Ufisadi na usenene. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi na usenene.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JosM, Mar 9, 2009.

 1. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MSAADA TUTANI

  NDUGU WANA JAMII ASANTENI KUNIRUHUSU KELENDELEZA LIBENEKE LA KUPINGA UFISADI NA USENENE.

  KWA LEO MIMI NAWAANDIKIA WANENE, MH. RAIS, MZEE WA PAMBA, MZEE WA BAGAMOYO, DR. JAKAYA KIKWETE PAMOJA NA RAIS MTARAJIWA 2015, JOHN MASHAKA, WAZIRI MKUU DR. HILDEBRAND SHAYO, MAKAMU WA RAIS JANUARY MAKAMBA, NA BILA KUMSAHAU WAZIRI WA MAMBO YA NJE MTARAJIWA RIDHWANI KIKWETE, WOTE WA 2015.

  MZEE WETU JK, BADO TUNAMPA KURA 2010 KWA SABABU AMEWAONJESHA RUPANGO WANA EPA NA WAKINA LIUMBE WA MAGARI NYEKUNDU, ISIPOKUWA MZEE WA VIJISENTI NA WAKINA NANIHIII, AMBAO BADO ANAWASHUGULIKIWA NA FELESHI WA MASHITAKA

  NDUGU WAHESHIMIWA, MIMI NDIYE MPIGA DEBE WENU NAMBA RI-WANI, NA HALI NI NGUMU SANA, MSINIACHE. AU WATU WA ZEIN KAMA MNAWEZA KUNISAIDIA NA INTERNET KWA SABABU MUHAJIRI WANGU WA ZAMANI ALINIACHIA KA LAPTOPU LENYE JINA LA IBM ALIPORUDI KWAO, WALL-STREET, COLORADO HUKO MEREKANI. KWA HIYO SITAKI MAKUBWA ISIPOKUWA INTANETI ILI NIWEZE KUENDELEA NA SHUGULI ZA MCHANGO WANGU KWA TAIFA ZA KUPINGA USENENE NA UFISADI

  WANENE, MIMI NIMEKUMBWA NA MATATIZO YA KIUCHUMI AMBAYO YANAWEZA KUNIFANYA NIPOTEE KATIKA ULINGO AU BLOGU YA JAMII. ILA KWA VILE NYIE MPO KWENYE SEHEMU NYETI, NAWAOMBENI MNIKUMBUKE KWANI SERIKALI YETU YA 2015 TUTAKUWA PAMOJA MIMI NIKIWAKILISHA KULE YOMBO VITUKA.

  KUJA KWENYE INTERNET CAFÉ KUCHANGIA DHIDI YA UHOVU KATIKA JAMII YETU, INIGHARIMU TSH. 5,000 KWA WIKI WAKATI KIPATO CHANGU KWA SIKU ZA NYUMA ILIKUWA NI Tsh.100, 000/= NILISHUKURU MUNGU KWA HICHO KIDOGO KWANI WENGINE HAWAPATI HATA ELFU KUMI KWA MWEZI. LAKINI KWA SASA NAONA MATATIZO YA KIUCHUMI YALIYOIKUMBA DUNIA YAMENIKUMBA NA MIMI, KWA HIYO SINA KAZI.

  NAOMBA MNIKUMBUKE, AU MDAU YEYOTE ZAIDI YA NILIYOWATAJA ANAYEWEZA KUSAIDIA ANISAIDIE, NITASHUKURU MKIWASILIANA NA MKUU WA WILAYA MWENZANGU WA TEGETA, NA BALOZI WA TANZANIA, UGHAIBUNI MH. ISSA MICHUZI, AMBAYE ANAWEZA KUNITUMIA UJUMBE ILI TUENDELEZE LIBENEKE LA KUPINGA UFISADI NA USENENE.

  VIJANA MACHACHARI WAMEKUWA GUMZO NA VIVUTIO SANA HATA KWA MAMA LISHE WANAOSOMA GLOBU WA JAMII WANAJUA KWAMBA NYINYI NDIO WATARAJIWA 2015 NA WATAWAPIGIENI KURA KWA VISHINDO. YAANI MTAPATA KURA BILA KUPINGWA MKINIPA UONGOZI WA KUENDESHA KAMPENI KWA WALAHOI WENZANGU.

  ZIDUMU FIKRA ZA MZEE WA PAMBA JK
  ZIDUMU

  KIDUMU FIRKA ZA RAIS MTARAJIWA 2015
  ZIDUMU

  ZIDUMU FIKRA ZA MAKAMU WA RAIS 2015
  ZIDUMU

  MASENENE YOTE KAMA US-BLOGGER YALAANIWE
  YALAANIWE

  MAFISADI YOTE KAMA VIJISENTI NAYO YACHAPWE MBOKO
  YACHAPWE
  MALIMBWENDE YOTE YANAYOVUNJA MAGARI YA WATU YAOMBEWE DUA MOLA AWASAIDIE YAOMBEWE

  MKEREKETWA, YOMBO VITUKA!!!!-------------------------------------------------

  Dakika 30 za Internet Café Zimekwisha
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Waharibu mada...
   
 3. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenielewa vizuri? nadhani ujaelewa dhumuni langu,
  naomba ufafanuzi unapo sema nimeharibu mada?
   
 4. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  We josm!!
  Acha kujipendekeza!!! Hao wote unaojipendekeza kwao ni sehemu ya ufwisadi(nikiitwa ikulu poa tu, ila ukweli ndo huo!)
   
Loading...