Ufisadi, ufisadi, tumepigwa changa la macho! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi, ufisadi, tumepigwa changa la macho!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msanii, Dec 13, 2009.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Wakati taifa zima likiwa katika mwangwi wa vita dhidi ya ufisadi, huku uadilifu wa viongozi wengi ukiporomoka chali, sisi wananchi tumekuwa kama kasuku kuimba nyimbo za hao mafisadi pasina kuchukua hatua.

  Baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 uliomweka Muungwana ktk himaya kwa minajili ya kutumikiwa (si kutumikia wananchi), kwa kauli yake mwenyewe alisema kuwa alishangazwa sana pesa nyingi ilivyotumika katika uchaguzi hivyo kwa kauli yake akaitisha uchunguzi wa zilipotoka hizo fedha. Punde si punde kukaibuka fununu za kukwapuliwa fedha za akaunti ya madeni ya nje (EPA) na kashfa sindikizi nyenginezo (mf; meremeta/tangold, Deepgreen, Richimonduli/Dowansinyo na watakatifu wengine wa uharibifu). Pamoja na yoote hayo na ukweli kuanikwa barazani, mara mdau mkuu akashikwa na kwikwi iliyomkinza kuchukua hatua kwa waliohusika. Sana sana alitangaza msamaha kabla hakimu hajasoma hukumu yake. Wale waliokataa kukubaliana na masharti ya msamaha ndo tunaowaona leo wakisubiri hakimu awasomee hukumu.

  Baada ya tangulizi fukuzi hapo juu, sasa tizama namna huo mchanga ulivyoingizwa kwenye macho yetu. Ni kwamba baada ya shinikizo la ndani na nje kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoendelea kuibuliwa kila kukicha dhidi ya viongozi adili tena wasaidizi wa sahili wa muungwana, sasa wamejibu mapigo kisayansi tena yahitaji darubini taradadi kuweza kung’amua hili. Ushudavi (ushujaa) wao katika propaganda ndio unaotupeleka harijojo sasa. Kwani baada ya kuona wananchi wamekaza shingo zao wakipiga kelele za “mwiziiiii, mwiziiii wa mali ya umma huyoooo” wao wakaja na kampeni ‘chaos’ yaani mkakati wa changanya utawale. Wameleta picha ya kwamba hawaelewani na kuanza kutoleana kashfa na maneno makali wenyewe kwa wenyewe ili tugeuze macho yetu yasielekee kwenye kuwakomalia na kuwafanyia maamuzi magumu 2010. Na hili la changanya-changanya wameliweza kweli. Kwani sidhani kama vyombo vya usalama vingeweza kukaa kimya ambapo Muungwana anashambuliwa na kuanikwa waziwazi pasina kuchukua hatua. Heshima ya ofisi ya Muungwana ni taasisi na si mtu hivyo kuna ambao wanaangalia kila mtikisiko wa nyasi usilete madhara katika hatua za Muungwana kusongambele. Sikubali kabisa kwamba mzee msemahovyo mgoshi wandima, mshika vitabu wa kilinge chao anaweza kuwaita WEHU wazee weledi wa kilinge chao. Pia siamini kama mzee wangu wa kule bwawani (bwawa la umeme idodomya hukooo ndani ndani) anaweza kumfananisha au kumhukumu msaidizi kuntu wa Muungwana kuwa ni mgonjwa wa akili halafu akaachwa tu. Napingana na ufahamu wangu kwamba jamaa wanatoana macho tena kipindi hiki cha kuelekea ile nyakati turufu ya NUNUA UTAWALE. Lazima kuna ishu inafutwa au inafuatwa katika kuwaweka sawa wabongohoi. Nadhani mtasikia wameitisha semina na makongamano ya upatanisho halafu sisi tutapiga makofi na kuwahurumia ktk sanduku la kura.

  NB (Nachokonoa Bifu)
  Haiwezekani kwamba DEEPGREEN wachote fedha kwa kusingizia ni kwa ajili ya taasisi ya UwT. Mimi kama mlipa kodi ya mkishahara yao, kwa nini siambiwi ukweli wa zilipoenda pesa za deepgreen? Au zile fedha zinahusiana na ile ripoti ya UN kuhusu TZ kusaidia waasi kule Congo DRC?


  Una maoni gani....?
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Sanaa ya siasa za Bongo hakuna mfanowe na hii ndiyo wanayoiita demokrasia ya kweli (kwa mujibu wa wapiga porojo wa bongo)
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kwa akili za wananchi waliowengi TZ ni dhahili chama cha mafisadi (CCM) kitashinda tu.
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Unajua kinachowashindisha ccm ni kura za uoga, kwani ktk mhula wao wa uongozi wanaeneza fear miongoni mwa jamii ili ionekane kuwa hakuna tanzania nje ya ccm.

  Wabongo amkeni jengeni chama imara kisha enendeni ktk sanduku la kura kwa maamuzi sahili
   
Loading...