ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,603
Hivi karibuni tumeshuhudia kuwepo kwa sintofahamu baina ya mataifa matatu ambayo ni China, Korea kusini na Marekani kufuatia kile kinachodaiwa na Uchina kwamba ni mpango wa Marekani kutishia usalama kwa kuruhusu uwekwaji wa mtambo wa kisasa wa kuzuia makombora(THAAD) nchini Korea kusini ikiwa ni moja ya njia za kukabiliana na vitisho vya Korea kaskazini.
He, ni kwanini China inahofu kwa mtambo huo kupelekwa nchini Korea Kusini.
Vifuatavyo ni vitu vya kujua kuhusiana na mtambo huu wa kuzuia makombora ujulikanao kama THAAD(TERMINAL HIGH ALTITUDE AREA DEFENCE)
Terminal High Altitude Area Defence(THAAD) ni mtambo wa kisasa kutungua makombora uliotengenezwa na Marekani.Umetengenezwa kwa ajili ya kutungua makombora ya masafa mafupi, ya kati na hata yale ya masafa marefu. Mtambo huu umebuniwa kutungua makombora yakiwa kwenye Terminal phase yaani kabla kombora halijatengana na milipuko.
Makombora ya mtambo huu hayatumii milipuko katika shughuli yake ya utunguaji makombora mengine kama mitambo mingine kama S300 n.k bali hutumia teknolojia ya Hit to kill(au kinetic kill technology) teknolojia hii pia inapatikana kwenye mfumo wa Arrow 3 unaotumiwa na Israel pia unatarajiwa kuwepo kwenye mtambo wa kisasa wa Urusi ujulikanao kama S500.
Mtambo huu unatumia rada aina ya X Band iliyotengenezwa na kampuni ya kimarekani ya Raytheon.Hii ni moja ya rada kubwa aina ya X band ambazo zinaweza kusafirishwa kirahisi kwa njia ya ardhi au anga na kupelekwa popote pale.
Sifa nyinginezo:
Weight: 900kg:
Length: 6.17m
Diameter: 34cm
Interception Range: 200km(actual range is classified)
Speed: Mach 8.24
Guidance system:
Indium antimonide imaging infrared seeker head.