Ufisadi mpya kutikisa Bunge

Ufisadi mpya kutikisa Bunge

jme

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
4,768
Reaction score
5,102
KWA UFUPI

  • PAC kusoma ripoti ya kashfa tatu kubwa kesho Dodoma
  • Jengo la watu mashuhuri Uwanja wa Ndege ni balaa
  • Misamaha ya kodi, nyumba ya mbunge kutawala vikao

Dar es Salaam. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kesho itawasha moto upya bungeni wakati itakaposoma ripoti maalumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ikitarajiwa kuibua kashfa tatu nzito ikiwamo ya misamaha ya kodi.

Kashfa nyingine zinazotarajiwa kuibuliwa kesho ni, ufisadi katika gharama za ujenzi wa jengo la watu mashuhuri (VIP) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na uuzaji wa nyumba ya Bodi ya Korosho.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe zilisema kuwa, tayari kamati hiyo imepokea ripoti ya ukaguzi huo ambayo inaonyesha ufisadi wa kutisha katika maeneo hayo matatu na mengineyo.

Masuala hayo matatu pia yaliibuka wakati wa vikao vya kamati za Bunge vilivyomalizika Dar es Salaam wiki iliyopita, huku bodi ya korosho ikibanwa kuhusu nyumba yake aliyouziwa Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Silvestry Koka.

Kwa mujibu wa habari hizo, ripoti hiyo inayoonyesha jinsi ufisadi wa kutisha ulivyofanywa katika ujenzi wa jengo la (VIP Lounge) na Serikali inadai ilitumia Sh12 bilioni kulijenga, lakini mthamini wa majengo ya Serikali ameeleza kuwa jengo hilo lina thamani ya Sh3 bilioni.

Katika suala la misamaha ya kodi, PAC imepokea taarifa kutoka kwa CAG ikionyesha kuwa misamaha hiyo iliyokuwa imefikia Sh1.5 trilioni mpaka Juni 2013, lakini baada ya mwaka moja misamaha hiyo imeongezeka hadi Sh1.8 trilioni mpaka Juni 2014.

"Kwa mwaka moja tu, misamaha ya kodi imeongezeka kwa zaidi ya Sh300 bilioni. Kiasi hiki ni kama escrow fulani (Fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow, Sh306 bilioni)," chanzo cha habari kilidokeza.

Katika vikao vya kamati hiyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilieleza kuwa misamaha ya kodi imepanda kutoka Sh1.4 trilioni mwaka 2012/13 hadi Sh1.8 trilioni mwaka 2013/14, chanzo kikiwa ni misamaha ya kodi katika miradi mikubwa. Ilisema kati ya misamaha hiyo, Sh676 bilioni zinatokana na misamaha ya kodi inayotokana na Ongezeko la Thamani (VAT) na kuwa hali hiyo itapungua iwapo nchi itaanza kutumia Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Pia, TRA ilifafanua kuwa mpaka sasa wafanyabiashara na kampuni kubwa zimefungua kesi katika mahakama ya rufaa wakipinga kulipa kodi ambayo inafikia Sh1.7 trilioni.

Mvutano mwingine unaotarajiwa kuibuliwa katika ripoti hiyo ni uwasilishwaji wa utata wa uuzwaji wa nyumba ya Bodi ya Korosho.

Awali, hati ya nyumba hiyo ilikuwa ya Taasisi ya Kilimo Tanzania ambayo ilifutwa mwaka 1963, kabla ya mtu mwingine kuibadilisha hati na kuiuza kwa Koka mwaka 2011.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mudhihir Mudhihir alisema Koka aliuziwa nyumba na taasisi hiyo ambayo haikuwa mmiliki halali.

Alisema nyumba hiyo iliuzwa kwa Sh300 milioni na katika juhudi za bodi kufuatilia taratibu za kuirudisha, ikagundulika kuwa hati imeshabadilishwa, kusisitiza kuwa uuzwaji wa nyumba hiyo ulifanyika kimakosa bila kufuata sheria na taratibu.

Juzi Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alikaririwa akiwataka wananchi kutoa taarifa kuhusu makusudio ya kuuza nyumba za Serikali na mashirika ya umma, kutokana na madeni mbalimbali ili ziweze kukombolewa kabla ya kuuzwa.


Chanzo: mwananchi

 
Misamsha ya kodi wanajipa viongozi wenyewe kwa Kampuni zao wenyewe, hizo Nyumba wanauziana viongozi wenyewe mpaka kiongozi akibadilishwa eneo la kazi anaenda kuishi hotelini.
Leo hii mnadai serikali haina hela, hizo mnazoiba ndizo za serikali.
 
  • Thanks
Reactions: jme
Misukule ya Lumumba itavamia hapa na kuchafua hali ya hewa sasa hivi, wa kwanza kujilipua atakuwa laki si pesa kama sio faizafox kwa pamoja na........
 
