Ufisadi Mkubwa wa Halmashauri Manispaa ya Temeke

Ufisadi Mkubwa wa Halmashauri Manispaa ya Temeke

Aristides Pastory

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2012
Posts
348
Reaction score
60
Wajumbe na wanabodi salaamu kwenu.

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoa wa Dar Es Salaam kuanzia Tarehe 13/3/2013 mpaka 18/3/2013 itaendesha zoezi la UPULIZIAJI dawa kuzuia WADUDU na MAGONJWA mlipuko kata Mbali mbali wilayani humu.

Zoezi hilo litasimamiwa na kampuni teule iitwayo KIHO COMPANY.

Gharama zilizopendekezwa ni kama ifuatavyo:
1. Kila Nyumba itatozwa= tshs 2000/=
2. Vibanda vya Mama lishe= tshs 4000/=
3. Gesti na Baa= tshs 8000/=

Habari nilizonazo ni kuwa kila baada ya miezi miwili lazima operesheni hiyo itekelezwe.

Je, kwa hali hii tutafika?
Nawasilisha.
 
Hiyo kazi imeidhinishwa na baraza la madiwani? na wananchi walishirikishwa?
Unaweza kutuwekea mchanganuo wa hizo fedha, kwanini wengine walipe 2,000 wengine 4,000 na wengine 8,000???
 
Hiyo kazi imeidhinishwa na baraza la madiwani? na wananchi walishirikishwa?
Unaweza kutuwekea mchanganuo wa hizo fedha, kwanini wengine walipe 2,000 wengine 4,000 na wengine 8,000???
Ndio maana mleta thread akatumia kichwa cha habari "Ufisadi mkubwa wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke" Kumaanisha alicho posti ni maagizo ya Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, nawala siyo yake, hivyo ndivyo nilivyo elewa mimi
 
Michango inasaidia maendeleo, kam kuna jambo la maana kwa jamii husika why not?
 
hio mbona inafanyika ktk jiji zima na nikawaida toka zamani? ufisadi wake ni nini?
Wajumbe na
wanabodi salaamu kwenu.

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoa wa Dar Es Salaam kuanzia Tarehe
13/3/2013 mpaka 18/3/2013 itaendesha zoezi la UPULIZIAJI dawa kuzuia
WADUDU na MAGONJWA mlipuko kata Mbali mbali wilayani humu.

Zoezi hilo litasimamiwa na kampuni teule iitwayo KIHO COMPANY.

Gharama zilizopendekezwa ni kama ifuatavyo:
1. Kila Nyumba itatozwa= tshs 2000/=
2. Vibanda vya Mama lishe= tshs 4000/=
3. Gesti na Baa= tshs 8000/=

Habari nilizonazo ni kuwa kila baada ya miezi miwili lazima operesheni
hiyo itekelezwe.

Je, kwa hali hii tutafika?
Nawasilisha.
 
kwa hiyo wakiua wadudu kwako kila baada ya miezi miwili na kutozwa 2000/= ni ufisadi?!!!elezea vizuri bana
 
Hiyo kazi imeidhinishwa na baraza la madiwani? na wananchi walishirikishwa?
Unaweza kutuwekea mchanganuo wa hizo fedha, kwanini wengine walipe 2,000 wengine 4,000 na wengine 8,000???

mkuu Mwita Maranya tuhuma juu ya chadema kupitia kwa lwakatare mna majibu gani?ile clip imekata appetite yangu ya lunch leo
 
Hivi "fumigation" si inakuwa na "guarantee" ya muda fulani! Je, kama mnabambikiwa madawa feki ndiyo mlipe kila baada ya miezi miwili kweli?
 
Back
Top Bottom