Ufilipino sio dangulo la taka - Rais Duterte

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1079765


Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameifokea nchi ya Canada kwa kushindwa kuchukua hatua juu ya takataka ilizosafirisha hadi katika nchi yake iliyopo kusini mashariki mwa Asia miaka kadhaa uliopita.

Nchi hiyo imewasilisha mara kadhaa malalamiko yake kupinga kidiplomasia hatua ya Canada ya kutuma tani za uchafu nchini Ufilipino kati ya mwaka 2013 na 2014.

Wiki hii Rais Duterte alitishia kurejesha takataka hizo nchini Canada, Canada inasema "ina nia sana "ya kutatua swala hilo na itashirikiana na Wafilipino kufanya hivyo.

Rais Duterte aliikosoa Canada juu ya mzozo huo wa muda mrefu wa kidiplomasia , akisema imeibadilisha nchi yake kuwa "dangulo la kutupa uchafu".

Rais Duterte anafahamika kwa mtindo wake wa kutoa kaulli za wazi na mara nyingi hutumia lugha na kauli kali zenye utata.
 
Back
Top Bottom