Ufisadi na Undumilakwili wa Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi na Undumilakwili wa Watanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sokomoko, Aug 31, 2008.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu mjadala unauhusu Ufisadi ndani ya nchi yetu ya "Maziwa na Asali" yenye kila aina ya uzuri na kila aina ya utajiri yenye madini yote yenye thamani kuanzia Dhahabu mpaka Nikkei iliyogundulika juzi juzi maeneo ya Kigoma.

  Lakini juu ya utajiri wote huu tumekuwa mayatima,mambumbumbu,tumekuwa wasaliti wa vizazi vijavyo!tumekuwa ndumilakwili! Kwani sote tumeshuhudia hotuba mbili za EPA na RICHMOND jinsi watuhumiwa walivyo "samehewa" kiaina na bila ya sisi kuchukua hatua yoyote!

  Ni ukweli hatuwezi kuandamana ni kweli sisi ni majuha tunashindwa hata na watoto wetu wameweza kuandamana kwaajili ya kuwakilisha kilio chetu cha hali ngumu ya maisha baada ya nauli kutoka sh 50 mpaka sh 100. Sasa sie waoga na majuha tunatakiwa tufanye nini?

  Sote tunawajua wahujumu uchumi wale wa EPA na RICHMOND tunajua makampuni yao na bidhaa zao kwanini tusizigomee bidhaa zao kuonyesha kama kweli tunapingana nao kuliko kuendelea kuwaneemasha kwa kuzinunua? Nani asiejua katika hiyo list yumo Rostam? nani asie jua Rostam anamiliki hisa 30% za Vodacom? mpo tayari kufanya hili? hamjui kuwa Habari Cooperation ni ya Rostam? Kwanini msigomee kununua magaazeti yanayochaipishwa na kampuni hiyo? Wenzetu wa Kenya walijaribu kugomea baadhi ya bidhaa za makampuni yaliyompongeza Kibaki alipopora kura. Sisi sidhani kama tutaweza kugoma kwa hili kupinga UFISADI kazi kwenu.

  sokomoko
   
Loading...