Ufedhuli wa Familia ya Rais Gaddafi nchini Libya na Somo Kwa Wa-Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufedhuli wa Familia ya Rais Gaddafi nchini Libya na Somo Kwa Wa-Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uwezo Tunao, Feb 23, 2011.

 1. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0


  WikiLeaks Exposed Gadhafi Family Abuses
  Clan's abuse of power helped fuel unrest

  [​IMG]
  By Rob Quinn, Newser Staff

  Posted Feb 23, 2011 4:51 AM CST | Updated Feb 23, 2011 4:57 AM CST

  (Newser) – Libyans had plenty of reasons to despise Moammar Gadhafi and his clan long before the leader ordered the use of heavy artillery on protesters.

  State Department cables released by WikiLeaks detail some of the Gadhafis' abuses of power, which are known to Libyans despite the regime's control of the media, and are helping fuel unrest, the New York Times reports.

  The cables describe (1) power struggles between the leader's eight children, at least two of whom have been involved in crushing protests.

  The clan and its scandals "provided local observers with enough dirt for a Libyan soap opera," US diplomats observed. (2) All the Gadhafi children appear to have received vast amounts of money from state oil firms, diplomats noted.

  According to one cable, (3) Gadhafi's son Muatassim demanded $1.2 billion from the national oil corporation to establish his own militia, to keep up with his brother Khamis, head of a special forces group that "effectively serves as a regime protection unit."

  (4) Gadhafi himself was described as a hypochondriac who feared flying over water.

  One 2008 cable to Condoleezza Rice described him as (5) "self-styled intellectual and philosopher" who "has been eagerly anticipating for several years the opportunity to share with you his views on global affairs.”

  SOURCE: WikiLeaks Exposed Gadhafi Family Abuses - Clan's abuse of power helped fuel unrest

  UJUMBE HUMU:

  Wikileaks sasa waweka hadharani Ufedhuli wa familia ya Kanali Gaddafi; moyo wa kupenda saaana ufisadi, uroho wa madaraka, kiburi kwa wananchi na ulaini wa raisi wa Libya zaidi ya 'embe dodo iliyoiva' tofauti na wengi tunavyomfikiria siku zote!!

  Mpaka hivi sasa taifa la watu wa Libya, kwa familia ya Kanali Gaddafi, wao waliona tu kama shamba la bibi ambapo vita vya ndani kwa ndani ya familia kati ya watoto wake 8 ni vikali sana kuliko vita vya kikundi chochote kingine ndani au nje ya taifa hilo, kila mmoja akitaka ukubwa wa kuliongoza. Kama haitoshi, ni wiki iliopita tu wamefwatuliana mi-risasi nyumbani na taarifa zaidi bado wamezikalia.

  Kwa mujibu wa wikileaks, kila mtoto wa Gaddafi ni TRA wa biashara zote pale Libya. Wazunguka hovyo wakijivisha joho la urais wa baba yao kuendelea kutoza mabilioni ya dollar hasa kwa makampuni ya nje yanayoshughulika na biashara ya mafuta kama nasi tulivyoanza kule Mnazi Bay na hapo nyuma tu kwa Kigoma Malima Junior.

  Mashirika ya mafuta ya taifa lao, sawa yake TPDC yetu hii hapa ni wa kupigwa mkono kila wakati kama trafiki polisi na daladala pindi wanakaukiwa kifedha - hawachukui hela ya kitoto huko. Mnakumbuka kuna mtoto wa kiongozi wetu fulani naye alipoteza vijisenti milioni 10 asigundue mapema eeehhh???

  Kama haitoshi, yeye Mautassim Gaddafi (mwanae mojawapo) yeye alionelea aheri akakamate kabisa shiko wa
  dollar bilioni 1.2 kusudi akaanzishe jeshi lake binafsi ili aweze kumkabili vilivyo kaka yake mojawapo, Khamis Gaddafi, ambaye ndiye hivi sasa mkuu wa kikosi maalum cha makomandoo ambao ndio wanaohusika na ulinzi na usalama wa serikali ya baba yao.

  Hata ule mkurupuko wa Seif Al-Islam Gaddafi wala haikutokana na uchungu kwamba Libya inavurugika bali ilikua ni katika kumuaminisha baba kwamba wakati wa shida kidume ni hiki hapa na wala si wale wanandugu wengine saba. Kwa ufupi, Gaddafi kifo chake kinaweza kikatokea nyumbani kwake zaidi kuliko hata kutoka kwa mikono ya wapinzani wake wengine.

  Licha ya ujasiri wa Gaddafi alivyokua akidhaniwa na wengi miaka yote huko nyuma kabla ya msingi huo kusalitiwa na ujumbe wa lugha ya mwili wake wakati akito hotuba zote za sekunde 20 na baadaye ile ya dakika 17, Gaddafi ni mwanajeshi muoga kuliko wote ambaye kwa kuendekeza anasa na kuacha mazoezi ya kijeshi, japo kumebaki tuakili ya kijeshi lakini MWILI UNAKATAA sawa na jinsi mshsmbulizi machachari wa Brazil Ronaldo Dalima alivyojikuta kabla ya kuamua kutundika daluga kabisa kucheza soka.

  Huyu baba anaogo ajabu kuona kitu maji na hasa kuruka na ndege juu yake - hivyo kwa Nguvu ya Umma Gaddafi ni laini kuliko embe dodo iliyoiva ukizingatia uwepo wake katikati ya familia iliyogawanyika ambayo mdoli wao wa kuchezea siku zote ni 'paja la kuku'!!!

  Isitoshe, tabia ya kiongozi huyu ambayo ni mtaalam wa kila kitu; hashauriki, msomi mwenyewe, mwanafalsa ya mambo ya mapinduzi yote yeye, mfalme wa wafalme bado yeye yeye, Nguvu ya Umma itamdaka mchona kweupe kama panzi na kummaliza kwa kumvuta tu viungo vya mwili kila upande na kugawanyika kama kuku iandaliwayo kwa mgeni rasmi kijijini.

  Wa-Tanzania tuwe tunayasoma haya tunayoyaandika hapa mtandaoni na TUCHUKUE HATUA ZA DHATI KUZUIA DALILI ZOZOTE ZA VIONGOZI KUTAMANI KURITHISHA UKUBWA WATOTO WAO NDANI YA NCHI YETU. La sivyo, haya yanayosomeka leo hii kama simulizi na hadithi za kawaida tu zisije zikatupata.

  Unafikiri kwa kashfa hiyo nzito ya Gongolamboto kama Husseini hakua mtoto wa Mzee Mwinyi bado angelikua kwenye kiti hicho licha ya kutamani hata na midaraja mikubwa zaidi ya kiungozi ndani ya taifa hili hapo baadaye kana kwamba Wa-Tanzania wengine taaluma ya kuongoza haipandi???????????


  Hii ndio familia ya kifahari ya Kanali Moammar Gaddafi isiyofahamu kitu Libya zaidi ya mipaka ya uzio wa nyumba yao.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Endapo tutaendekeza ugonjwa wa kurithishana watoto UKUBWA katika maeneo mbalimbali ndani ya nchi basi kuna shida kubwa inatusubiri kama taifa huko mbele ya safari.

  Kwanza wazee wengine wao walijizuia vipi wakafanikiwa kulikwepa gonjwa hili ndani ya taifa letu. Iweje wengine wawe wanaliendekeza kana kwamba ni haki kabisa anayopata mtu katika kipande cha shamba la ukoo aliyomegewa???

  Tanzania tuamke sasa hivi tu!!!!
   
Loading...