Ufisadi uliokithiri Chuo cha Ufundi Arusha

TUNDE

Senior Member
Apr 23, 2016
129
77
Kwa zaidi ya miaka mitano sasa CHUO CHA UFUNDI ARUSHA kimeandikwa mara kwa mara na vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.

Sababu ya chuo hiki kuandikwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni ufisadi ulioshamiri katika chuo hiki. Makamo wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema kwamba watu wasiokuwa na sifa wakipewa kazi ni matatizo kwa Taifa. Kumekuwa na malalamiko kwamba Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha hauna sifa stahili kwa kuwa usahili wa nafasi ya Mkuu wa chuo uligubikwa na figisufigisu nyingi.

Taarifa za ndani kabisa za iliyokuwa Bodi ya Chuo zilieleza kwamba waliokuwa wameshinda katika usahili kwa ajili ya nafasi ya Mkuu wa Chuo hawakuweza kupatikana kutokana na sababu mbalimbali. Katika mazingira yasiyoeleweka, Bodi iliamua kumpa kazi kuwa Mkuu wa chuo aliyeshika nafasi ya pili kutoka mwisho, Ndugu Richard J. Masika Mushi.

Inaaminika kwamba pengine uwezo mdogo wa kiuongozi na tabia ya ubinafsi wa kupenda kujilimbikizia mali ndiyo sababu kubwa na chanzo cha Ufisadi wa Chuo cha Ufundi Arusha. Imefahamika kuwa nguvu kubwa ya ushawishi na fedha zilitumika ili kupata nafasi hiyo ya kuwa Mkuu wa chuo.

Katika mazingira yanayofanana na yaliyotumika kupata Mkuu wa chuo, Bodi ya Chuo nayo iliundwa katika mazingira ya kujuana na kulindana. Baada ya kazi hiyo kufanyika na kufanikiwa, ikabaki kazi moja tu, Kufanya ufisadi wa mali ya umma kupitia chuo.

Fedha za umma zenye utata na harufu ya ufisadi ni kama ifuatavyo:
1) Matumizi ya fedha za mafunzo viwandani (IPT) kiasi cha TZS 320,000,000/= zina utata.
Utata wa fedha za mafunzo viwandani ni kuanzia 2011/12 – 2014/2015. Kwa miaka minne mfululizo kiasi cha zaidi ya TZS 80,000,000/= kila mwaka hazijulikani zilikwenda wapi au zilifanya nini. Kwa mfano: Katika mwaka wa masomo 2011/12 Serikali kupitia Wizara ya Elimu ilipeleka Chuoni kiasi cha Tsh 546,743,000/= kwa ajili ya Mafunzo viwandani kwa wanafunzi na waalimu kwenda kuwakagua viwandani. Kadhalika, katika mwaka wa masomo 2012/13 Serikali kupitia Wizara ya Elimu ilipeleka Chuoni kiasi cha Tsh 559,860,000/= kwa ajili ya Mafunzo viwandani kwa wanafunzi na waalimu kwenda kuwakagua viwandani

2) Matumizi ya fedha za mishahara ya wafanyakazi mwezi Januari 2014 kwa wafanyakazi walioajiriwa Desemba 2013. Wastani wa TZS 30,000,000/= fedha za mishahara hazijulikani zilikwenda wapi au zilifanya nini na ni mamlaka gani iliidhinisha kutumika kwa fedha hiyo tofauti na ilivyotakiwa, kulipa wafanyakazi hao mishahara yao.

3) Miradi hewa ya ujenzi ililipwa wastani wa TZS 400,000,000/= ambapo miradi hiyo haipo lakini fedha hiyo ililipwa kwa ajili ya miradi hiyo.

4) Malipo hewa ya miradi ya ujenzi kupitia ATC-PCB, ilifikia wastani wa TZS 250,000,000/=. Matumizi ya malipo hayo hayajulikani na fedha hiyo pia haijulikani ilikwenda wapi.

5) Upanuzi wa jengo la Utawala uligharimu wastani wa TZS 700,000,000/=. Gharama halisi za ujenzi huo hailingani na kiasi hicho kinachodaiwa kutumika.

