Ufikiri wa Police wa Tanzania

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
195
Ukiandika tamko la polisi likawa la kipuuzi, unadhalilisha jeshi. Tunafikiri na wengine hawana akili, lakini kumbe pengine sio. Sasa kwanini wewe uliyepewa jukumu la kukaa mezani kuandika kwa niaba ya Polisi uchafue jeshi zima kwa sababu za fikra ndogo?. Watu wanatilia shaka kuwa uteuzi wa majaji hauzingatii sifa, je na polisi uteuzi hauangalii hayo? Ni hatari sana kuongozwa na watu wenye maono madogo.

Pengine hata tunaposema, mauaji, vitendo vya kikatili, na vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi vinazidi. Vitendo hivi vinazidishwa pamoja na utendaji na matamko ya polisi ya kizembe kama hili ninalotaka watu waelewe uwezo wa polisi ulivyo.

Hivi majuzi tunatambua kuwa msanii mahiri wa filamu na muziki wa kizazi kipya nchini, Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea' alipata ajali, ajali hiyo ilipelelekea kifo chake, na watuw asio waungwana wakamwibia kabisa na kila mtu mwenye maadili mema akasitikishwa na kitendo hicho.

Tarehe 30/12/2012, jeshi la polisi lilitoa taarifa kuwa vitu vilivyoporwa na watu wasiojuliana katika ajali ya msanii mahiri wa filamu na muziki wa kizazi kipya nchini, Marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea' eneo la Songa Kibaoni wilayani Muheza mkoani Tanga, vimesalimishwa na wananchi wanaosadikiwa ni wezi. Hivi kweli wananchi ni wezi?, tunazumgumzia wananchi wenye hasira kali, kumbe ahta siku hizi tunaweza kusema wananchi wezi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, alithibitisha kupatikana vitu hivyo, ambako alisema upatikanaji wake ulitokana na msako mkali uliofanywa na uongozi wa serikali Muheza wakishirikiana na Jeshi la Polisi wilayani humo. Mpaka hapo hakuna shida, tunawapongeza kwa msako. Hii ni kazi nzuri Kamanda alisema, baada ya kutokea kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Tanga, liliweka mtego na kutangaza kuinunua simu ya mkononi ya msanii huyo aina ya ‘blackberry' ndipo moja kati ya wanaodaiwa vibaka waliohusika kwenye tukio hilo, alipojitokeza na kuipeleka kwa ajili ya kuiuza. Hii ni intelijensia nzuri, mliweka mtego, mwizi akaleta simu nako ni sawa. Tunamshukukru kachero aliyeweka mtego simu ikaletwea.

Kamanda alisema, wakati wezi walipofika eneo ambalo walikubaliana, walikabidhi simu hiyo kwa ajili ya kuikagua, lakini baadaye wezi hao walishtukia mtego huo na kukimbia huku wakiiacha simu hiyo. Hapo ndo huwa nakasirishwa na polisi. Walijua anayekuja ni mwizi, alipokimbia kwanini hawakumkamata? Kwanini hawakumfukuza? Hawakuwa na bunduki kumtishia? Kwanini mwizi amekimbia, na amekimbilia wapi? Polisi semeni vizuri kuondoa dhana kuwa mmehongwa kuwaachia watu wasio waungwana.

Kamanda hakuishia hapo ametaja vitu ambavyo vimesalimishwa kwa jeshi hilo kuwa ni simu ya mkononi aina ya blackberry, Betri la gari, tairi la akiba, radio ya gari, begi ambalo lilikuwa na nguo za marehemu, saa ya mkononi na nguo ambazo alikuwa amevuliwa na vibaka wa eneo hilo mara baada ya kutokea ajali hiyo. Mmesema Mwizi wa simu alikimbia, wa tairi la fari, na Yule wa betri, na Yule wa redio ya gari, na Yule wa begi la nguo. Wote hawa walikimbia, au polisi kweli mtaaminika lini kwa utendaji wa aina hii?

Inasononesha sana lakini matamko kama haya yanazidisha hasira za wananchi, na kuongeza vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi.Kwanini Mwizi alipokimbilia kusipojulikana, Polisi hawakwenda naye ili tujue huko kusikojulikana ni wapi? wakati mwizi na polisi walikuwa eneo moja, tena polisi akijua anayekuja ni mwizi. Sielewi Badilikeni.
 
Welu

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
852
500
kazi ya amepigwa na kitu kizito lakini baaba kuua hicho kitu kizito hakionekani. kazi za intelejensia.
 
Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
195
Moderators Asanteni, mpo makini asanteni kwa kurekebisha post yangu na kuirudisha tena.
 
lm317

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
451
195
Polisi wa Tanzania wamewahi kuibiwa MISHAHARA YAO ndani ya KITUO CHAO CHA POLISI!
Ila umakini na uhodari wa polisi utauona wanapoidhibiti CHADEMA
 
Inno laka

JF-Expert Member
Mar 24, 2012
1,619
2,000
Acheni majungu na mambo yasiyokuwa na maana ya aina yoyote kila siku police police.....

Kwan kuna ulazma wa kumkimbiza mwiz kama amekimbia...mwache akimbie kwan chakufia nini.....police akikimbia akavunjika mguu we utamsaidia nini.'.
 
KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
877
250
Inabidi lifunguliwe jukwaa la polisi, majuzi nilifungua uzi katika jukwaa la siasa kuhusu polisi (huu hapa) ukahamishiwa jukwaa la Habari na Hoja mchanganyiko, baada ya hapo nikaikuta jukwaa la sheria. Leo tunaona malalamiko mengine kuhusu polisi, maombi yangu kwa mods ni kwamba siasa inahusu kila nyanja iwe afya, sheria , elimu, na tunapotoa malalamiko yetu humu tunaamini kwamba watunga sera (wanasiasa) ndio wapo kwenye nafasi ya kushughulikia haya mambo
 
BULOLE BUKOMBE

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
488
0
Acheni majungu na mambo yasiyokuwa na maana ya aina yoyote kila siku police police.....

Kwan kuna ulazma wa kumkimbiza mwiz kama amekimbia...mwache akimbie kwan chakufia nini.....police akikimbia akavunjika mguu we utamsaidia nini.'.

Kumbe wakati unaomba kazi ya polisi uliambiwa ni kucheza kiduku?
kama huwezi kufukuza mwizi kwa hofu ya kuvunjika mguu je jambazi utapambana nalo wewe? ninachojua kwa uhakika mmekata tamaa na kazi kutokana na uongozi wenu mbovu unavyowaminya, pole sana ningekuwa mimi ningeacha kazi hiyo na kufanya nyingine, ila wengine mkiingia humo hamtaki kujifunza kazi zingine kazi kusubiri pesa za rushwa tu hapo ndipo mnapoteseka kuliko pole sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Cha msingi ni pesa tu hzo zingne ni kelele tu
 
Fpam

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
290
0
utawasikia" tunayapa majambazi haya masaa 24 yajisalimishe vinginevyo watakiona cha moto'' stupid yaani mmewakamat then wamekimbia eti wajisalimishe sasa uwezo wa police uko wapi hapo?
 
BHULULU

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
4,937
2,000
Acheni majungu na mambo yasiyokuwa na maana ya aina yoyote kila siku police police.....

Kwan kuna ulazma wa kumkimbiza mwiz kama amekimbia...mwache akimbie kwan chakufia nini.....police akikimbia akavunjika mguu we utamsaidia nini.'.
Tumia ubongo kufikiri,hapa watu hawachezi kiduku
 
CRN

Member
Oct 24, 2012
60
0
Acheni majungu na mambo yasiyokuwa na maana ya aina yoyote kila siku police police.....

Kwan kuna ulazma wa kumkimbiza mwiz kama amekimbia...mwache akimbie kwan chakufia nini.....police akikimbia akavunjika mguu we utamsaidia nini.'.

Na CRIMINAL PROCEDURE ACT iko wazi kwenye suala la Arrest,kukimbizana na mtu kisa unataka umkamate ni suala la MAY na siyo SHALL,kwanza kupatikana kwa vitu pekee ni Polisi jamii imetekelezwa,hebu tusilaumu polisi wetu kwa kila kitu alaaaaah!
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,870
1,500
Tatizo sio kwamba POLISI hawawezi kuandika/kutoa taarifa vizuri kama watu wengine waliokwenda shule. Tatizo ni kwamba taarifa wanazotoa ni UONGO unaotungwa OFISINI ndiyo maana zinakosa mantiki.
 
Inno laka

JF-Expert Member
Mar 24, 2012
1,619
2,000
Tatizo sio kwamba POLISI hawawezi kuandika/kutoa taarifa vizuri kama watu wengine waliokwenda shule. Tatizo ni kwamba taarifa wanazotoa ni UONGO unaotungwa OFISINI ndiyo maana zinakosa mantiki.

hakuna taarifa ambayo itatungwa ofisin ndugu hapo Umetudanganya.:-@
 
Jig saw fit

Member
Nov 30, 2011
89
0
acheni ya kishabiki, sumtym tuwe tunachuja mambo co kila desa tumeze mengine matango pori, mbona watu wanne wamekamatwa na walifikishwa police na jana walikuwa mahakamani????
Tatzo lako Isango siku zote mada zako huwa ni polisi tu, ni sahihi bt usiwe ktk upande mmoja tu, sasa tizama ulivowadanganya wa-tz mchana kweupe ktk hili???
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,870
1,500
hakuna taarifa ambayo itatungwa ofisin ndugu hapo Umetudanganya.:-@

Wewe utaamini kila kitu hapa Duniani hata akina Kibwetele kama hutaki kusgughulisha akili yako.

Ina maana hadi leo unaamini ile taarifa ya ACP Kova, kwamba Dr. Ulimboka alitekwa na Kichaa Mkenya aliyekwenda kutubu kwa mchungaji Gwajima

Ina maana wewe hadi leo unaamini taarifa ya Paul Changoja kwamba Marehemu Daud Mwagosi alipigwa na kitu kizito kilichorushwa na washabiki wa CDM.

Hizi zote ni TAARIFA zilizokuwa COOKED kwenye OFISI ZA POLISI. Ndiyo maana hazileti mantiki

Kama wewe unaziamini hizo taarifa basi amini kwamba, mwisho wa dunia ni 1/1/2013 anza kuponda raha!
 
Mimi sikuung mkono kabisa nina sababu ya msingi......hvyo basi m2 anapouwawa maiti ake hufanyiwa uchunguz na Dr....na huyo ndo mtaalam anayetoa ripoti kuhusiana na kifo unaponambia polisi wanadanganya nakubishia kabisa

.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom