Ufisadi: Mtu tajiri Brazil afungwa miaka 19

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
150729060902_marcelo_odebrecht__640x360_reuters_nocredit.jpg


Ufisadi: Mtu tajiri Brazil afungwa miaka 19

Mtu tajiri zaidi nchini Brazil amehukumiwa kifungo cha miaka 19 jela kwa kushiriki ufisadi.

Mfanyibiashara huyo mashuhuri katika sekta ya ujezi, Marcelo Odebrecht, alipatikana na hatia ya kuhusika katika ufisadi unaohusu viwango vikubwa vya fedha .

Mahakama ya huko inasema kuwa Bw. Odebrecht amepatikana na hatia ya ulanguzi wa pesa , utoaji hongo na pia kuwa na ushirikiano na watu wahalifu.

Aidha Mahakama hiyo imesema Odebrecht alilipa hongo ya hadi dolla millioni 30 kwa kampuni kubwa ya mafuta nchini humo Petrobras,ili apendelewe na kupewa kandarasi.

Amekuwa kizuizini tangu mwezi Desemba.
150619135120_odebrecht_sp640.jpg

Makao makuu ya kampuni yake Odebrecht

Kampuni yake ya Odebrecht ndio kubwa zaidi katika kanda ya Amerika ya Kusini ambako inahudumu katika mataifa 21.

Vilevile Odebrecht imewaajiri wafanyikazi katika kanda zima katika sekta ya ujenzi.

Bwenyenye huyo alijiuzulu kutoka kwa kampuni hiyo ilioanzishwa na familia yake na ambako amekuwa akifanyaka. BBC
 
Huku kwetu tunatumbua wafanyakazi Wa uma tu. Wafanyasiasa na wafanyabiashara hao no, nchi itatetereka eti
 
Huku kwetu matajiri hawaguswi wanaombwa kulipa kodi,kurejesha pesa EPA
 
Hapa kwetu, Danganyika....kamwe majipu halisi hayawezi kutumbuliwa kwa kuwa mtumbuaji anafahm fika ya kwamba hayo majipu yanamfaham kiundani...

Unataka yamtumbue kabla hajayatumbua....thubutuuu

Ataishia kwenye vijipu tu, hayo majipu makubwa kabisa, yaliyompisha hapo hayawezi kuguswa....usaha wake unaweza kummwagikia mwili mzima....una harufu Kali sana...
 
Kwetu sisi itatuchukua miaka hamsini tena kuanza kutoa hukumu kama hizi kwa wakwepa kodi na walarushwa wakubwa
 
MBONA BAKHRESA AMETUMBULIWA KWA KUTAKIWA KULIPA BILION MBILI NA TRA KUTOKANA NA KASHFA YA MAKONTENA. TARATIBU MAMBO YATABADILIKA KWA MATAJIRI HAWA. IRANI TAJIRI MKUBWA KABISA AMEHUKUMIWA KUNYONGWE KWA KOSA LA KUGUSHI NA KUWEZA KUJIPATIA PESA NYINGI KUTOKA SERIKALINI.
 
Back
Top Bottom