Mtazamowangu usilinganishe yale majengo ya mlimanicity na mabweni ya chuo yaliyojengwa na Mwizrael.
Yale majengo ya mlimani city yanajengwa kitapeli kabisa !! Ni temporaly buildings zile. Nenda kaangalie material anayotumia lile jengo analojenga pembeni pale sasa hivi.
1. Anatumia mabati sehemu kubwa ukutani. Hii ina maana ameshafanya study kwamba for 20 yrs itakuwa maximum lazima yataanza kuoza mabati yale na kufikia hiyo 50 yrs yenu hamtabaki na kitu.
2. Pili kwa kuona pale wana eneo kubwa basi wameamua kujenga mijengo ya godown ambayo ni cheap bila kujali land value!! Pamoja na kujenga lile la kwanza godown nilitegemea uongozi wa chuo uliojaa wasomi, Maprofessor wa majengo , Civil building, Land valuers, n.k wanaojua jinzi ardhi ya dar ilivyoadimu basi wasingemruhusu aendeleze ujenzi kama huo tena sehemu ya pili. Lakini wamemwacha anachojenga ule upande wa pili ni uchafu zaidi ya ule wa kwanza.
3. Yale maeneo ya Chuo kikuu yalitengwa na wataalamu enzi hizo wakisaidiwa na Mwingereza kwa manufaa ya chuo, na yalikuwa na lengo la kwamba yatasaidia ukuaji wa chuo na upanuaji wa chuo. Nilitegemea kama ni investment wangewekeza kujenga Student villages ambazo zingesaidia wanafunzi wanalala Manzese warudi maeneo ya pamoja. Na hizo student villages zingesaidia sana kwa vyuo vyote vilivyopo Dar.
Hivi ni kweli hawa waliofanya maamuzi hawapiti maeneo ya vyuo vikuu vya nje wakaona vinavyokuwa na maeneo makubwa na yanatumika kwa manufaa ya vyuo siyo kuingia miradi ya kijinga kama hiyo isiyo na manufaa kwa taifa.