Ufisadi-mfumo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi-mfumo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlenge, Feb 15, 2010.

 1. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #1
  Feb 15, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Enzi zile za chekechea na darasa la kwanza (kabla ya 1980) tulisoma kwenye kitabu jamii fulani ikitafuta kiongozi:


  • Awe mrefu kuliko wote
  • Awe mlimbwende kuliko wote
  • Awe na akili kuliko wote
  • Awe na nguvu kuliko wote
  • Awe na mbio kuliko wote
  • Awe shujaa kuliko wote
  • Awe mwerevu kuliko wote
  • Awe mjanja kuliko wote
  • Awe na hekima kuliko wote
  • Awe na busara kuliko wote
  • Awe mwadilifu kuliko wote
  • Awe na upendo kuliko wote
  • Mdemokrasia kuliko wote
  • Mtawala bora kuliko wote
  • Asipende kujilimbikizia mali na madaraka, kuliko wote
  Kwa sasa, mtu anapokuwa mtawala Tanzania, huchukuliwa kuwa na sifa hizo zote hapo juu. Si cheo cha urais tu, bali hata nafasi nyinginezo kwenye taasisi za umma.

  Kwa vile hutegemewa mtu aliyeko madarakani ni mwenye sifa za aina hiyo, kama zile tulizosomaga enzi zetu za chekechea, hakuna utaratibu madhubuti wa kuwadhibiti.

  Jambo la kusikitisha, ni kwamba, kelele nyingi zipigwazo pale jamii inapogundua mtu huyo hana sifa hizo zote, huwa ni kwamba mtu abadilishwe, pengine atakayekuja atakuwa nazo; na wala si mfumo, taratibu na kanuni zilizowezesha mtu huyo kufanya jambo ambalo jamii hailipendi.

  Badala ya kushughulika na 'ufisadi-mfumo', tunahangaika na watu binafsi. This is what is killing Tanzania.

  Palikuwa na wakati kwenye chama cha mpira wa miguu, FAT, iliposemekana kwamba, kwa mfumo uliokuwepo, hata angeenda Mother Theresa baada ya muda naye angekuwa mwizi tu.

  Nchi za wenzetu zinachukulia kwamba mtu yeyote atakayepewa madaraka atakuwa mwizi, mdikteta, mfisadi na mbinafsi. Kwa hiyo huwekwa mfumo wa kuhakikisha mtu yeyote atakayepewa madaraka atatimiza yale jamii inayotaka, hata kama mtu huyo hategemewi kuwa ni 'malaika'.

  Ikitokea mtu akafanya madudu kwenye utawala, jambo la kwanza litakalofanyika ni kuangalia mfumo una tatizo gani uliowezesha mtu huyo kufanya ufisadi., kabla ya kushughulika naye. Ndipo mabadiliko ya mfumo hufanyika, na mtu mwingine atakayekaa kwenye nafasi badala yake, hataweza kufanya ufisadi wa aina ile.

  Ndio maana kwetu tunapoteza nishati nyingi kujadili watu, jinsi walivyo mafisi-mafisadi, wasio na huruma na nchi yetu, wasivyo na uchungu nayo, wasivyotujali wananchi, kana kwamba hayo ni mambo ambayo hatukuyategemea, pasi na kujadili mfumo ukoje mpaka wameweza kufanya hayo, na nini kibadilishwe ili mabaya hayo yasijirudie.

  Mfano mdogo: Wabunge wamekuwa wakilalamika kwamba mikataba ambayo serikali inaingia ni mibovu, na ni hasara kwa taifa. Lakini miaka nenda, miaka rudi wimbo wa malalamishi ni huohuo. Kwa nini wabunge wasitunge sheria kwamba hakuna mkataba wowote (mkubwa) ambao serikali itauingia, pasipo kuidhinishwa na bunge., na kwamba mkataba wowote ambao serikali itauingia bila kuupeleka bungeni, bunge litakuwa na nguvu za kuuagizia muda wowote ukajadiliwe bungeni, na bunge likawa na nguvu za kuufanya usiwe na nguvu za kisheria.

  Mfano mwingine, topiki nyingi kwenye jukwaa hili ni la kujadili ufisadi-mafisi badala ya ufisadi-mfumo.

  Ili tuendelee, yabidi tujadili ufisadi-mfumo, badala ya ufisadi-mafisi.

  -- Mlenge
   
 2. Ndjabu Da Dude

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,858
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Fy faen!! Given such "superhuman" personal traits, no wonder we virtually only have psychopathic individuals in most all positions of immense political influence in society...
   
 3. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #3
  Feb 15, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Because we believe anyone in leadership position has such powers, we shun any effort to check and balance their powers.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Feb 16, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  ''Awe mlimbwende kuliko wote'' una maana gani?
   
 5. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #5
  Feb 17, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  ""pretty" / "handsome" = 'mlimbwende'
   
 6. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,480
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu Chumvi,

  Mbona umeniwahi? Maana nilitaka nianze kuandika kuhusu Uongozi na Viongozi na naona ushawahi. Lakini langu nitakaloandika ni pana zaidi na si kuhusiana na Ufisadi pekee, bali hali halisi ya Tanzania!
   
 7. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #7
  Feb 17, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Tyuti,

  Usiufiche mchango wako!

  Mlenge
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...