Ufaulu mwisho iwe Division 3

Ufaulu mwisho iwe Division 3

Kweli mkuu yani ni upumbavu ulioje mtu anapata div four kisa ana vi D vinne anaenda kusoma clinical medicine au engineering...
Unakuta mgonjwa alifaulu vizuri biology kuliko daktari..

Kikawaida mtu akipata D uwezo wake kwenye somo husika ni mdogo kuliko kawaida mwenye D na F hawana utofaut
Ndio elimu ya Bongo hio mkuu unga unga pata connection endelea na maisha mengine nani atajua una D 4 na F 3 ukienda NTA level mpaka 6 unapiga GPA 4.5 ya mchongo nani ataangalia cheti cha form 4
 
Kidato gani unazungumzia? maana form four div 4 huendelei mbele labda vyuo vya kati, lkn form two ukiwa na D mbili umepita au C moja unaenda form three
Nimefatilia kuwa kuna Form 2 zaidi ya 370,000 wamepata Division 4 ila wanasonga mbele
 
Warudie mitihani.

Hilo ni wazo zuri sanaaaaaaaaaaaa

Hakuna kwenda chuo na division 4
Maana lengo lisiwe wanafunzi wengi kufanya mitihani.

Serikali kwa sasa ina lengo la wengi kusoma ila haijaweka lengo la kutoa elimu bora.

Division 4 ni mtu aliyefeli
 
Unambiwa mtoto akipata C moja ya kiswahili mengine yote F ,anasonga kidato Cha tatu "hatuachi mtu nyuma"
Afu tutegemee miujiza huko mbeleni.

Ukiona wanafunzi wengi wanafeli Form 2 maana yake wengi hawakupaswa ingia Form 1, wameingizwa kisiasa. Haiwezekani watu 370,000 wapate Division 4 afu muwaruhusu kuendelea na masomo
 
Vyuo vina ngazi kama certificate, diploma, degree na kuendelea....!!! Au acha tu niishie hapa.
Huko ndio tunazalisha Walimu, Manesi, Madaktari, Wahandisi wabovu kwa kupitia huu mfumo
 
Kama ulipata division four form four basi wewe ni mjinga tu.

Kilichokubeba chuo ni assignment tu na kumuotea lecturer tu.

Wengi kwenye reasoning hamna kitu.
ukipima reasoning kwa kuangalia form four ulipata nini utakuwa una fail pakubwa mnoo, kuna watu mtaani wana reasoning capacity na general knowledge kubwa mno na hawajafika hata university. Reasoning haipimwi kwa kuzingatia uwezo wa kukariri. Mfano mzuri ni wenzenu wa Law school, au umesahau kilichowakuta?
 
Wajinga kama nyie lazima muwe na mawazo sawa nchi hii tuta import hadi nyanya siku za usoni kwa akili kama hizi,

Mnaabudu Div?
Hahahaha mbona umepanic mkuu. No hard feeling haya ni mawazo tu. Inaonekana umetukana sana huko uliko. Namimi nasemaje kama umetukana nawewe hivyohivyo mara 10 yako.
 
Walio fanya vizuri aje? Kukariri? Then baada ya hapo watuundie Ndege? Kukariri types of Rock, Coffee Farming in Brazili na kujua tarehe Vita kuu ya kwanza ya Dunia ilianza hizo sio akili ni mambo ya kukariri, Dunia isha hama huko kutambo sana Wakenya hawakuw wajinga kupiga stop mitihani ya Taifa, Bongo bado mnaabudu Div
Nitajie nchi iliyoendelea duniani isiyo na mitihani. Ambayo mtu yeyote tu anaweza soma akawa astronaut au akawa neurosurgeon. Ambayo ukimtaka aeronautical engineer unafyatua kilaza yeyote unafundisha anaelewa.
 
Elimu ni nini yaani hata mtu aliyepata Sifuri unaweza kusema hajaelimika chochote kuliko mtu ambaye hajaenda kabisa shule ?

Ifike wakati tuache kupima uelewa kwa madaraja
 
Afu tutegemee miujiza huko mbeleni.

Ukiona wanafunzi wengi wanafeli Form 2 maana yake wengi hawakupaswa ingia Form 1, wameingizwa kisiasa. Haiwezekani watu 370,000 wapate Division 4 afu muwaruhusu kuendelea na masomo
Hyo form two mambo ya division ni upuuzi tuu watumie wastani kama miaka ya nyuma, mtoto akishindwa kufikisha wastani wa 50 arudie darasa akifeli mara ya pili aende veta tuu sio lazma wote wasome elimu ya sekondari
 
Nitajie nchi iliyoendelea duniani isiyo na mitihani. Ambayo mtu yeyote tu anaweza soma akawa astronaut au akawa neurosurgeon. Ambayo ukimtaka aeronautical engineer unafyatua kilaza yeyote unafundisha anaelewa.
Tatizo la Tanzania ni siasa hadi kwenye vitu vya msingi.