Last edited by a moderator:
Maskini Tanzania na waishio Ndani yake,thamani ya billion 3 wahuni wanasema 12........CCM inakufa kifo kibaya sana si ajabu ikikoroma na mdomo ukiwa wazi.
Nakumbuka hii ishu kuna siku Mbowe aliigusia kidogo bungeni akapozwa kuwa suala litafanyiwa kazi,tnx PAC mumekuja upya.
 
Misukule ya Lumumba itavamia hapa na kuchafua hali ya hewa sasa hivi, wa kwanza kujilipua atakuwa laki si pesa kama sio faizafox kwa pamoja na........

Na hawa watu wanamoyo sana sijapata kuona,katikati ya uozo wa harufu kali wenyewe ndio wanapojitumbukiza.
 
Last edited by a moderator:
Jengo wanasema bilioni 12 gharama halisi bilion 3 hizi 9 zimekwenda wapi jaman?barabara ngapi za mtaani zingejengwa hapa?Kwa nn nyie masisiem mnatuibia hivi jaman?Nina hasira jamani hata ya kujilipua kwa kweli.
 
Hii Tanzn jaman mwenye nayo nn yaani tunaishi kwa matukio kila siku ni kutibu ugongwa kwann isiwe kinga jamaan ni ss ni mambumbulula kwann tunawapa kura .Tuamkeni
 
Njoni hapa, wezi ukoo wa panya, mtetee wizi wenu. Siku zenu 40 za wezi, zimefika, ni siku ya kufa kwa nyani, miti yote sasa inateleza!!!
 
Ah jaman hii nchi yaan nataman nihame kabisaa" wanipe changu kiasi chochote kile nifanye bauli nikaishi na wanadam huko nch za wenzetu" looh this country it is rotern bw loooh
 
Jengo wanasema bilioni 12 gharama halisi bilion 3 hizi 9 zimekwenda wapi jaman?barabara ngapi za mtaani zingejengwa hapa?Kwa nn nyie masisiem mnatuibia hivi jaman?Nina hasira jamani hata ya kujilipua kwa kweli.

Hii ndiyo sababu ya Dr mwakyembe kuondolewa mapema asingebaki salama
 
Tulishasema kuwa CCM ilishakufa zamani...na kinachoonekana sasa kujitetea au kutetewa ni 'mzimu' au 'mzuka' tu wa kinachosadikika kilikuwa CCM, na hata JK alishasema kuwa kwa 'hali ya ndani' anayoijua, ikifikia 2015, CCM itatoweka baada ya kushindwa vibaya...! anayebisha ni nani?? Mie ntakuwa wa kwanza kukamata haya majamaa majizi kama kumbi kumbi..na najua ntakapoanzia, maana akili zao, IQ zao na fikra zao kwa sasa ni kama 'kuku wa broilers' ..hata kuzinduka kiakili wanahitaji booster! ...na baada ya kushindwa vibaya Oktoba, watakuwa wanagongana vichwa wenyewe kwa wenyewe, wakikimbiana na wakati huo huo wanalikimbia 'jeshi la umma' a.k.a...UKAWA....! ni kuwadaka tu kama kumbi kumbi...! hapatakalika wakati wa kulisafisha taifa na kujenga uhai mpya! CCM mjiandae tu..
 
Zitto apishe ofisi kwanza ndo tujadili hili, natoa wito mzuieni huyu mtu kuingia bungeni hadi aachie ngazi, koka kanunua nyumba tena yenye hati halali, PAC imekuwa ofisi ya DCI kila siku kufatilia madili tu hawana mipango yoyote ya kututoa hapa tulipo na kupiga hatua ya maendeleo.

Ushauri wa hawa PAC umetugarimu sana, ndo hawa walishauri kuvunja mkataba wa Richmond miezi mitatu kabla ya mkataba kuisha ukatugarimu kweli, sasa wameshauri kutaifisha mitambo ya watu ushauri hata mganga wa kienyeji hawezi kutoa.
 
Zitto apishe ofisi kwanza ndo tujadili hili, natoa wito mzuieni huyu mtu kuingia bungeni hadi aachie ngazi, koka kanunua nyumba tena yenye hati halali, PAC imekuwa ofisi ya DCI kila siku kufatilia madili tu hawana mipango yoyote ya kututoa hapa tulipo na kupiga hatua ya maendeleo.

Ushauri wa hawa PAC umetugarimu sana, ndo hawa walishauri kuvunja mkataba wa Richmond miezi mitatu kabla ya mkataba kuisha ukatugarimu kweli, sasa wameshauri kutaifisha mitambo ya watu ushauri hata mganga wa kienyeji hawezi kutoa.

Mapepo wachafu wanatumia akili na midomo yako kuongea haya MAKUFURU.
 
Hivi VAT huwa mwisho si ni sisi walaji ndo tunailipa???
Sasa huwa inakuwaje serikali kusamehe VAT inaonekana ni hasara!!
VAT ikisamehewa sisi walaji si ndo tunakuwa tumepunguziwa bei katika bidhaa!!???

Mwenye utaalamu zaidi katika VAT anifahamishe hapa zaidi tafadhali.
 
Back
Top Bottom