishwa na bodi ya zabuni ya shirika kuwa mshindi wa zabuni husika.

“Kampuni hiyo haikuwa na sifa, matokeo yake baada ya miezi miwili kabla ya mkataba kuisha muda wake kampuni ililiandikia shirika barua ya kutaka kubadilisha aina ya malighafi ambayo ingetumika kutengenezea transfoma kwa mujibu wa makataba hali iliyopendekeza ongezeko la kazi na bei kwa jumla ya sh. bilioni 3.707,” inaeleza taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa Tanesco ilimlipa mkandarasi Ms Consortum Sae Power Lines and Associated Structure Ltd kiasi cha Sh. 2,876,057,520 kama fidia kwa kipindi cha miezi tisa ambacho alikaa bila kufanya kazi yeyote kutokana na mgogoro wa eneo la kupitisha mradi wa laini ya umeme katika maeneo ya Kurasini na Mbagala, Dar es Salaam.

Alisema baada ya mjadala mrefu, kampuni ya MGS International (T) Ltd ililipwa kiasi cha Sh. bilioni 1.638 na kampuni ya MPS Oil kiasi cha Sh. bilioni 1.175 kama fidia ya kuchukuliwa eneo la kupitishia mradi.

Taarifa hiyo imeanisha kuwa gharama hizo zililipwa kutokana na udhaifu wa menejimenti ya Tanesco katika kufanya upembuzi yakinifu juu ya maeneo ambayo mradi ungepita.
“Tumebaini kuwa gharama za mshauri wa mradi ziliongezeka kutoka Sh. bilioni 3.659 hadi Sh. bilioni 5.485 sawa na ongezeko la Sh. 1,825,156 bila idhini ya Bodi ya zabuni,” alibainisha.

Pia, taarifa hiyo imebainisha kuwa ukaguzi wa usimamizi wa mikataba Tanesco ulibaini kuwa lilipa gharama za ziada Sh. bilioni 9.5 kwa kampuni za Semco Martine AS na Rolls Royce Maritime AS.

“Malipo haya yalitokana na mapungufu ya menejimenti katika kufanya upembuzi yakinifu juu ya dosari za kimazingira katika mradi wa mafuta mazito, ilipelekea kufanyika uopya kwa utafiti ambao ulichelewesha mradi kwa miezi kumi na Tanesco kugharamia kiasi cha Sh. bilioni 9.5,” taarifa ya CAG inabainisha.

BODI YA MIKOPO
Taarifa hiyo imeainisha kuwa ukaguzi katika Bodi ya HESLB ulibaini kuwa mikopo ya kiasi cha Sh. milioni 214.5 kilitolewa kwa wanafunzi walioshindwa mitihani na kutoendelea na chuo na wengine waliohairisha masomo.

Taarifa hiyo imezitaja vyuo hivyo na kiwango kwenye mabano kuwa ni Algeria na Cuba (Sh. milioni 132), Chuo Kikuu cha Dodoma ( Sh. milioni 43.9), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ( Sh. milioni 28.9) na Chuo Kikuu cha nchini Urusi (Sh. milioni 9.6).

SOUTHERN PAPER MILLS
Ripoti hiyo imeeleza kuwa Mgodi wa Southern Paper Mills uliuzwa kwa kampuni ya Rai Group ya Kenya kwa bei ya Sh. bilioni 1.68 wakati na thamani yake ni Sh. bilioni 43.68.

“Kwa makubaliano yaliyokuwepo, Sh. bilioni 1.68 zingelipwa wakati wa kusaini mkataba, Sh. bilioni 5.04 zingewekwa kwenye akaunti ya Escrow ambazo mwekezaji angeweza kuzitoa baada ya miaka mitatu na Sh. bilioni 37 zingewekezwa katika kipindi cha miaka mitatu, lakini baada ya uwekezaji huo mgodi umeendelea kumilikiwa na mwekezaji huyo kwa asilimia 100.

VETA
Ripoti hiyo imeonyesha kuwa Chuo cha Ufundi Mpanda kina mashine zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni moja ambazo zimetelekezwa na kwamba menejimenti ya Veta ingepaswa kuweka mikakati ya kuhamisha mashine hizo ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu jinsi ya kuzitumia kulingana na utandawazi badala ya kuzitelekeza.

PRIDE, BENKI YA AZANIA
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa mujibu wa taarifa za msajili wa Hazina mwaka 2008, serikali inamiliki kwa asilimia 100 ya Taasisi ya Pride Tanzania, lakini uchunguzi wa CAG ulibaini kuwa taasisi hiyo ilitolewa kwenye daftari la Msajili wa Hazina bila maelezo ya kina.

Imeeleza kuwa katika Benki ya Azania inamilikiwa kwa asilimia 91 na mifuko ya Pensheni ambayo ni Mashirika ya umma na kwamba hazijawahi kuwasilisha taarifa za hesabu kwa CAG kwa ajili ya ukaguzi.

BODI YA KOROSHO
CAG alisema ukaguzi maalum wa Bodi ya Korosho ulibaini kuwa kiasi cha Sh. bilioni 1.075 kilitumiwa na Bodi hiyo kulipia matumizi mbalimbali ya ofisi ikiwamo mishahara, gharama za matengenezo, ankara za umeme na gharama nyinginezo kinyume cha sheria inayotaka fedha hizo kutumika kwa ajili ya kuendeleza zao la korosho Mtwara.

TANTRADE
CAG amebainisha kuwa katika kipindi cha Agosti na Septemba, 2012, magari 11 yaliyosadikiwa kuwa ni ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade) yalisajiliwa kwa namba binafsi na kwamba hayakupokelewa baada ya usajili na taasisi haikujulishwa.

