Umekurupuka!!Kwanini Marekani kuna vyama viwili tu vya Siasa tofauti na baadhi ya nchi nyingine??
Na je mtu akitaka kuanzisha chama chake cha Siasa anaruhusiwa kwa Sasa?
Thanks for refference Ndugu.Kuna vyama vya siasa zaidi ya hivyo viwili.Its just that Democratic na Republican ni two of the largest na more well known.
Kwamfano the third largest ni Libertarian party, pia kuna Green party.
Kujua vyama vingine zaidi, take a look at this link: List of political parties in the United States - Wikipedia
Asante kunijuza nikipata muda nijifunze kidogo siasa za MarekaniNa ni vizuri kwa Taifa kama USA kuwa na vyama ambavyo ni taasisi na ni za kitaifa kuliko vyama vidogo vidogo. Ujue nchi ile ni mkusanyiko wa majimbo zaidi ya 50 yanayoendesha mambo yao kivyao
Walikuwa na wagombea, Libertarian mgombea wake ni Gary Johnson ambae pia ni former governor wa New Mexico na Green Party mgombea wake ni Jill Stein ambao ni former doctor na mwalimu at Harvard Medical School.Thanks for refference Ndugu.
Kwanini hivyo vingine hawana wagombea?
Walikuwa na wagombea, Libertarian mgombea wake ni Gary Johnson ambae pia ni former governor wa New Mexico na Green Party mgombea wake ni Jill Stein ambao ni former doctor na mwalimu at Harvard Medical School.
Gary Johnson alipata kura za wananchi 4.1m sawa na 3.3% lakini hakupata any electoral votes, na Jill Stein alipata kura 1.2m sawa na 1% nae pia hakupata any electoral votes, ukilingnisha na Trump na Clinton ambao walipata kura za wananchi atleast 60m each na electoral votes.
Walikuwa na wagombea, Libertarian mgombea wake ni Gary Johnson ambae pia ni former governor wa New Mexico na Green Party mgombea wake ni Jill Stein ambao ni former doctor na mwalimu at Harvard Medical School.
Gary Johnson alipata kura za wananchi 4.1m sawa na 3.3% lakini hakupata any electoral votes, na Jill Stein alipata kura 1.2m sawa na 1% nae pia hakupata any electoral votes, ukilinganisha na Trump na Clinton ambao walipata kura za wananchi atleast 60m each na electoral votes.
Naona mfumo wao upo tofauti kabisa na baadhi ya Nchi kura za wananchi then electoral votes
Wanaopiga Hizo electoral votes ni akina nani hasa?
Ngoja nijaribu kujibu na hili. Hapana magavana sio wabunge.Asante kunijuza nikipata muda nijifunze kidogo siasa za Marekani
Na wale Magavana kazi zao hasa ni nini na tunaweza kuwalinganisha na Wabunge kwa hapa kwetu Tanzania?
Asante kunifungua akili kwa hiyo kuna wabunge na Magavana?Ngoja nijaribu kujibu na hili. Hapana magavana sio wabunge.
So Marekani wanatumia mfumo wa federation, Tanzania ni a republic.
So according to google federation ni a "group of states with a central government but independence in internal affairs", yaani ni shirikisho la nchi mbalimbali lenye serikali kuu lakini pia zinazokuwa na uhuru katika mambo yao ya ndani.
So marekani ni muunganiko wa nchi 50 na kila state ina bunge lake na kiongozi mkuu wa hizo states ni governor. E.g fikiria Tanzania, Uganda na Kenya ingekuwa ni federation, tuiite East Africa Federation inamaana kungekuwa na Rais wa East Africa Federation na pia bunge la East Africa Federation lakini inamaana Magufuli angekuwa Governor wa Tanzania, Kenyatta angekuwa Governor wa Kenya na Museveni angekuwa Governor wa Uganda na pia kila nchi ingebaki na mabunge yake kama ilivyo sasa kwaajili ya kutunga sheria za ndani ya nchi zao.
Tuanze na magavana, hawa wanachaguliwa na wananchi wa states zao.Asante kunifungua akili kwa hiyo kuna wabunge na Magavana?
Na wabunge wanachaguliwaje?
Na magavana wanapatikaje?
Sababu nimesikia kuna Mbunge mwenye asili ya Somalia amechaguliwa na Watu wa Jimbo husika ndo wanachagua wabunge wao au?
Mkuu nashukuru kwa maneno mazuri hakika nimejifunza kitu. Kwa hiyo unamanisha kila jimbo(nchi) ina rais wake(governor) na ina bunge lake(senate) halafu na anatoka mbunge kutoka katika kila jimbo kuwakilisha hilo jimbo taifani(congress) ambao unaweeza kuwaita representative ambao nao huchaguliwa na wananchi pia.Tuanze na magavana, hawa wanachaguliwa na wananchi wa states zao.
Tuje kwa wabunge. Bunge la marekani na mabunge ya states mbalimbali ni bicameral hii inamaana bunge linakuwa na two assemblies, chambers au houses. Ukicompare na Tanzania ambalo ni unicameral.
Kwasababu hii, ndio maana unakuta kuna wabunge wengine wanaitwa Senators na pia kuna wabunge wakawaida.
Bunge la marekani ambalo linaitwa Congress, kwasababu ni bicameral kuna two chambers, Senate na House of Representatives.
Jumla lina wabunge 535, 435 ni wabunge ambao wao wanawaita Representatives na wako kwenye chamber ya House of Representative na 100 ni Senators ambao wako kwenye chamber inaitwa Senate, wabunge wote hawa wa aina hizi mbili wanachaguliwa na wananchi.
Wabunge wa House of Representatives, kama huyo mbunge mwenye asili ya Somalia, wanachaguliwa na wananchi wa majimbo yao ambao wao wanayaita districts, kwa muhula wa miaka miwili. Hayo majimbo yanagawanywa katika kila states kulingana na idadi ya wananchi wa hiyo state. Na wabunge ambao ni masenator wanachaguliwa na wananchi wa states zao kwa muhula wa miaka sita. Na kila state inachagua masenator wawili.
Kazi kubwa ya House of Representatives ni kutengeneza na kupitisha sheria za nchi nzima, ambazo miswada hiyo pia itahitajika kupitishwa na Senate na kupatiwa sahihi ya Rais ili iweze kuwa sheria.Pia wanaweza kuweka sheria za kodi mbalimbali na pia kumshitaki au "impeach" kiongozi yoyote yule wa serikali. Kiongozi atakaeshitakiwa lazima akajibu mashitaka na kuhukumiwa mbele ya Senate. Na pia wanamchagua Rais wa Marekani ikitokea wagombea wote wa urais wamepata kura sawa za electoral votes.
Kazi ya Senate ni wanaweza kumchagua makamu wa Rais endapo hao makamu wa rais pia wamepata kura sawa za electoral votes. Pia kukubali au kukataa teuzi mbalimbali za secretaries of different departments za serikali, secretaries ni sawa na mawaziri, pia kukubali au kukataa teuzi za majaji, viongozi wa jeshi, balozi na viongozi wa taasisi mbali mbali za serikali.
Chambers zote hizi mbili za Congress zipo located katika jengo moja, Capitol Building.