Kwamba pesa za eskroo siyo za wa tanzania (ccm 2015). Tanesco yakataa kufanya re-calculation! sababu pesa zishapigwaKuna njia mbili za kuonyesha kupingana na maamuzi ya taasisi unayoiongoza au kushirikiana nayo kiutendaji.
Moja ni kupinga maamuzi yote kwa uwazi bila kuogopa.
Mbili ni kujiuzuru na kuacha uovu wa taasisi au chama kile usihusike nao kamwe.
Sasa mnaopingana na ukweli wa mada Kuhusu UFISADI NDANI YA CCM NAOMBA niambieni ni Nani Mwenye Haki YA kupinga ufisadi na rushwa kwa Ujumla wake sasa kati ya wagombea Urais Tanzania Ni E.N. Lowassa au J. P. Magufuli MAANA mpaka Leo MMOJA anamsifu mmojawapo wa waliotajwa kama mafisadi na anakaa nae Meza moja wakifanya maamuzi pamoja bila kupinga Tena ya Nchi na Lowassa sio tu kajiondoa na kajisafisha kuwa Hahusiki na ufisadi wala taasisi ya CCM pia alijiuzuru mapema akiamini na kusema 'Najiuzuru kulinda Serikali NCHI' maana ccm sio baba yangu wala mama yake.
nikweli tena ushahidi anao dr slaa na shangaa hawa watu wanaosema lowassa ni msafi
Ishu si kumpigia kura liwasa bali ishu ni kwamba lowasa nae ni jizi kama mijizi ya ccm,sasa umpigie au usimpigie kura ujue yeye ni jizi pia,hakuna lugha nyingine ya kupamba hapa tutakua hatuna akili wala maana yoyote.
Ushahidi zaidi ya ule wa ESCROW,MUHONGO NA TIBAIJUKA ulioonesha hali halisi ya jinsi CCM ILIVYO NA WEZI WA FEDHA NA MALI ZA UMMA? halafu bado wezi wanalindana.
kwahiyo kama ccm wanawalinda majambazi nanyinyi mkaona bora mlinde jambazi kuu lowassa.kweli cdm ccm b
Mbona hamumshtaki?
unaniuliza mimi badala ya kumuuliza dr slaa aliyetuaminisha kuwa lowassa ni fisadi?
Sikuulizi wewe,nawauliza WEZI WA MALI WA TANZANIA KWA MIAKA YOTE ZAIDI YA 50,najua wanapita huku,labda wewe haikuhusu hii comment.
unaniuliza mimi badala ya kumuuliza dr slaa aliyetuaminisha kuwa lowassa ni fisadi?
Acheni majungu. Kama lowasa angekuwa fisadi kweli asingejitenga na ccm. Amefanya ufisadi wapi, mbona mna kigugumizi hamtaji. Wapo walootajwa kwenye epa, lowasa hayumo, wapo waliotajwa escrow lowasa hayumo, wapo waliotajwa richmod lowasa hayumo, wapo waotaja kuhusika na mikataba haramu inayoangamiza nchi hii lowasa hayumo, wapo wanajulikana kuchakachua katiba ya warioba iliyotungwa na wananchi lowasa hayumo. Basi ninyi mnomwita lowasa fisadi wenyewe ndio mafisadi wakubwa na wahujumu wa nchi yetu. Nyamazeni kimya.
Ni upotoshaji au uzuzu mkubwa kufikiria kuwa wizi wa kiwango cha import support, EPA, rada, ndege ya serikali, Richmond, n.k. Unaweza kuhusishwa na mtu mmoja mmoja kipekee (individuals). Wizi wa aina hizo huhusisha michakato yenye hatua kibao kupitia taasisi kuu za maamuzi nchini. Sioni ni vipi rais, waziri mkuu, waziri wa sekta husika, mwanasheria mkuu, wanaweza kupona katika kashfa za aina hiyo. Labda tu kama wahusika halisi wamekamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki katika wakati muafaka.
Na kama hao niliowataja hawahusiki basi si rahisi ufisadi aina hiyo ukafanikiwa; lazima utakwama katika hatua fulani za mchakato. Ndio maana katika nchi za waelewa (wasio wapumbavu na malofa), kashfa ya aina hiyo ikitokea, rais au serikali inaachia ngazi. Hawawezi kukubali porojo za watu wenye dhamana kubwa za uongozi wa nchi kunyoosheana vidole mitaani na kuitana mafisadi kwa kuviziana kwenye majukwaa ya kisiasa bila hatua stahiki kuchukuliwa. Ndio maana nakubali kabisa kuwa sisi Watanzania ni wapumbavu na malofa. Watu wanatuibia kimfumo halafu wanakuja kutuchezea komedi ya kuitana mafisadi na sisi tunadandia ngoma tusiyoijua kwa ushabiki mandazi!
Nimemsikia mgombea wa CCM anadai atatoa elimu bure hadi sekondari na dawa hospitalini zitapatikana kwa sababu PESA ZIPO SERIKALINI ILA TATIZO NI MAFISADI WANAZILA; YEYE ATAWAFAGILIA MBALI! Halafu akashangiliwa sana na wananchi! Kwa nini tusimpe kudos Mh. Mkapa kwa kutupa sifa inayotustahili! Nasubiri kampeni ya UKAWA nione kama nayo itaendeleza dhe komedi.