Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,650
- 21,011
siku za karibuni nilikuwa natafuta mbolea ya kuweka kwenye migomba. nikaambiwa mbolea ya kuku ni nzuri sana, nikaenda kuitafuta. nikakuta inabei kubwa sana. gunia la debe kumi wanauza 4,000 -7,000. nikasema hii ina uspecial gani? nikakutana na huu ulinganifu.
mbolea wanapozilinganisha huangalia zaidi NPK%. nitrogen husaidia kutengeneza majani na kufanya shamba kuwa la kijani. ikizidi huwa inaunguza mimea kwa kukausha maji, pia hufanya mizizi na matunda yasikuwe vizuri. hivyo inatakiwa umakini sana wakati wa kutumia mbolea zenye N nyingi kama ya kuku na sungura.
phosphorous husaidia kwenye utoaji wa maua na potasium hufanya kazi nyingi ikiwemo kukuza tunda. migomba ikikosa potasium huzaa mikongo midogo sana.
baada ya kuona huu ulinganifu nimeonelea niendelee kutumia mbolea ya ng'ombe. kwanza ina potasium sawa na ya kuku na kikubwa kwenye migomba ni potasium, bei yake ni rahisi sana, gari tani 5 haizidi laki 2. pia mahitaji phosphate skwa migomba siyo makubwa hivyo 0.4% ya ng'ombe itatosha. pia kutukuwa na N nyingi kunafanya mbolea ya ng'ombe iwe salama sana. niliona nishee hii.