Ufahamu ugonjwa wa ukoma (Leprosy)

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,338
33,163
Ugonjwa wa ukoma ni katika magonjwa yaliyosahaulika katika jamii yetu, lakini ugonjwa huu bado upo katika jamii yetu. Miongoni mwa sababu zinazopelekea ugonjwa huu kusahaulika au kuonekana kama haupo ni kuchelewa kujitokeza kwa dalili za ugonjwa huu.

kwa mtu aliyeambukizwa vimelea vya ukoma takribani inachukia kati ya miaka 3 hadi 30 mtu kuanza kuonekana na dalili za ukoma tangu alipoambukizwa.

Kuenea

Ukoma ni ugonjwa wa kuambukiza kwa njia pale mtu mwenye vimelea vya Ukoma ambaye bado hajaanza tiba anapokohoa au kupiga chafya au kucheka.

Dalili

1. Kuwa na mabaka meupe katika ngozi ambayo hayana hisia yaani hayaumi wala kuwasha.

2. Kuhisi ganzi katika vidole vya mikono au miguu au sehemu za viungo.

3. Kujikunja kwa vidole hali hii ikizadi inaweza kusababisha ulemavu.

4. Kutokwa na vitu kama mapele makubwa(nodules) hasa usoni.

Pia mgonjwa anaweza kushika moto na ukawa unamuunguza bila ya kusikia maumivu.

Madhara

Madhara makubwa ya ukoma ni yafuatayo:

1. Ulemavu wa viungo kama mikono na miguu.

2. Upofu.

3. Kutengwa au unyanyapaa na jamii.

Tiba

Tiba ya ukoma ipo na inatolewa bila malipo katika vituo vya huduma ya afya vya Serikali na binafsi.

Tiba ya maradhi ya ukoma, tiba mbadala ni maji ya hinna yanasaidia kutibu maradhi ya ugonjwa wa ukoma akinywa, huyo mgonjwa wa ukoma kwa muda wa siku 40 mfulululizo inshallah atapona huo ukoma wake.

Matayarisho

Namna ya Utengenezaji wa hayo maji ya hinna chukuwa majani ya hinna yawe mabichi kiasi cha mkono wako weka katika maji glasi 3 usiku weka ndani ya jagi la maji funika usiku kucha .

Asubuhi chuja hayo maji kunywa kabla ya kula kitu kisha ukae masaa 2 ndio waweza kula chakula pia unaweza kuongeza na kijiko kimoja cha asali safi ya nyuki kunywa pamoja na hayo maji ya hinna kwa muda wa siku 40.
 
Attachments

  • leprosy.jpg
    leprosy.jpg
    24.9 KB · Views: 723
  • ukoma.jpg
    ukoma.jpg
    130.7 KB · Views: 728
  • ukoma 1.jpg
    ukoma 1.jpg
    8.4 KB · Views: 583
  • maji+ya+hina.jpg
    maji+ya+hina.jpg
    37.2 KB · Views: 516
Watafiti wasema ukoma unaweza ukawa ugonjwa wa kumbukiza.

Watafiti wamegundua geni ambazo zinahusiana na ugonjwa wa ukoma, suala ambalo linaondoa fikra ya huko nyuma kwamba ukoma si ugonjwa wa kuzaliwa au wa kuridhi.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa huko China na kuchafishwa katika Jarida la Tiba la Uingereza, mabadiliko ya geni 7 mwilini yanaweza kuwa ndio chanzo cha uwezekano wa baadhi ya watu kupatwa na ukoma.

Wataalamu hao wamesema kuwa, tangu kale imekuwa ikifikiriwa kuwa ukoma ulikuwa ukisababishwa tu na vijidudu lakini uchunguzi wao umeonyesha kuwa maambukizo ya ugonjwa huo yansababishwa pia na genetiki.

Wamesema kwamba, iwapo mzazi ana ugonjwa huo, basi kuna uwezekano mkubwa mwanaye naye akapatwa na ugonjwa huo. Hata hivyo wataalamu hao wamesema, cha kushangaza ni kuwa, iwapo mmoja kati ya mke na mume wana ukoma, mwingine hawezi kuambukizwa ugonjwa huo kwa miaka mingi.