6) Matumizi ya ujenzi wa jengo la Umwagiliaji lililogharimu TZS 4,000,000,000/=. Wastani wa TZS 2,500,000,000/= zinakadiriwa kutosha kujenga jengo hili na hasa ikizingatiwa kwamba matofali na shughuli nyingine kama paa na madirisha zilifanywa kwa rasilimali za Chuo. Wastani wa TZS 1,500,000,000/= zinadaiwa kutumika kifisadi. Kadhalika zaidi ya matofali 20,000 yalichukuliwa na Uongozi kwa matumizi binafsi.

7) Fedha za msaada kwa ajili ya shamba la Oljoro ni wastani wa TZS 400,000,000/=. Fedha hii haijulikani ilifanyia nini na au iko wapi.

8) Fedha zinazokatwa kutoka mishahara ya wafanyakazi kwa ajili ya ukarabati wa nyumba ni wastani wa TZS 300,000,000/=. Fedha hii haijulikani imefanyia nini au iko wapi.

9) Kutokana na miongozo ya NACTE, Mkuu wa chuo alitakiwa kulipwa mshahara kwa ngazi ya PHTS 12 katika mwaka 2011 mpaka 2014. Lakini kwa kutumia madaraka yake, Mkuu wa chuo alilipwa mshahara kama ifuatavyo: Mwaka 2011/12 alitakiwa kulipwa Tsh 3,330,700/=, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,303,400/= kwa mwezi. Mwaka 2012/13 alitakiwa kulipwa Tsh 3,697,000/=, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,734,000/= kwa mwezi. Mwaka 2013/14 alitakiwa kulipwa Tsh 3,837,000/=, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,823,000/= kwa mwezi.

10) Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo ilimaliza muda wake ambapo kisheria Bodi ingekuwa haipo na hivyo kuundwa upya. Lakini Mkuu wa Chuo alimteua rafiki na class mate wake kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ili tu Bodi hiyo iweze kuendelea na Mkuu wa chuo aweze kuendelea na ufisadi wake kupitia Bodi hiyo. Mkuu wa Chuo alifanya hivyo bila kujali kwamba kwa kufanya hivyo ni kufanya kazi ya Mamlaka ya Rais na ni kuvunja sheria.

Inasemekana chuo kimekuwa na sheria mpya tangu Julai 2015. Sheria hiyo imetoa mwelekeo tofauti wa Bodi ya Chuo. Lakini kutokana na kwamba uwepo wa Bodi mpya utaharibu kabisa malengo ya Mkuu wa chuo na wajumbe wake, kuendelea kufanya ufisadi, ilimlazimu kuandika Barua kwa Katibu Mkuu akiomba mwongozo ili ikiwezekana wajumbe wa Bodi iliyokuwepo waweze kuendelea kuwa wajumbe wa Bodi kufuatana na sheria mpya ya chuo.

Wajumbe wanao ombewa ili ikiwezekana waendelee na ujumbe wa Bodi kutokana na barua iliyoandikwa na mwanasheria wa chuo kwa niaba ya Mkuu wa Chuo ambaye ni mchaga kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ni hawa wafuatao: Christian Nyahumwa (School mate); Suzan Mnafe (Mchaga & girlfriend); Lyne Ukio (Mchaga); Hyacintha Makileo (Mchaga); Karoli Njau (Mchaga); Benedict Lema (Mchaga & School mate); Namnyaki Mattasia (Girlfried) na Thomas Katebalirwe (Mwakilishi wa Wizara).

Pamoja na maombi hayo ya Mkuu wa chuo kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara, Mkuu wa chuo aliendelea kutumia madaraka yake kama alivyozoea na kuitisha vikao vya Bodi ya chuo chini ya Uenyekiti wa Christian Wambura Nyahumwa (school mate) huku akifahamu vizuri, kwamba Mwenye mamlaka ya kuteua Mwenyekiti wa Bodi ya chuo ni Rais wa nchi peke yake.
 
Mkuu mbona umeandika general sana, jaribu kutoa ushahidi kidogo wa ulichokiaandika ili habari yako ipewe uzito! Mfano wa jengo lililotumia 4Bilion wakati 2Billion zingetosha, ungeweka nyama kidogo

Mwisho habari yako itaonekana ni ya majungu tu, ilhali ina kaukweli flani
 
Profesa Ndalichako amefanya mengi, Amewajibisha TCU, Bodi ya Mikopo na NACTE. Tafadhali mheshimiwa waziri, maliza kadhia ya Chuo cha Ufundi Arusha. Taarifa za chuo hicho ni aibu kwa taifa
 
Serikali haitapoteza, pengine itapata mengi na pengine kuokoa fedha ya umma. Nashauri kwamba, kuna haja ya kuunda Kamati/Tume ya wenye uadilifu kuchunguza tuhuma hizi nyingi za Chuo cha Ufundi Arusha.

