Ufisadi wa Kutisha kuelekea bajeti ya serikali 2011/2012

mopaozi

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
3,301
520
Wakuu nawajulisha kuwa kuna ufisadi unaoendelea katika wizara, idara na taasisi zote za serikali katika kipindi hiki cha kuelekea bajeti tajwa kwa kisingizio cha kumalizia mafungu ya 2010/2011!

Yaani kuna semina mbuzi zimeanzishwa, kuna safari watu wanapeana ili kupata posho (per diem). Mi hapa nimeunganishwa kwenye semina haina kichwa wala miguu kuna posho zinagawiwa hadi nasikia uchungu.

Kama hali ndiyo hii basi watz wataendelea kuwa katika hali ngumu ya maisha. Kwanini haya mafungu yaliyobaki yasiunganishwe yote yakapelekwa kwenye shughuli za maendeleo kama kweli tuna nia ya dhati ya kuwasaidia watz badala ya kuendekeza ukware wetu!!!
 
Pole ndugu na asante kwa kutujuza ila kwa taarifa yako bila magamba kuwa nje ya ring hakuna linaloweza kufanyika
 
Sio huko tu, huku Arusha kuna tasisi moja ya uma wanapeana per diem za kufa mtu, eti wameandaa semina ya kufundishwa jinsi ya ku log in and kulog out kwenye mtandao wa internet.

Cheki hiyo
 
ile ni budget ama utumbo? eti 10 bilions makarabati ya ikulu wkt maendeleo 2 bilions ndio zimetengwa, hovyo sana!
 
Semina yetu tumeambiwa ni elekezi lakini sioni cha maana.

Humu walimu ni mabosi wetu wanalipwa perdiem kubwa, honoraria Tsh 500,000 kwa siku; ni semina ya siku tano. Pia wapo na wahudumu wa kubeba mafaili ambao nao wanalipwa pia. Wao hata sielewi wanachofanya, wanazurura tu kwenye korido hakuna kazi wanayofanya tisa kumi wawezeshaji wakiingia ni stori nyingi hamna jipya wanalotueleza sijui waliiandalia nini hii semina!!!
 
Ahsante kwa kujua hilo na kupata ujasiri wa kuyasema mkuu!

Nchi hii hadi tuache hizi tabia za ujanja ujanja, wizi wizi, mkato mkato kuwa tajiri ni rahisi huku ukidiriki hata kuua watu wengi kwa kukwepa kulipa kodi au kuwanyima watu wengine fursa za kupata hata dawa za kutibu maradhi kama malaria, utapia mlo nk.

Idara nyingi za serikali, wafanya kazi wake choka mbaya bila huo wizi wizi nadhani wangekuwa walishaasha kazi na kutafuta njia mbadala. Na hata hiyo mishahara ingekuwa inaridhisha. Kwa sasa kuwabadili hao watumishi wa umma ni ngumu, njia rahisi ni kuendelea kupiga kelele na kujipanga kuwamwaga CCM hapo 2015.
 
Sio huko tu, huku Arusha kuna tasisi moja ya uma wanapeana per diem za kufa mtu, eti wameandaa semina ya kufundishwa jinsi ya ku log in and kulog out kwenye mtandao wa internet.

Cheki hiyo

? ? ? hii ya mwaka jombaa
 
Wamezoea kusubiri hadi bajeti nyingine ya mwaka wa fedha ili waendelee kula fedha za umma, hivyo nakubaliana na mawazo yako mhe., na katika hali ya kawaida wananchi wa hali ya chini hawawezi kujua namna viongozi wa serikali jinsi wanavyoiba fedha hizo hasa wakati wa bajeti mpya inapoenda kusomwa......
Wakuu nawajulisha kuwa kuna ufisadi unaoendelea katika wizara, idara na taasisi zote za serikali katika kipindi hiki cha kuelekea bajeti tajwa kwa kisingizio cha kumalizia mafungu ya 2010/2011!

Yaani kuna semina mbuzi zimeanzishwa, kuna safari watu wanapeana ili kupata posho (per diem). Mi hapa nimeunganishwa kwenye semina haina kichwa wala miguu kuna posho zinagawiwa hadi nasikia uchungu.

Kama hali ndiyo hii basi watz wataendelea kuwa katika hali ngumu ya maisha. Kwanini haya mafungu yaliyobaki yasiunganishwe yote yakapelekwa kwenye shughuli za maendeleo kama kweli tuna nia ya dhati ya kuwasaidia watz badala ya kuendekeza ukware wetu!!!
 
Ahsante kwa dodoso mkuu,

Kama vip tuwekee kaushaidi hata ka barua ka mwaliko ili utilikomalie vizuri vizuri.
 
sasa kazi yetu kuibana serikali inaonekana na finyu sana kwasababu ya ufahamu wetu mdogo hasa wa masuala ya fedha, labda wachache wenye kuelewa zaidi watusaidie katka kutetea na kukemea hali hii.
 
Back
Top Bottom