Ufanisi hafifu vivuko vya Kigamboni

Ufanisi hafifu vivuko vya Kigamboni

mutanim

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2010
Posts
203
Reaction score
77
Tumeshuhudia kwa muda mrefu sasa namna ambavyo wakazi wa Kigamboni wanataabika katika utaratibu mzima wa kuvuka kwa kutumia vivuko vyake vya MV Kigamboni na Magogoni, na baada sasa, Mv Lami inayofanya kazi pahala pa Magogoni iliyopo matengenezoni, na Azam sea tax, ambayo ni ubunifu mwingine ambao mzalendo Bakhresa anajaribu kuufanya.

Jambo ambalo linaukakasi ni kwamba uendeshaji wa vivuko umekuwa usioridhisha kabisa, tena kwa muda mrefu sana. Huduma hii bado inaendeshwa na mamlaka ya serikali, TEMESA, kwa ushirika usio wa wazi na vikosi vya jeshi. Washirika hawa wamedhihirisha kushindwa kujipanga kutumia rasilimali hiyo, kwanza kutoa huduma, na pia kuchangia ktk mfuko wa serikali kama ilivyo mfano, BRT.

Swali la wazi ni kwamba imewezekana vipi kwa mabasi ya mwendo kasi kuendeshwa na kampuni binafsi, pia usafiri wa ferry kwenda Unguja na Pemba, pia shughuli za upakiaji na upakuaji mizigo kule TICTS.

Hapa kivukoni Maxmalipo wanasaidia ukusanyaji wa nauli, lakini nina mashaka kama wanaweza kutoa hesabu yao kwa siku (masaa 24). Na pengine kueleza fedha hizo zinatumika vipi kuboresha huduma.

Matatizo ya sasa ni pamoja na kusubiri kivuko kwa zaidi ya nusu saa, na kuongezeka kwa msongamano wakati wa asubuhi na jioni, pia kutumia muda mtrefu kuvuka, pengine zaidi ya dakika 15, na wakati mwingi pia, kushindwa kwa waendeshaji (mabaharia) kuegesha vizuri na kuendeleza kero kwa watumiaji.

Pamoja na juhudi za kutukuka,za ndugu yetu km nilivyomtaja hapo mwanzo, lakini hakuna utaratibu rasmi wa matumizi yake, mpaka kupelekea purukushani za kinyamanyama hivi iwapo mtu atajaribu kutumia Azam Sea tax.

Ushauri wangu kwa msistizo, ambao bila shaka umetolewa pia na wengi ni kwamba, huduma hii ibinafsishwe, tena kwa mtoa huduma ambaye ameonyesha uwezo mkubwa na upendo wake katika kusaidia wananchi bila kudai ziada yoyote. AZAM amekuwa mstari wa mbele katika kuokoa jahazi wakati wote wa kushindikana kutoa huduma kwa vivuko vya serikali.

Azam apewe mkataba wa kuendesha vivuko hivyo, ndipo itakapoonekana faida kubwa iliyokuwa ikipotea kwa muda mrefu, na ataboresha sana huduma pamoja na kuondoa kabisa kwa wananchi. Hakuna sababu inayofanya watu wa Kigamboni tuendelee kutaabika pale tunapojaribu kuvuka.

Tusisubiri kila jambo mpaka Mh Rais ndiyo atoe maamuzi, kila mmoja katika eneo lake afanye kazi na kujenga taifa kwelikweli. Ni aibu kwa serikali kwamba bado tunazungumzia kero hii ambayo ufumbuzi wake upo wazi kabisa. Tusiin'gan'gania kama ilivyo ATCL, hakuna sababu ya msingi.
 
Back
Top Bottom