Kila siku tunasikia matatizo: mara ngono, mara Bodi, mara taaluma inashuka, mara ufisadi, mara upendeleo wa ajira na kila aina ya tuhuma. Dawa ya mambo ya aina hiyo ni uchunguzi huru tu. Ikithibitika hatua za kisheria zichukue mkondo wake. Kama haijathibitika watu waambiwe wakae kimya. Hizi kelele zinachosha
 
Mtu kama hana sifa ya nafasi aliyopewa yupo tayari kutumia njia zozote zile ambazo siyo halali ili aendelee kushika nafasi hiyo .Katika taasisi hiyo ubadhirifu na rushwa ndiyo mahali pake .Msingi wa mambo yote hayo ni kulindana kutoka Wizara .Hali hii siyo rahisi kuondoka nchini kwa kuwa walioasisi utamaduni huu bado wapo na wanasauti na wanasikilizwa.Kazi ni kubwa sana.
 
Ufisadi ni sehemu ya mkakati wa kutoka kimaisha ktk vichwa vya Watanzania wengi hasa penye mali ya Umma.
 
Hata Arusha iliyo chini ya chadema ,nako kuna ufisadi??

Chagadema hovyo kabisa
Umenena mkuu. Chadema ni jina na maneno tu, hakuna kitu. Mbunge wa Arusha Mh. Lema ni mtu wa show game tu. Mambo yasiyompa sifa ya kisiasa hashughuliki nayo. Kuna matatizo mengi sana na ufisadi wa mali ya umma katika taasisi tatu (Chuo cha Ufundi Arusha, Chuo cha Uhasibu Arusha na Taasisi ya Teknolojia ya Nelson Mandela) mkoani Arusha na yameripotiwa kila mahali na vyombo vya habari.

Wabunge wa chadema wa maeneo hayo hawakuwahi hata kufuatilia kujua chanzo cha matatizo hayo na wala hawajajaribu hata kuuliza bungeni ili kujua kama serikali inajua na pengine ina mpango gani wa kushughulikia matatizo hayo sugu ya ufisadi katika taasisi hizo

Lakini wabunge hao wa Chadema wa maeneo hayo wanapigana bungeni ili Bunge lioneshwe live tu, hawajui mambo yanayoumiza wananchi au ufisadi unaofanywa maeneo yao ya kazi. Kwa kweli aliyewahi kuwa mbunge mahiri Arusha ni Kinana wa CCM pekee, wengine ni wasindikizaji tu.
 
Wengi waliojaliwa uwezo wa kuiba mali ya umma na kupatikana kirahisi mara nyingi hawakufanya vizuri kitaaluma. Kama anataaluma ya ualimu atakuwa hajui kufundisha, kama ni mhandisi atakuwa hawezi kutengeneza kinachotakiwa , kama ni mwanasheria hivyohivyo, kama ni mhasibu hivyohivyo nk.

Mtu ambaye hata taaluma yake haiwezi, akiwekwa kuwa kiongozi ndio baraa zaidi maana atakuwa ni mtu wa kujaribu tu maana hawezi kwa sababu hajui na hata akijitahidi kujifunza haelewi na hataelewa. Matokeo yake kila siku itakuwa ni vurugu na anaowaongoza maana hawataelewa anafanya nini, watakuwa wanamwona kama kituko tu. Ndio maana kitaaluma, kiongozi anatakiwa kuwa mfano wa ubora wa uwezo kwa maana ya ujuzi, maarifa na ubunifu. Awe mwepesi wa kujifunza na kuelewa mambo mapya nk.

Tanzania itaweza kupiga hatua na kufika Taifa la uchumi wa kati iwapo taaluma itatiliwa mkazo na zile taratibu (principles) za kitaaluma zikawa zinafuatwa. Watu wasipewe kazi kwa kuangalia sura, wala watu wasipewe kazi kwa sababu wametoa rushwa. watu wapewe kazi kwa kuangalia historia ya uwezo wake kuanzia mbali, akiwa shuleni na kazini.

