Ufafanuzi wa SSRA kuhusu hali na mwenendo wa NSSF

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
logo-ssra.png


Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zisizo rasmi kuhusu hali na mwenendo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Baadhi ya taarifa hizo zimekuwa zikieleza kwamba mali za Mfuko huo zimetumiwa vibaya na hivyo kuathiri mafao kwa wanachama.

Taarifa hizi zimesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wanachama wa NSSF na wadau wa Sekta ya Hifadhi ya jamii kwa ujumla kwa kuhofia usalama wa wa fedha na mafao yao.

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inapenda kuwaondoa hofu wanachama wote wa Mfuko wa NSSF na Wananchi kwa ujumla na kuwahakikishi kwamba Mfuko wa NSSF upo katika hali nzuri kifedha na unaendelea kulipa mafao ya wanachama kama kawaida.

Kama mnavyofahamu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko alikwishateuliwa na anaendelea na majukumu ya kusimamia shughuli zote za Mfuko.

Vilevile, taratibu za kupata Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko huo zipo katika hatua za mwisho.

Aidha, SSRA kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania kwa mamlaka waliyopewa chini ya Kifungu cha 6(2) (c) cha Sheria Na.8 ya mwaka 2008 ikisomwa pamoja na kifungu cha 40 na cha 48 wanaendelea kufanya kaguzi za Mifuko yote ukiwemo Mfuko wa NSSF kwa lengo la kuhakikisha kwamba muda wote Mifuko yote inakuwa katika hali nzuri kwa maslahi ya wanachama na taifa kwa ujumla.

Mwisho, Mamlaka inapenda kuwaondoa wasiwasi wanachama walioathirika na taarifa hizi pamoja na wanachama wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuwahakikishia kwamba fedha na mafao yao yapo salama na Mamlaka inazifanyia kazi kero zao kwa bidii kubwa.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar es Salaam
 
Kwa maana hiyo hakuna matumizi mabaya katika Mifuko yetu pamoja na hakikisho kwamba wanachama tutalipwa stahiki zetu?
 
Maoni yangu kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii inatakiwa kutoa mikopo kwa wanachama wake kwa riba nafuu ili kuweza kujikimu na halu ya maisha ya sasa ambayo yana mahitaji mengi ukizingatia mabadiliko yaliyokuja na serikali ya awamu ya tano ambayo ni kubana matumiz, hivyo kuwaacha watumishi hasa waserikali kutokuwa na fedha za kumudu maisha.. Pia kusubiri mpaka mfanyakaz astaafu ndo apewe mafao ktk umri wa miaka 60 linabaki kuwa bahati kwa kuwa hata life sparn ya mtazania kwa sasa ni chini ya miaka 45 hivyo wafanyakaz hufariki na kuacha mafao yao au kutofaidi matunda ya mifuko ya jamii. La mwisho, tumeshuhudia miradi mikubwa ikifanywa na hii mifuko kwa mfano, nssf kwa kupitia mirad ya daraja la kgamboni, chuo kikuu cha dodoma na nyumba zinazojengwa hazina faida ya mojakwamoja kwa wanachama wa mifuko hiyo.. Nitoe rai kwa mifuko hii kukaa na kutafakari njia zipi bora zitakazoweza kumsaidia mchangiaji kunufaika kabla ya kustaafu.
 
Back
Top Bottom