Ufanyeje mtoto asikudanganye?

Jielewe

Member
Jan 10, 2017
40
62
Fikiria uko jikoni ukiandaa chakula cha jioni. Watoto wako wawili wadogo Fred na Joe wanacheza sebuleni. Salome yuko mezani akifanya kazi za shule.

Mara unasikia mlio wa kitu kuvunjika sebuleni. Unapatwa na wasiwasi. Unakwenda haraka kujua kilichotokea. Maji yanatiririka sakafuni. Chupa ya chai imedondoka na kupasuka. Unakasirika.

Fred, mwanao mdogo, haonekani kuwa na wasiwasi. Haraka anamsemea mkubwa, ‘Sio mimi mama…ni Joe!’ Kwa hasira unamtazama Joe. Uso wake kweli unaonyesha wasiwasi. Kwa ukali unamwuuliza, ‘Wewe ndo’ umevunja chupa?’

Anasita. Amejaa wasiwasi. ‘Nauliza ni wewe?’ unarudia. Kwa haraka anajibu huku akitikita na kichwa, ‘A-a-a! Sio mimi mama!’

‘Nani amevunja chupa?’ Unauliza kwa hasira kali. Mdogo anasisitiza, ‘Ni Joe!’ Unamshika mkono kwa ghadhabu kubwa huku ukilalamika, ‘Kwa nini umevunja chupa?’

Salome anaona aokoe jahazi. ‘Usimchape Joe mama. Aliyevunja chupa ni Fred!’ ‘Fred?’ Unakasirika kudanganywa na mtoto wa miaka miwili. Mbaya zaidi haonekani kujutia anachokifanya.

Kwa nyakati na sababu tofauti watoto wote hudanganya. Kudanganya ni kusema uongo. Ni kutoa habari zisizo za kweli.

Uongo ni dhambi. Uongo huumiza watu. Uongo unaharibu uhusiano wetu na watu. Mtu mwongo haaminiki. Hakuna mzazi anaweza kuvumilia kuona analea mtu ambaye hataaminika kwa jamii.

Tabia ya uongo ikiachwa ikomae ni hatari kwa mstakabali wa mtoto. Kama mzazi unayetamani kukuza mtoto mwadilifu atakayeaminiwa na watu ni lazima kuushughulikia mapema.

Jifunze sababu za mtoto kusema uongo, na mambo ya kufanya mwanao awe mkweli.
 
kwanza unatakiwa kuwa na kipande cha bakora ndani na kila mtoto ajuwe kuwa baba/mama ana kipisi cha bakora kisichokatila.

kisha ongea nao hasa yule anayesema uongo kwamba 'sema ukweli sikuchapi. sema uongo nikuchape'

next time akikosa ukamshikia bakora atakuuliza 'nikisema ukweli hunichapi baba/mama?' mzazi utaitika ndiyo. na kweli usimchape. ila hiyo ni kwa matukio ambayo haukuona akitenda.

ila ikitokea anatenda unaona/unasikia. mfano anatukana ukisikia mubashara. hapo hakuna mjadala ni kuvuta bakora na kucharaza.

taratibu with time utaona nidhamu inatamalaki na hatimae unakuza mtoto mwema.
 
Ni km serikali hairuhusu kuchapa watoto??!1
 
Adhabu ndiyo matofali ya kujengea uongo. Namna mzazi unavyo-react mtoto akikosea inaweza kuchangia kukuza tabia ya mtoto kujihami kwa kukudanganya.
 
Back
Top Bottom