Kuna watu wamepewa dhamana ya kuwa viongozi lakini badala ya kuwa nuru na msaada kwa kutatua matatizo wamegeuka kuwa matatizo katika taasisi zao. Hapo kazi haitafanyika, eneo hilo litakuwa ni migogoro kila siku. Kuna faida gani kuwa na kiongozi wa aina hiyo mahali pa kazi?

Kiongozi anayependa vitu vya kona-kona na michoromichoro kwa faida yake binafsi anafaida gani kwa Taifa masikini lililofanywa masikini na wachache linalotaka sasa kukua na kufika uchumi wa kati?
 
Report ya CAG mbona iko clean. Watanzania tuna wivu
Report ya CAG iko clean? Iweke hapa watu waione imekaaje! Usijekuta imechongwa, maana hata vyeti vya kitaaluma siku hizi vinachongwa tu bila shida, sembuse hati safi?.
 
Kwa zaidi ya miaka mitano sasa CHUO CHA UFUNDI ARUSHA kimeandikwa mara kwa mara na vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.

Sababu ya chuo hiki kuandikwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni ufisadi ulioshamiri katika chuo hiki. Makamo wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema kwamba watu wasiokuwa na sifa wakipewa kazi ni matatizo kwa Taifa. Kumekuwa na malalamiko kwamba Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha hauna sifa stahili kwa kuwa usahili wa nafasi ya Mkuu wa chuo uligubikwa na figisufigisu nyingi.

Taarifa za ndani kabisa za iliyokuwa Bodi ya Chuo zilieleza kwamba waliokuwa wameshinda katika usahili kwa ajili ya nafasi ya Mkuu wa Chuo hawakuweza kupatikana kutokana na sababu mbalimbali. Katika mazingira yasiyoeleweka, Bodi iliamua kumpa kazi kuwa Mkuu wa chuo aliyeshika nafasi ya pili kutoka mwisho, Ndugu Richard J. Masika Mushi.

Inaaminika kwamba pengine uwezo mdogo wa kiuongozi na tabia ya ubinafsi wa kupenda kujilimbikizia mali ndiyo sababu kubwa na chanzo cha Ufisadi wa Chuo cha Ufundi Arusha. Imefahamika kuwa nguvu kubwa ya ushawishi na fedha zilitumika ili kupata nafasi hiyo ya kuwa Mkuu wa chuo.

Katika mazingira yanayofanana na yaliyotumika kupata Mkuu wa chuo, Bodi ya Chuo nayo iliundwa katika mazingira ya kujuana na kulindana. Baada ya kazi hiyo kufanyika na kufanikiwa, ikabaki kazi moja tu, Kufanya ufisadi wa mali ya umma kupitia chuo.

Fedha za umma zenye utata na harufu ya ufisadi ni kama ifuatavyo:
1) Matumizi ya fedha za mafunzo viwandani (IPT) kiasi cha TZS 320,000,000/= zina utata.
Utata wa fedha za mafunzo viwandani ni kuanzia 2011/12 – 2014/2015. Kwa miaka minne mfululizo kiasi cha zaidi ya TZS 80,000,000/= kila mwaka hazijulikani zilikwenda wapi au zilifanya nini. Kwa mfano: Katika mwaka wa masomo 2011/12 Serikali kupitia Wizara ya Elimu ilipeleka Chuoni kiasi cha Tsh 546,743,000/= kwa ajili ya Mafunzo viwandani kwa wanafunzi na waalimu kwenda kuwakagua viwandani. Kadhalika, katika mwaka wa masomo 2012/13 Serikali kupitia Wizara ya Elimu ilipeleka Chuoni kiasi cha Tsh 559,860,000/= kwa ajili ya Mafunzo viwandani kwa wanafunzi na waalimu kwenda kuwakagua viwandani

2) Matumizi ya fedha za mishahara ya wafanyakazi mwezi Januari 2014 kwa wafanyakazi walioajiriwa Desemba 2013. Wastani wa TZS 30,000,000/= fedha za mishahara hazijulikani zilikwenda wapi au zilifanya nini na ni mamlaka gani iliidhinisha kutumika kwa fedha hiyo tofauti na ilivyotakiwa, kulipa wafanyakazi hao mishahara yao.

3) Miradi hewa ya ujenzi ililipwa wastani wa TZS 400,000,000/= ambapo miradi hiyo haipo lakini fedha hiyo ililipwa kwa ajili ya miradi hiyo.

4) Malipo hewa ya miradi ya ujenzi kupitia ATC-PCB, ilifikia wastani wa TZS 250,000,000/=. Matumizi ya malipo hayo hayajulikani na fedha hiyo pia haijulikani ilikwenda wapi.

