Ufalme wa Uingereza

Ufalme wa Uingereza

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
362
Reaction score
906
UFALME WA UINGEREZA.

Na. Comred Mbwana Allyamtu CMCA
Monday-12/09/2022
Tabora- Tanzania

Kwanza kabisa Familia ya kifalme nchini Uingereza hairuhusiwi kikatiba kujihusisha na masuala ya kisiasa kabisa.

Siasa na ufalme ni vitu viwili vilivyo tenganishwa kabisa, ndio maana sio rahisi kukuta familia ya kifalme ikipata shuta au kuhusishwa na siasa za Uingereza.

Japokuwa mfalme au Malkia wa Uingereza huwa na ushawishi wa kiutawala nchini Uingereza, sio rahisi kukuta mfalme au malikia kuwa na mgongano na serikali (inayoongozwa na Waziri mkuu) mara ya mwisho kutokea hilo ilikuwa ni mwaka 1812.

Mfalme au Malkia wa Uingereza huwa hana chama cha Siasa, na hatakiwi kuwa na mlengo wa upande wowote ule na vyama vya kisiasa.

Kimamlaka mfalme au Malkia ndie mwenye nguvu Uingereza, lakini hapaswi kuingilia utawala wa umma (serikali inyoongozwa na Waziri mkuu).

Ili kutenganisha hilo, mfalme au Malkia sio mkuu wa serikali (Head of government), japo nguvu yake ina turufu kwenye bunge au serikali.

Mfalme au Malkia wa Uingereza ndio mkuu wa nchi (Head of state) na Amiri wa majeshi ya Uingereza.

Uteua na kumpa baraka Waziri mkuu baada ya michakato ya kwenye vyama au uchaguzi kumalizika.

Ndio Mkuu wa kanisa la Uingereza (Anglican) na mkuu wa bunge la Westminster (rejelea chemba ya bunge la Mabunyenye "House of Lord") soma hii makala yangu kuhusu bunge la Westminster la Uingereza na mamlaka yake kulijua hili... .

Mfalme au Malkia wa Uingereza ana mamlaka ya kuivunja serikali na kuitisha uchaguzi mkuu.

Kwa mujibu wa sheria ya "Royal monarch Code" Malkia au Mfalme wa Uingereza ndie absolute voice juu ya Sheria zote zitakazopitishwa na bunge la walalahoi " House of Common" hii ni kuwa Bunge likisha jadili muswada wa Sheria, malkia au Mfalme huwa anapelekewa muswada kuupitisha ili uwe Sheria rasmi, utaratibu huu huitwa "Royal assent".

Hii Royal assent kwa utamaduni wa Uingereza ni utaratibu ambao mswada wowote lazima upite mbele ya mfalme au Malkia ili kuidhinishwa kuwa Sheria.

Kiuhalisia ni ngumu Malkia au Mfalme wa Uingereza kutopitisha mswada huo kuwa Sheria.

Japo mara ya mwisho ilishatokea hilo kwa Malkia Anne l kugomea kupitisha Sheria mwaka 1708, toka hapo aijatokea tena mpaka leo.

Utawala wa kifalme nchini Uingereza ulianza rasmi mwaka 519 chini ya mwasisi wa Anglo-Saxon of Wessex iliyoanzishwa na mwasisi wao aitwae mfalme Cerdic.

Lakini Uingereza hii ya leo ilianzia England na Wales, hii ndio iliyoanzisha huu ufalme wa sasa, ufalme huu ulianza mwaka 827 chini ya ufalme wa Saxon na mfalme wake wa kwanza ni EGBERT aliyetawazwa mwaka 827 na kufariki mwaka 839, jina lake huitwa Egbert (Ecgherht) neno "England" limetokana na neno lake.

Huyu ndie hutajwa kama mfalme wa Kwanza wa Uingereza hii ya sasa.

Toka yeye umeshapita jumla ya ufalme 67 (royal monarch) rasmi, na 20 wasio rasmi, lakini jumla ya watawala wote ni 110.

Kabla ya huyu EGBERT kulikuwa na mfalme aliyeitwa Brihtric (jina Britain linatokea kwake) huyu Brihtric ndie alipanua utawala wa Wessex.

Nimesema, falme rasmi za Saxon ziko 67 na za Wessex zipo 20 hivyo kuwa jumla 87, falme ndogo za Kent ni 23 rasmi, jumla tunapata falme 110.

Ni hivi.....

