Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Afisa habari wa Yanga Jerry Muro wakati akimkejeli afisa habari wa Simba Haji Manara, alijisifu kuwa yeye ni msomi na kingine ambacho ni bora kwake ni kwamba anaishi Mbezi Beach. Muro aliongea akiwa na muonekano wa mtu asiye na utani, alimaanisha kwamba Mbezi Beach ni sehemu ambayo sio kila mtu anaweza kuishi.
Baada ya kumsikia Jerry Muro akimwanga mbwembwe mbele ya waandishi wa habari, nikaukumbuka wimbo wa afande sele miaka kadhaa iliyopita, pale ambapo kuna mstari unasema "kwani ukiishi mbezi beach ukifa hauozi".
Lakini katika siku za karibuni, tingatinga limeonekana likivunja nyumba moja ya mbezi beach iliyojengwa kwenye kiwanja cha mtu aliyedhulumiwa eneo. Wapo wauza poda ambao wanadakwa na vyombo vya usalama, wanatiwa nguvuni wakitokea kwenye majengo yao ya kifahari yaliyopo mbezi beach. Kesi nzito za uhujumu wa uchumi zikiendeshwa kwa haki, ninao uhakika wengi tu wa mbezi beach watatiwa nguvuni.
Na maeneo kama mbezi beach au mikocheni na masaki yapo mengi tu barani Afrika, watu wanaoishi katika sehemu zenye hadhi kubwa huwa na mbwembwe kama za yule msemaji wa Yanga, lakini siku haki ikija kutendeka na kinachoibiwa kinapopiganiwa ili kirudi kwa wale walioibiwa, basi yale majumba makubwa na yenye mageti ya gharama, hushindwa kumsaidia yule aliyejisahau na kuanza kuidharau dunia inayomzunguka.
Umasikini wa mtu anayeishi sehemu inayojulikana kuwa ni maalum kwa watu wa hali ya chini anayo mateso mengi lakini hata yule ambaye jamii inamuona kama vile ameshayatoa maisha huku akiwa mkazi wa mbezi beach, na yeye huwa na siku zinazomkumbusha kuwa anaishi kwenye nchi moja na yule mlala hoi.