tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,767
- 29,214
Nikiwa mwanachama hai wa CCM, sipendezwi kabisa jinsi mwenyekiti wa chama chetu anavyoongoza nchi hii. Huwa tunashindwa kutoa ushauri wetu kwenye vikao vya chama kwa kuwa mwenyekiti wetu huwa mkali sana pale anaposhauriwa jambo lolote ambalo haafikiani nalo.
Tangu aingie madarakani, maisha ya wananchi wa kawaida yamekuwa magumu maradufu ukilinganisha na uongozi wa Rais aliyetangulia. Rais wa sasa amekuja na staili yake ya kuzuia ufisadi pasipo kuelewa jinsi ufisadi unavyowanufaisha wananchi masikini. Alipaswa kwanza kufanya utafiti kabla ya kubana mianya ya ufisadi iliyokuwa imeshamiri wakati wa uongozi wa Dr Kikwete. Asidhani Kikwete alikuwa mjinga kuachia ufisadi ushamiri….Dr JK alijua umuhimu wa ufisadi katika kuboresha maisha ya wananchi wa kawaida. Falsafa yake ya “Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania” hakuitunga kwa bahati mbaya.
Nitatoa mifano michache (mingine mtaongezea) kuonyesha ni namna gani vitendo vya kifisadi vinavyowanufaisha wananchi wa kipato cha chini. Bidhaa zinazopitishwa bandarini bila kulipiwa ushuru, huuzwa kwa bei ya chini, hivyo kumnufaisha masikini moja kwa moja. Ni jambo lililo wazi kwamba mfanyabiashara anapolipa ushuru wa bidhaa, gharama hizo huzihamishia kwa mlaji wa mwisho kwa kukomaza bei ya bidhaa. Mfano halisi ni kodi kwenye vifaa vya ujenzi. Vifaa vya ujenzi vikipatikana kwa bei rahisi, wananchi masikini wataweza kumudu gharama za ujenzi hivyo kila mwanchi ataweza kujenga nyumba bora ya kuishi.
Utafiti wangu unaonyesha kwamba tangu uongozi mpya uingie madrakani, ukuaji wa mji wa Dar es Salaam umeshuka kwa 30%. Kupungua huku kwa upanukaji wa jiji kumesababishwa na kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi baada ya serikali kuongeza kodi kwenye vifaa hivyo na kuwabana wafanyabishara kulipa kodi bandarini.
Viwanda vingi hutegemea malighafi kutoka nje, kwa mfano, viwanda vya soda na bia huagiza malighafi (kama vile sukari bora na kimea) kutoka nje ya nchi. Baada ya serikali kuzuia uagizaji wa sukari na kubana mianya ya ukwepaji kodi, viwanda vingi vimesitisha uzalishaji na kulazimika kuwapunguza wafanyakazi wake. Serikali inataka watu wafanye kazi (Hapa Kazi Tu) lakini haishtushwi na idadi kubwa ya watu wanaoachishwa au kupunguzwa kazi kufuatia kushuka kwa uzalishaji.
Aidha, baa nyingi zimefungwa na nyingine kugeuzwa nyumba za ibada. Mfano halisi wa baa zilizofungwa na kugeuzwa nyumba za ibada ni hii baa ya Tshentemba iliyopo hapa mtaani kwangu (mtaa wa Mgobanya) hapa Kinondoni. Baa hii ilikuwa na wafanyakazi (baamedi) wasiopungua 50. Baada ya kufutwa kazi, wasichana hawa wasiokuwa na hatia, ambao wengi wana umri mdogo, wamegeukia biashara ya ukahaba hapa Kinondoni makaburini. Nimetafiti na kugundua kwamba bei ya makahaba imeshuka sio tu kwa sababu upatikanaji wa fedha umekuwa mdogo, bali ni kwa sababu ya kuongezeka kwa idadi ya makahaba (baada ya baa walizokuwa wakizitumikia kufungwa), hivyo kupelekea kuwepo ushindani mkubwa wa kibiashara. Kama hali ikiendelea kuwa hivi, jitihada za serikali kupambana dhidi ya maambukizi ya UKIMWI hazitafua dafu.
N.B
Haya ni maoni yangu binafsi kama raia halali wa nchi hii. Sitegemei kunyooshewa vidole kwamba nimetumwa na mafisadi kwa kuwa nimetoa mifano hai jinsi ufisadi unavyowanufaisha wananchi wa kipato cha chini na jinsi ubanaji wa mianya ya ufisadi unavyosababisha maisha magumu kwa wananchi. Karibu kwenye mjadala…tujadiliane kwa ufasaha pasipo kunyoosheana vidole. Kama una mawazo kinzani na haya mawazo yangu, yatetee…usimshambulie mto mada, shambulia hoja. Mods naomba mnilinde.