NARCO
Ripoti hiyo ilibainisha kuwa wafanyakazi wa Narco wamekatwa kiasi cha Sh. milioni 716.238 kwa kipindi cha Juni 1992 hadi Julai 2012, makato ya kodi na mifuko ya hifadhi ya jamii, lakini hayakupelekwa kwenye mamlaka husika kama TRA, NSSF, PPF kwa usahihi na kwa wakati.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Narco haikuwa na udhibiti mzuri wa fedha kwa kuwa kiasi cha Sh. milioni 392.911 hazikupelekwa benki na kutumika kwenye matumzi mengine kinyume cha sheria.

Ukaguzi huo ulibaini kuwa thamani ya ng’ombe 380 wenye thamani ya Sh. milioni 123.806 wa mradi ambao bado hawajauzwa ilikuwa ndogo ikilinganishwa na kiasi cha deni la mkopo ambao haujarejeshwa benki na kuiweka Narco katika hatari ya kuuza mali zake zilizowekwa rehani kufidia mkopo wa benki ya CRDB.

BODI YA PAMBA
CAG alisema ukaguzi ulibaini kuwa Bodi ya Pamba ina jengo la ghorofa sita, nne zinatumika na mbili hazitumiki ambazo zingeweza kuipatia kiasi cha Sh. 260,400,000 kwa mwaka.

CHANZO: NIPASHE

Hawa MACCM Mkuu ni sawa na mzoga Mkuu Rocky. Hakuna mwenye akili timamu ambaye anataka kuusogelea mzoga kufanya hivyo itabidi kwanza uminye pua ili kuepukana na harufu mbaya, ndipo chama hiki cha wahuni kilipofikia hivi sasa. Na wenyewe wanalijua hili ndio maana wameamua kubaki madarakani kwa kutumia mabavu, wizi na udanganyifu wa kila aina ili tu waendelee kuiangamiza Tanzania milele.

Hapa wale wa lumumba hutawaona wala hutawasikia na mwingine ni kama huyo anauliza hesabu za Chadema as if hesabu za Chadema ni miongoni mwa kilichoandikwa hapo juu BAK uko wapi aise hebu soma hapa
 
Last edited by a moderator:
Huu nao ni utekelezaji wa ilani wa ccm....serkl sikivu kabisa....wanakula bila kunawa na bado wanajiandaa kuongoza nchi wanayotafuna kila kukicha!!!

Hata kama tungekuwa na sera na mikakati mizuri namna gani...bila kubana matumizi ya hovyo na mianya ya rushwa kama hii....sahau nchi kwenda mbele!!! Mfano..tanesco ambayo imekuwa ikipigiwa kelele kila kukicha bado wapigaji wanaendelea kuchota chao na kusababisha gharama za uwekezaji kuwa juu na kumlemea mtumiaji wa kawaida kabisa.

Huwezi kufikili Taifa ambalo deni lake linakua kwa kasi....ujinga ka huu ungeuona....haya ni maajabu mengine kweny kizazi chetu chini ya uongozi wa hovyo wa kifisadi wa ccm
 
Hawa MACCM Mkuu ni sawa na mzoga Mkuu Rocky. Hakuna mwenye akili timamu ambaye anataka kuusogelea mzoga kufanya hivyo itabidi kwanza uminye pua ili kuepukana na harufu mbaya, ndipo chama hiki cha wahuni kilipofikia hivi sasa. Na wenyewe wanalijua hili ndio maana wameamua kubaki madarakani kwa kutumia mabavu, wizi na udanganyifu wa kila aina ili tu waendelee kuiangamiza Tanzania milele.

Mkuu BAK huu ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama na wanakula bila kusaza maana wanajua mwakani wengine hawatakuwepo tena. Tanesco imefanywa kama shamba la bibi kila mwenye uwezo achukue kile kinachowezekana. Shirika lina wataalam na wazomi walliobonea wanaohitajika kufanya upembuzi yakinifu kwa kila mradi ila shangaa wanafanya upuuzi wao hasara kwa shirika. Zabuni zinapitishwa ila yule mwenye maslahi yake anaona kampuni yake haijapitishwa anaichomeka humo na wala uongozi wa shirika wala menejimenti haijiulizi au kujiuzulu kutokana na hilo
Na bado huu ni mfano mmoja tuu ikija kwenye serikali za mitaa ndio usiombe. Wanatafuna pesa kama hawana akili nzuri au kama hakuna kesho. Nyjmba ya vyumba viwili inatumia Mil 89 na mkuu wa Wilaya ameona na amechefuka tuu sijui amechefukwa kwa sababu mgao haujampitia au amewaonea wivu waliotafuna pesa
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Hawa MACCM Mkuu ni sawa na mzoga Mkuu Rocky. Hakuna mwenye akili timamu ambaye anataka kuusogelea mzoga kufanya hivyo itabidi kwanza uminye pua ili kuepukana na harufu mbaya, ndipo chama hiki cha wahuni kilipofikia hivi sasa. Na wenyewe wanalijua hili ndio maana wameamua kubaki madarakani kwa kutumia mabavu, wizi na udanganyifu wa kila aina ili tu waendelee kuiangamiza Tanzania milele.

Wakati mkuu wa nchi ameshakata tamaa na anafika Ikulu kubadilisha nguo tu amehamishia makazi angani, sasa tutegemee nini kwa watumishi walio chini yake?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hakukosea kabisa Dr Slaa aliposema Kikwete ni Janga la Taifa. Ukiangalia rekodi yake toka aingie madarakani 2005 hadi leo hii ni majanga tu moja baada ya jingine mwaka nenda mwaka rudi.

Wakati mkuu wa nchi ameshakata tamaa na anafika Ikulu kubadilisha nguo tu amehamishia makazi angani, sasa tutegemee nini kwa watumishi walio chini yake?
 
Back
Top Bottom