Asili ya Uingereza ilianzia kwa jamii ya Wessex (makazi ya Anglo-Saxon) chini ya mwanzilishi wao Cerdic, huyu Cerdic ndio mwanzilishi wa utawala wa Uingereza mwaka 519.

Huyu ndie mwanzilishi wa nasaba ya Anglo-Saxons (Anglo Saxon Chronicle) ndie kiongozi wa makazi ya Anglo-Saxon ya kwanza ya Uingereza.

Ndiye mwanzilishi na mfalme wa kwanza wa Saxon-Wessex, aliyetawala kuanzia mwaka 519 hadi 534 AD.

Wafalme wote waliomfuata wa Wessex wametokana na nasaba yake.

Huyu Cerdic ndie babu wa waingereza, Baba wa taifa la Uingereza na Mwasisi wa ufalme wa Uingereza.

Huyu Malkia Elizabeth ll ni Malkia wa 8 kwa jumla ya wanawake walio wahi kuwa malkia na wa 6 kwa Malkia rasimi kuvishwa taji na kutawazwa kuwa malkia wa Uingereza.

Malkia wa kwanza kuwa mtawala wa Uingereza ni Malkia Matilda l mwaka 1102, japo huyu atambuliwi rasmi, Malkia wa kwanza kutambuliwa kama Malkia ni Malkia Mary l wa mwaka 1516.

Kisha Malkia Elisabeth I aliyezaliwa mwaka 1533 na kufariki mwaka 1603, huyu ndie yule mtoto wa mfalme Henry VIII aliyefuta ukatoriki na kuanzisha Anglican Uingereza kwasababu tu Papa Clement Vll aligoma kumuozesha mke wa pili ili apate mtoto wa kiume.

Malkia mwenye historia muhimu Uingereza ni Malkia ANNE l huyu ndio aliyeunganisha England na Scotland (rejea sheria ya Act of Union) ndio Malkia wa kwanza wa UK.

Yes elewa UK....

UK (United kingdom) ni muungano wa eneo la England, Wales na Scotland na northern Ireland baadae 1920.

Hivyo Malkia ANNE l ndio mtawala wa kwanza wa Uingereza kuongoza mpaka Scotland.

Ufalme wa Uingereza unaongozwa chini ya Katiba ya Uingereza, sheria ya succession (Succession Code), utamaduni wa Uingereza na kanuni za kifalme za Asili.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057.
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.
 
kutawazwa kuwa malkia wa Uingereza.
Mkuu naomba kuuliza kwa nini huwa hawajitawazi wenyewe mpaka akatawazwe na mtu mwingine?? kama mtoto mdogo! ! je hawaoni aibu labda!!

kwa sababu hata mumeo tu hawezi kukutawaza!! je huwa wanatawazwa kila siku au ni mara moja tu!....km hawaoni aibu je huwa ni kwa kificho? kama wazikavyoo?
 
Braza nasaba aliyonayo Charles haitoki Wessex au Mercia. Inatoka Normandy. Kumbuka 1066 baada ya Edward the confessor kufa mtawala wa Duchy of Normandy aitwae William the conqueror aliivamia England na kuotawala. Toka hapo wametawala watu wa nasaba yake japo waingereza wengi wana nasaba za Anglo-saxons. Kwenye doomsday book waliopewa majumba makubwa hawakua Waingereza wazawa bali waja kutoka Ufaransa. Damu hiyo imeshachanganywa sana kwanza na Wascot, Wajeruman mara mbili na sasa Wagiriki. The Duke of Edinburgh ni mgiriki wa kuzaliwa.
 
Mkuu naomba kuuliza kwa nini huwa hawajitawazi wenyewe mpaka akatawazwe na mtu mwingine?? kama mtoto mdogo! ! je hawaoni aibu labda!!

kwa sababu hata mumeo tu hawezi kukutawaza!! je huwa wanatawazwa kila siku au ni mara moja tu!....km hawaoni aibu je huwa ni kwa kificho? kama wazikavyoo?
Mkuu uliuliza kuchangamsha genge au uliuliza kwa kumaanisha?

Kama uliuliza kwa kumaanisha, basi elimu yenu ya sasa ikishirikiana na uandishi kanjanja wa mitandao ya kijamii inawatesa kwa kutohimiza matumizi sahihi ya sarufi!

Kutawadha(kuchamba ama kunawa) na kutawaza(kutoa madaraka ama kutawalisha) ni neno moja?
 
Back
Top Bottom