Geni 5 kati ya hizo 7 zinazosababisha ugonjwa huo, inaaminiwa kuwa zinauhusiano wa karibu na mfumo wa kulinda mwili. Uchunguzi huo unaleta matumaini ya kuweza kukingwa mapema wale wanaodhaniwa kuwa wana uwezekano wa kupatwa na ugonjwa huo.

Vilevile utafiti huo unaweza kutumika kuchunguza zaidi vijidudu vya magonjwa mengine ambavyo vinakaribiana na vijidudu vinayosababisha ukoma, kama vile vijidudu vya kufua kikuu ugonjwa ambao husababisha vifo vya watu milioni 1.8 duniani.

Sio vibaya kujua kuwa, ugonjwa wa ukoma au Leprosy kwa kiingereza na kitaalamu Hansen's disease, unaosabaishwa na bacteria waitwao Mycobacterium Lapracea na Mycobacterium Lepromatosis huathiri ngozi, utando telezi (mucous membranes), neva za ukingoni (peripheral nerve) pamoja na macho.

Kuharibika daima neva au mishipa ya fahamu kunakosababishwa na ugonjwa wa ukoma, humzuia mtu anayepona ugonjwa huo kuhisi maumivu, suala ambalo huwafanya wagonjwa wa ukoma kuwa wenye kupata kwa urahisi majeraha madogo madogo na vidonda ambayo baadaye huwa makovu ya kudumu.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kuwa, kuna kesi 254,525 mpya za ugonjwa wa ukoma katika nchi za tropiki na zilizo chini ya jangwa la sahara.

Kumbuka kuwa ugonjwa wa ukoma unatibika na unapotibiwa mapema huweza kumuepusha mgonjwa kupata madhara makubwa ya kukatika viungo na kuwa mkoma.
 
Ugonjwa wa ukoma ni katika magonjwa yaliyosahaulika katika jamii yetu, lakini ugonjwa huu bado upo katika jamii yetu. Miongoni mwa sababu zinazopelekea ugonjwa huu kusahaulika au kuonekana kama haupo ni kuchelewa kujitokeza kwa dalili za ugonjwa huu.

kwa mtu aliyeambukizwa vimelea vya ukoma takribani inachukia kati ya miaka 3 hadi 30 mtu kuanza kuonekana na dalili za ukoma tangu alipoambukizwa.

Kuenea

Ukoma ni ugonjwa wa kuambukiza kwa njia pale mtu mwenye vimelea vya Ukoma ambaye bado hajaanza tiba anapokohoa au kupiga chafya au kucheka.

Dalili

1. Kuwa na mabaka meupe katika ngozi ambayo hayana hisia yaani hayaumi wala kuwasha.

2. Kuhisi ganzi katika vidole vya mikono au miguu au sehemu za viungo.

3. Kujikunja kwa vidole hali hii ikizadi inaweza kusababisha ulemavu.

4. Kutokwa na vitu kama mapele makubwa(nodules) hasa usoni.

Pia mgonjwa anaweza kushika moto na ukawa unamuunguza bila ya kusikia maumivu.

Madhara

Madhara makubwa ya ukoma ni yafuatayo:

1. Ulemavu wa viungo kama mikono na miguu.

2. Upofu.

3. Kutengwa au unyanyapaa na jamii.

Tiba

Tiba ya ukoma ipo na inatolewa bila malipo katika vituo vya huduma ya afya vya Serikali na binafsi.

Tiba ya maradhi ya ukoma, tiba mbadala ni maji ya hinna yanasaidia kutibu maradhi ya ugonjwa wa ukoma akinywa, huyo mgonjwa wa ukoma kwa muda wa siku 40 mfulululizo inshallah atapona huo ukoma wake.

Matayarisho

Namna ya Utengenezaji wa hayo maji ya hinna chukuwa majani ya hinna yawe mabichi kiasi cha mkono wako weka katika maji glasi 3 usiku weka ndani ya jagi la maji funika usiku kucha .

Asubuhi chuja hayo maji kunywa kabla ya kula kitu kisha ukae masaa 2 ndio waweza kula chakula pia unaweza kuongeza na kijiko kimoja cha asali safi ya nyuki kunywa pamoja na hayo maji ya hinna kwa muda wa siku 40.
Pamoja sana Mzizi mkavu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom