Ufahamu kuhusu kulangua mpunga.

Top gun maverick

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
2,018
2,599
Habari poleni na majukumu ya Kazi na mihangaiko ya usiku mchana.mimi Ni kijana ambaye na ndoto ya kufanya biashara ya nafaka.hususani ya kulangua mpunga vijijini na kuuza mjini. Ila sina uzoefu wowote,pia ufahamu kuhusu mtaji,na changamoto,na faida yake hivyo naomba mwenye ujuzi aweze kunisaidia natanguliza shukrani.
 
Ukitaka kufanya iyo biashara nenda wilaya kilombero, Mahenge na Malinyi mkoa wa morogoro.

Beba pesa ya uwezo wako. Nunua Mpunga tena kipindi hiki ndio wanavuna Nenda mashambani nunu mpunga kisha uanike kisha upaki kwenye mifuko na uweke kwenye ma godown ya kukodisha. Ikifika mwezi wa 10 na 11 nenda kakoboe mpunga na kusafirisha mchele kwenda miji mikubwa
 
Kuna uwezekano ukanunua mpunga ambao haukuvunwa vzr au uliozama kwenye tope n.k hii n hasara kubwa mnoo utakapoukoboa utatoka vby na hivyo utauza kwa bei ya hasara so hyo inakata mtaj fastaa.
Changamoto ya pili, n kwamba kuna mpunga mwingne unakuwa n mwepesi sana ukiukoboa unatoa kg chache sn hivyo inapelekea kuporomosha matazamio yako ya faida na hadi kupelekea hasara.
Kwa ufupi n biashara ya leo unapata, kesho unakosa so unapofanya jiandae kwa hali hizo.
Biashara inayokupa uhakika wa pesa yako n ya kununua mchele moja kwa moja maana utaona ubora wake pia utakuwa na uhakika wa kg unazoingiza kwenye mzunguko hivyo kuifahamu faida halisi.
 
Huu ndio ushauri tosha!! Biashara ya kununua mpunga ni pasua kichwa sana!!! Kwani kwenye kwenda kununua, kuna kununua BIRIANI, utakuja lia. Biashara nzuri ni ya mchele
 
What if akinunua mpunga akahifadhi na badae akaja kuuza mpunga bila ya kuukoboa ukipanda bei?
Tatizo la biashara ya mpunga, ina hitaji utalaam sana kwenye kuuchagu huko. Polini wakati wa kununua, kwani wataalam wanatumia mikono kuupalua ndio ajue ubora wake, sasa wewe ukiingia kichwa kichwa utanunua mbaya, hata ukiuweka store uje kuuza badaye kama mpunga tena, bado kama ni mbaya mnunuzi atauparuza kwanza kuona ubora wake, ndio mkubaliane bei!!! Kiufupi biashara ya mpunga ni pasua kichwa,hasa kwenye manunuzi. Huko polini, ukitaka maelezo zaidi njoo pm!! Hii biashara nina uzoefu nayo sana
 
Duuh aisee nilikuwa nafikir hii biashara ni rahisi tu kwamba nanunua naweka stoo halaf naondoka kufanya shughuli zangu zingine miezi 3 mbele naenda kupiga faida tu.
 
Tatizo la biashara ya mpunga, ina hitaji utalaam sana kwenye kuuchagu huko. Polini wakati wa kununua, kwani wataalam wanatumia mikono kuupalua ndio ajue ubora wake, sasa wewe ukiingia kichwa kichwa utanunua mbaya, hata ukiuweka store uje kuuza badaye kama mpunga tena, bado kama ni mbaya mnunuzi atauparuza kwanza kuona ubora wake, ndio mkubaliane bei!!! Kiufupi biashara ya mpunga ni pasua kichwa,hasa kwenye manunuzi. Huko polini, ukitaka maelezo zaidi njoo pm!! Hii biashara nina uzoefu nayo sana
Nimekuelewa mkuu,barikiwa sana
 
Habari poleni na majukumu ya Kazi na mihangaiko ya usiku mchana.mimi Ni kijana ambaye na ndoto ya kufanya biashara ya nafaka.hususani ya kulangua mpunga vijijini na kuuza mjini. Ila sina uzoefu wowote,pia ufahamu kuhusu mtaji,na changamoto,na faida yake hivyo naomba mwenye ujuzi aweze kunisaidia natanguliza shukrani.

!
!
Chukua Ndoo Ya lita ishirini, kisha tia petroli kama lita nne hivi. Ukimaliza funika na nailon halafu bandika mfuniko kisha anika juani kwa siku kama tano hivi mfululizo. Baada ya hapo osha ndoo yako vizuri ingia nayo huko unakokwenda kununua huo mpunga wako. Tumia ndoo hiyo Kununulia, lakini kwenye kuuza unauza kwa kutumia ndoo ya kawaida
 
mkuu siku hizi kuna ndoo za kupimia huo mpunga huko polini zimeshafanyiwa utundu kitaalamu ndoo moja inauzwa laki 2!!sio mchezo hata mkulima kuishitukia ni shida ila hizo nyingine za kutengeneza mwenyewe local wanazishitukia sana na utapelekwa hadi kwa mwenyekiti wa kijiji kwa uhujumu uchumi !!!tatizo la biashara ya kununua mpunga ni kwenye kuukagua ubora wake kwani huuoni unakuja kuukoboa baba ni chenga/biliani(rangi ya uvundo)tayari hasara tofauti na biashara ya. mchele unanunua kitu unachokiona.
 
Wabongo kwa teknolojia za wizi wako juu sana.
 
Biashara ya nafaka hususani mpunga ni nzuri ikiwa tu utafanya mambo yafuatayo;

1.Uvumilivu (kuweka stoo mpunga then uje kuuza mchele baadae au hata mpunga huohuo)

2.Uchaguzi mzuri wa mpunga (Kuna mbegu nyingine sio nzuri au mpunga kulowa maji wakati wa kuvuna baadae huwa unakatika sana ukiukoboa)

3.Ghala (Hakikisha una sehemu nzuri ya kuhifadhi mpunga ila usiharibiwe panya maana huwa wanaweza kula hata gunia moja likaisha)

Mwaka jana nilikuwa na gunia 30 za mpunga 15 nilipata hela nzuri kwakuwa mpunga ulikuwa fresh ila 15 nyingine niliuza kwa bei ndogo japokuwa sikupata hasara.

N.b; Ukizingatia hivyo vitu 3, ukauza bei nzuri sokoni utapiga sana hela mkuu, nataka nisifanye makosa tena najiandaa niingie porini.
 
Kwa kuanza mm ningeshauri ununue mchele mpunga kuna mengi ya kuzingatia na kwa mgeni n rahisi kupigwa. Ukipata mpungu alioingia maji ukikoboa unafubaa na kuvunjika hiyo n hasara tayari n afadhali mchele unauona. Unaweza kusafirisha mpunga tani 10 ukifikisha na kukiboa utapata sio zaidi ya tani 6.
 
Tatizo la biashara ya mpunga, ina hitaji utalaam sana kwenye kuuchagu huko. Polini wakati wa kununua, kwani wataalam wanatumia mikono kuupalua ndio ajue ubora wake, sasa wewe ukiingia kichwa kichwa utanunua mbaya, hata ukiuweka store uje kuuza badaye kama mpunga tena, bado kama ni mbaya mnunuzi atauparuza kwanza kuona ubora wake, ndio mkubaliane bei!!! Kiufupi biashara ya mpunga ni pasua kichwa,hasa kwenye manunuzi. Huko polini, ukitaka maelezo zaidi njoo pm!! Hii biashara nina uzoefu nayo sana
kwa hiyo mkuu unataka kusema stock za mpunga siku hizi hazilipi, maana kuna maeneo amabayo yanasifika kwa kuivisha mpunga mzuri.
 
Biashara ya nafaka hususani mpunga ni nzuri ikiwa tu utafanya mambo yafuatayo;

1.Uvumilivu (kuweka stoo mpunga then uje kuuza mchele baadae au hata mpunga huohuo)

2.Uchaguzi mzuri wa mpunga (Kuna mbegu nyingine sio nzuri au mpunga kulowa maji wakati wa kuvuna baadae huwa unakatika sana ukiukoboa)

3.Ghala (Hakikisha una sehemu nzuri ya kuhifadhi mpunga ila usiharibiwe panya maana huwa wanaweza kula hata gunia moja likaisha)

Mwaka jana nilikuwa na gunia 30 za mpunga 15 nilipata hela nzuri kwakuwa mpunga ulikuwa fresh ila 15 nyingine niliuza kwa bei ndogo japokuwa sikupata hasara.

N.b; Ukizingatia hivyo vitu 3, ukauza bei nzuri sokoni utapiga sana hela mkuu, nataka nisifanye makosa tena najiandaa niingie porini.
VIpi bei ya kuuzia ilifika japo 1.5 kwa aulionunulia, na zile 15 zilikuwa na shida gani mkuu?. kingine nachojua kwenye mpunga uwe na mtu mzoefu na mwaminifu wakati unakusanya.
 
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png

Wabongo kwa teknolojia za wizi wako juu sana.
baba hiyo ndoo sio mchezo ukiiona kwa juu juu tu huwezi gundua ila anza kutia kitu humo ndio utaona jinsi linavyomeza!!wewe ndoo hii iuzwe laki 2!!!nchi hii mkulima anapata tabu saa
kwa hiyo mkuu unataka kusema stock za mpunga siku hizi hazilipi, maana kuna maeneo amabayo yanasifika kwa kuivisha mpunga mzuri.
kwa kweli biashara ya mpunga inahitaji umakini sana!!hasa kwenye manunuzi kwani ukibugi kidogo tu una kata mtaji!!mfano mwaka jana wakati wa mavuno kuna sehemu gunia la mpunga liliuzwa kwa 30,000!!hukopolini hadi linafika mjini ni kama 45,000 ,hapo hujalipia store!!unakuta bei inafika hadi 55,000,mwezi wa nne mwaka huu bei ya kuuzia ilikuwa 55,000-60,000!!!!hapo kuna nini??miaka ya nyuma kweli ilikuwa inalipa kwani mtu akiweka store alikuwa anaweza kuuza hadi 80,000 ila sio kwa kipindi hiki!!labda uukoboe uuze mchele na utoke vizuri sasa
 
baba hiyo ndoo sio mchezo ukiiona kwa juu juu tu huwezi gundua ila anza kutia kitu humo ndio utaona jinsi linavyomeza!!wewe ndoo hii iuzwe laki 2!!!nchi hii mkulima anapata tabu saa

kwa kweli biashara ya mpunga inahitaji umakini sana!!hasa kwenye manunuzi kwani ukibugi kidogo tu una kata mtaji!!mfano mwaka jana wakati wa mavuno kuna sehemu gunia la mpunga liliuzwa kwa 30,000!!hukopolini hadi linafika mjini ni kama 45,000 ,hapo hujalipia store!!unakuta bei inafika hadi 55,000,mwezi wa nne mwaka huu bei ya kuuzia ilikuwa 55,000-60,000!!!!hapo kuna nini??miaka ya nyuma kweli ilikuwa inalipa kwani mtu akiweka store alikuwa anaweza kuuza hadi 80,000 ila sio kwa kipindi hiki!!labda uukoboe uuze mchele na utoke vizuri sasa
Ni kweli msimu uliopita mpunga ulikuwa mwingi sana maeneo mengi bei haikupanda. pia we unaonekana unaenda porini mbali sana kozi mi navojua maeneo mengi mpaka gunia linafika store haizidi 5000.
 
mimi nilikuwa mdau wa biashara hiyo huko nyuma ila bado naifuatilia kwani kuna watu wanaifanya mfano mwaka huu hadi sasa gunia sehemu nyingi linauzwa 45,000,ushuru 3000,usafiri 5000,wabebaji hapo bado gharama za store za kuuhifadhi ambazo kwa gunia ni 4000!!!
 
Back
Top Bottom