Ufisadi | Vita Imefikia Patamu, Gonga Nikugonge

Sekenke

Senior Member
Mar 3, 2008
132
29
Kumekucha
Tulidhani vita ya ufisadi imefikia ukingoni. Kuna hata baadhi ya viongozi walifikia kututahadharisha kwamba tuachane na hili, kwani limekwisha.

Sasa ndo kama kumekucha vile. Vita au vuguvugu la ufisadi limefikia hatua tamu. Kama ni mtego basi unafanikiwa. Chambo kinafanya kazi.

We'nyewe wanaanza kujitokeza, waziwazi, mmoja mmoja, in the open range, in the firing zone. No more spinning, its mano-o-mano!

Wote tunajua Rostam hayuko peeke yake. Je wadhani Mengi yuko peke yake? Nani wako nyuma ya hawa watu? Wadhani mwisho wake ni nini? Je kweli tutashinda vita hii?

Purukushani
Ilipotoka orodha ya mafisadi, Dr Slaa aliwapa changamoto aliowataja wakutane mahakamani. Hakuna aliyethubutu hadi leo, akiwamo RA.

Mengi kaja, tumemsikia. Na mabaya yake mengi tushayasikia, na tumeyasikia tena leo kupitia RA. Lakini, swali la msingi, Rostam alikuwa wapi siku zote na hivyo vielelezo/makabrasha yenye ushahidi juu ya ufisadi wa Mengi?

Je, kweli polisi na upelelezi wetu ni wachovu kiasi hicho hawakuweza kuwa na ushahidi alionao RA, siku zote hizi? Huyu RA, ni polisi yeye, je ni kachero yeye? Kavipata wapi hivyo?

Hivi waziri Ghasia atajitokeza na kumtuhumu wizi wa nyaraka za serikali. Maana baadhhi ya yaliyotajwa yanaihusu serikali.

Na je, Sophia Simba, atajitokeza kumshambulia RA, kama alivyofanya kwa Mengi? Na Mkuchika je?

Nyoka Pangoni.. and getting closer
Kitu ambacho kwa mtazamo wangu kimefanikiwa ni kuwatoa nyoka pangoni. Moto unawaka nje ya pango, hawana budi kujichomoa.

Are we getting closer to the finish line? Au huku ni kuchafua tu hali ya hewa? Ili kutuondoa kwenye mada?

Sasa Mengi naye hakusubiri. Kajibu na kumtaka RA aende mahakamani, hata kama ni kesho asubuhi.

What's still left in their bag of tricks? What's Next?
 
Divided kingdom will never stand.Ufisadi umeingiliwa na nionavyo mambo kamwe hayatabaki vile tulivyozoea. Inabidi kuwe na mabadiliko na kukataa mabadiliko hayo, yatatubadilisha ikibidi kwa vimbuga vya kisulisuli na moto
 
Nakwambia Mungu kasikia kilio chetu, Kama mnakumbuka ombi la Mchungaji yule wa Mbeya baada ya Sofia kuleta usngaingi wa kitchen party, kwa mambo serious! nukuu 'hao mafisadi Mungu awachonganishe ndimi na wasielewane'! there we are! hawataelewana, na hakika ukombozi wetu u karibu!

Walio jifanya mabubu sasa wameanza kusema, mara wanakuja na kauli za serikali imeisha tusemea kupitia Sofia na Mkuchika, mara DPP kashindwa kutushitaki... patamu hapo!
 
Hawa mafisadi wanafikiri sisi wote hatuna akili, huyu RA badala ya kujibu tuhuma naye anatoa tuhuma zisizo na kichwa wala miguu. Yeye anakataa kuitwa Papa lakini anamwambia mwenzake kuwa ni nyangumi!
 
Huyu RA ndo serikali kwani nani asiyejua hili, akiguswa kila mbwa wake atabweka, na ndo maana anatoa reference ya viongozi wote wa serikali waliotangulia kumsemea.

Lakini Mungu mkubwa ndo mambo yanaiva sasa kwani watanzani siyo mabwege tena.
 
Mapapa na manyangumi yanapigana sasa. Patamu kweli. Lakini wa kulaumiwa ni hawa mapapa na manyangumi au wanaowaachia/wanaowapa fursa wafanye upapa na unyangumi wao? Au ndio "Miafrika ndivyo tulivyo"? Ikovipi jamani?
 
Back
Top Bottom