Matatizo ya Tanzania yamesababishwa na Elimu yetu.

Matatizo hayatakwisha sababu hatutabalisha mfumo na muelekeo wa elimu yetu.

Kwa sasa kila anayeingia lengo lake ni watu wengi kujiunga na shule. Hawajali wanajifunza nini huko shuleni
 
Hebu eleza ni kwa kiasi gani matatizo ya Nchi yetu yamesababishwa na elimu yetu.
Na wakati ukieleza hayo, nitaomba ulete uthibitisho ni matatizo mangapi yameletwa katika nchi yetu na chanzo chake ni hawa vilaza wenye Div. 4 walioachwa wakaendelea na shule.

Naomba ueleze kwa usahihi ili nisije kutoka hapa nikiwa na uthibitisho kwamba wewe ni kilaza.
 
Walio fanya vizuri aje? Kukariri? Then baada ya hapo watuundie Ndege? Kukariri types of Rock, Coffee Farming in Brazili na kujua tarehe Vita kuu ya kwanza ya Dunia ilianza hizo sio akili ni mambo ya kukariri, Dunia isha hama huko kutambo sana Wakenya hawakuw wajinga kupiga stop mitihani ya Taifa, Bongo bado mnaabudu Div
Kenya wameacha mitihani ya kitaifa? Na hii KCSE na hawa best students wa mwaka jana ni ya wapi?
IMG_20230107_093646.jpg

Kukariri kama sio sehemu ya kipimo cha akili ungekuwa hujui hata jina lako ambalo ulipewa, ulisikia wanakuita na ulifundishwa kuliandika. Hata kuvaa ungevaa sketi, maana umekariri umekuta wanaume wanavaa mavazi unayovaa sasa.

Hao waunda ndege huwa wanarudia kilekile kilichogunduliwa kwani. Si wanasoma kilichopo (kukariri na kuelewa) kisha wanafanya improvement. Yani unadhani Boeing kuna kichaa anayeenda pale anajikuta genius kisha aanze kuunda landing gear upya bila kuangalia na kukariri zilizopo na kuboresha, au unadhani pale Mercedes Benz unadhani kuna fala anaenda anaanza upya kuunda injini bila kusoma (kukariri na kuelewa) models na wapi kunahitaji improvement kama kudeal na torque, HP, carbon emission na fuel consumption, wakati kazi ya kuvumbua injini ilifanywa na Karl Benz late 1800s.

Kama huwezi kariri wewe moja kwa moja ni kilaza. Huo ni uwezo wa kawaida kabla hatujaja kwenye innovation, renovation na creation. Wewe unataka kidato cha pili wapewe mabati waunde helicopter bubu bila kujua basic laws of physics? Sasa nchi kama nchi yenye watu milioni 61 itajuaje kama wanafunzi milioni 2 wameelewa, wafuatwe mmoja mmoja nyumbani kwao wapewe mabati waunde ndege? Assessment ambayo ni convenient, possible, low cost, ya muda mfupi, standardized kuondoa lawama na inayopimika ni mitihani.

Hata kwenye kutoa hoja tu akili inapimwa. We unataka NECTA wawe na makenta yabebe vyuma wanafunzi wakaunde makabati sijui
 
Serikali itoe agizo kuwa wenye Divion 4 wasiruhusiwe kuendelea na elimu katika mfumo rasmi, warudie mitihani au wasiendelee na masomo kabisa
Tanzania Police Force watakosa watu wa kuwa ajiri mkuu,refer comment ya Waziri Simbachawene wakati flani katika mchakato wa ku wa ajiri...
 
Serikali itoe agizo kuwa wenye Divion 4 wasiruhusiwe kuendelea na elimu katika mfumo rasmi, warudie mitihani au wasiendelee na masomo kabisa
Mkuu hilo daraja la nne ndiyo ufaulu wa vigogo waliokuwa wengi pamoja na watoto wao. Sidhani kama ushauri wako wataukubali.
 
Kweli mkuu yani ni upumbavu ulioje mtu anapata div four kisa ana vi D vinne anaenda kusoma clinical medicine au engineering...
Unakuta mgonjwa alifaulu vizuri biology kuliko daktari..

Kikawaida mtu akipata D uwezo wake kwenye somo husika ni mdogo kuliko kawaida mwenye D na F hawana utofaut
cliniccal medicine au engineering courses usipo soma utafeli tu
 
Comments za wengi humu mnaonekana mlipata Division ONE humu na watoto wenu watakuwa na ONE Kali sana
JF ndo ivo,nyuma ya keyboard watu wajanja sana kam kwel mtu anajua mambo aingie venue utakapo jua hujui
 
changamoto ya ELIMU bongo ilianza kwenye lugha nyerere aliharibu apo tu, na amini tungekuea kama Nigeria
 
Back
Top Bottom