Ufisadi mkubwa ndani ya shirika la reli

Dragoon

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2013
Messages
7,058
Points
2,000

Dragoon

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2013
7,058 2,000
Habari za kuaminika kutoka Kampuni ya Reli Tanzania (reli ya kati) zinasema kuwa kuna ufisadi mkubwa sana umefanyika ndani ya kampuni hiyo kwenye uagizaji wa mabehewa ya treni mapya. Habari za kuaminika zinasema kuwa mabehewa yaliyoagizwa ni mabovu, na hayaendani na miundo mbinu ya reli ya kati.

Jumatatu iliyopita baadhi ya mabehewa yalifanyiwa majaribio na yalianguka kwa sababu za kiufundi.
Inasemekana kwamba mabehewa yaliyoagizwa hayakupitiwa na jopo la ufundi la kampuni hiyo ili kubaini dosari zilizopo. Uongozo wa kampuni haukutaka kamati ya ufundi ichunguze mabehewa hayo.

Kutokana na hayo kuna bosi mmoja wa kampuni hiyo (jina linahifadhiwa) wiki hii yote amekuwa akifika kazini kama mgonjwa kutokana na hofu aliyonayo. Inasemekana kapuni iliyopewa tenda kutengeneza mabehewa hayo haijishughulishi na utengenezaji wa mabehewa, bali ni kampuni ya madalali tu. Mabehewa yalitengenezwa bila kufanyiwa majaribio, majaribio yakafanyika Tz.

Kuna mengine ya abiria ambayo hayajafanyiwa majaribio. Hivi karibuni Dr. Mwakembe anatarajiwa kuwasili nchini akitokea ziarani nje ya nchi. Tutegemee tamko toka kwake na kubaini mafisadi walio husika katika hili.
 

Dragoon

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2013
Messages
7,058
Points
2,000

Dragoon

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2013
7,058 2,000
Mwakyembe atakuwa anahusika, ana tabia iliyokomaa sana ya kuingilia operational duties za management.
Hii ndio sababu JK kamtoa kwenye wizara ya uchukuzi, kapelekwa wizara ya ushirikiano wa afrika mashariki, hii ni demotion maana anakokwenda ni Kijiweni wala si wizarani. Bila shaka waziri mpya Sitta atasafisha wizara ya uchukuzi na kutolea ufafanuzi na ufumbuzi wa mabehewa feki
 

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
13,113
Points
2,000

Sangarara

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
13,113 2,000
Hii ndio sababu JK kamtoa kwenye wizara ya uchukuzi, kapelekwa wizara ya ushirikiano wa afrika mashariki, hii ni demotion maana anakokwenda ni Kijiweni wala si wizarani. Bila shaka waziri mpya Sitta atasafisha wizara ya uchukuzi na kutolea ufafanuzi na ufumbuzi wa mabehewa feki
Sitta ndo anaenda kuhaibu zaidi.
 

Forum statistics

Threads 1,380,849
Members 525,893
Posts 33,781,795
Top