5) Upanuzi wa jengo la Utawala uligharimu wastani wa TZS 700,000,000/=. Gharama halisi za ujenzi huo hailingani na kiasi hicho kinachodaiwa kutumika.

6) Matumizi ya ujenzi wa jengo la Umwagiliaji lililogharimu TZS 4,000,000,000/=. Wastani wa TZS 2,500,000,000/= zinakadiriwa kutosha kujenga jengo hili na hasa ikizingatiwa kwamba matofali na shughuli nyingine kama paa na madirisha zilifanywa kwa rasilimali za Chuo. Wastani wa TZS 1,500,000,000/= zinadaiwa kutumika kifisadi. Kadhalika zaidi ya matofali 20,000 yalichukuliwa na Uongozi kwa matumizi binafsi.

7) Fedha za msaada kwa ajili ya shamba la Oljoro ni wastani wa TZS 400,000,000/=. Fedha hii haijulikani ilifanyia nini na au iko wapi.

8) Fedha zinazokatwa kutoka mishahara ya wafanyakazi kwa ajili ya ukarabati wa nyumba ni wastani wa TZS 300,000,000/=. Fedha hii haijulikani imefanyia nini au iko wapi.

9) Kutokana na miongozo ya NACTE, Mkuu wa chuo alitakiwa kulipwa mshahara kwa ngazi ya PHTS 12 katika mwaka 2011 mpaka 2014. Lakini kwa kutumia madaraka yake, Mkuu wa chuo alilipwa mshahara kama ifuatavyo: Mwaka 2011/12 alitakiwa kulipwa Tsh 3,330,700/=, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,303,400/= kwa mwezi. Mwaka 2012/13 alitakiwa kulipwa Tsh 3,697,000/=, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,734,000/= kwa mwezi. Mwaka 2013/14 alitakiwa kulipwa Tsh 3,837,000/=, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,823,000/= kwa mwezi.

10) Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo ilimaliza muda wake ambapo kisheria Bodi ingekuwa haipo na hivyo kuundwa upya. Lakini Mkuu wa Chuo alimteua rafiki na class mate wake kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ili tu Bodi hiyo iweze kuendelea na Mkuu wa chuo aweze kuendelea na ufisadi wake kupitia Bodi hiyo. Mkuu wa Chuo alifanya hivyo bila kujali kwamba kwa kufanya hivyo ni kufanya kazi ya Mamlaka ya Rais na ni kuvunja sheria.

Inasemekana chuo kimekuwa na sheria mpya tangu Julai 2015. Sheria hiyo imetoa mwelekeo tofauti wa Bodi ya Chuo. Lakini kutokana na kwamba uwepo wa Bodi mpya utaharibu kabisa malengo ya Mkuu wa chuo na wajumbe wake, kuendelea kufanya ufisadi, ilimlazimu kuandika Barua kwa Katibu Mkuu akiomba mwongozo ili ikiwezekana wajumbe wa Bodi iliyokuwepo waweze kuendelea kuwa wajumbe wa Bodi kufuatana na sheria mpya ya chuo.

Wajumbe wanao ombewa ili ikiwezekana waendelee na ujumbe wa Bodi kutokana na barua iliyoandikwa na mwanasheria wa chuo kwa niaba ya Mkuu wa Chuo ambaye ni mchaga kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ni hawa wafuatao: Christian Nyahumwa (School mate); Suzan Mnafe (Mchaga & girlfriend); Lyne Ukio (Mchaga); Hyacintha Makileo (Mchaga); Karoli Njau (Mchaga); Benedict Lema (Mchaga & School mate); Namnyaki Mattasia (Girlfried) na Thomas Katebalirwe (Mwakilishi wa Wizara).

Pamoja na maombi hayo kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara, Mkuu wa chuo aliendelea kutumia madaraka yake kama alivyozoea na kuitisha vikao vya Bodi ya chuo chini ya Uenyekiti wa Christian Wambura Nyahumwa (school mate) huku akifahamu vizuri, kwamba Mwenye mamlaka ya kuteua Mwenyekiti wa Bodi ya chuo ni Rais wa nchi peke yake.
7640_10153996847952487_1296214619587581403_n.jpg

sheria_-_the_cyber_crimes_act_-_final-15.jpg
 
Back
Top Bottom