Leo asubuhi ITV nimemsikiliza afisa anayefuatilia madeni ya wanafunzi ambao hawajalipa, anasema sasa wanapekua makaratasi toka ya siku za mwanzoni na kuorodhesha wadhamini ili baadae wawatangazie, ndipo nilipogundua kuwa record system ni sifuri na ndio maana wanaibiwa kijinga, binaadamu gani mpaka leo bado wanaweka kumbukumbu kwenye matakataka a.k.a..makaratasi? Faili likiibiwa inakuwaje? Kweli Inabidi ICT toka Rwanda waje kutusaidia, fikiria inachukua muda gani kutafuta faili masjala ukilinganisha na kutafuta kwenye database?