Ufafanuzi wa matumizi na michango: Kila familia ilipewa Sh 1m siku ya kuaga, Zitapewa Sh 3,857,143

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema anasikitishwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao wamelichukulia suala la vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent kisiasa.

Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Gambo amesema uongozi wa mkoa wa Arusha umeamua kutoa taarifa ya wazi kwa yumma kuhusu michango iliyotolewa na matumizi yake.

“Hili si tukio la kisiasa bali ni mtihani na changamotyo kubwa uliozikumba familia za wananchi wetu. Wakati serikali inahangaika na shida za watu tunasikitika kuona baadhi ya viongozi wa kisiasa wanahangika na mitandao ya kijamii,”imesema taarifa hiyo

Taarifa hiyo iliyoambatana na jedwali lenye mchanganuo wa rambi rambi hizo inaonyesha kuwa jumla ya michango ya serikali na ya wadau ni Sh 261.3 milioni.

Michango ya Serikali ni Sh 102.7milioni na ya wadau ni Sh 158.5milioni.

Katika mchanganuo wa taarifa hiyo, Gambo amesema familia za wafiwa hao zitapewa Sh 3,857,143 kwa kila familia. Kila familia ilipewa Sh1milioni siku ya kuaga miili uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Chanzo: Mwananchi

------Ufafanuzi matumizi na michango------

1.png
2.png
3.png
4.png
5.png
6.png
7.png
 
Naomba niwatkane wote waliotoa michango. Kwani hawajui policy ya michango ya maafa kwa nchi hii. Wajinga. Kila mmoja angeliwapelekea wafiwa personally! Tunajenga miundo mbinu ya daraja lililoleta maafa! Haraka haraka wamesahau ya kagera. Watanzania wajinga! (Note: ujinga sio tusi please)
 
Ndio maana anaishi maisha ya kujifichajificha, mwenzie Lema anajiachia tu, kila anakokatiza kundi la wakazi wa Arusha linamsindikiza mbunge wao. Hapo Gambo ndio anasema eti Lema anafanya mikutano ya kisiasa, hajui kutofautisha kati la kulakiwa na mikutano ya siasa. Watu wa Arusha hongereni kumpata Lema.
 
Angeweka na hako kamchanganuo humu ingesaidia sana. Sasa mbona walipewa 1M tu badala ya kupewa zote? Lengo la kuwapa kidogo kwanza ilikuwa nini???
Hayo maswali ndio yamesababisha nianzishe uzi huu na kuweka hiyo ''title''.

Kuna mwalimu yule waliyemsafirisha Kyerwa, Kagera nakumbuka walisema kupewa 1m. Mara huku Gambo akawa anasema wametoa 3,850,000, nikajiuliza ni nani anayetoa figure sahihi. Pesa za rambirambi zina laana jamani tuache utani.
 
Naomba niwatkane wote waliotoa michango. Kwani hawajui policy ya michango ya maafa kwa nchi hii. Wajinga. Kila mmoja angeliwapelekea wafiwa personally! Tunajenga miundo mbinu ya daraja lililoleta maafa! Haraka haraka wamesahau ya kagera. Watanzania wajinga! (Note: ujinga sio tusi please)
Haya mkuu ila upumbavu ndo tusi..... angeweka wazi michango yote ni kiasi gani by names au kwa asiye taka tajwa aweka amount bila jina.... harafu kwa wafiwa aonyeshe wazi kazigawa vp maana kuna wanao sema yule yatima hakulipwa, kama hakulipwa ni kwa nn? Kwa nn wasipewe wamiliki wa alipo kuwa anaishi na yatima wenzake, mara mwalim na dereva hawakulipwa... .yawezekana wamelipwa lakini awe muwaz bana hasa katika nyakat hiz za waswas wa rambirambi za kagera la sivo halitamwacha salama hili na atakuwa anakuwa mentioned by name yeye kwa jinsi alivo handle issue nzima.....
 
Hayo maswali ndio yamesababisha nianzishe uzi huu na kuweka hiyo ''title''.

Kuna mwalimu yule waliyemsafirisha Kyerwa, Kagera nakumbuka walisema kupewa 1m. Mara huku Gambo akawa anasema wametoa 3,850,000, nikajiuliza ni nani anayetoa figure sahihi. Pesa za rambirambi zina laana jamani tuache utani.
wataogopaje laana wakati ccm yenyewe ni laana
 
cha msingi kwenye ishu kama hizi ni wafiwa kufungua account zao, Na kila anae changia awaingizie huko.full stop. Hawa viongozi wetu siwaaminifu kabisa! no waroho sana!
Ni ngumu kutekelezeka kwa kila mfiwa kuwa na akaunti yake mkuu, inabidi kutafta namna iliyo nzuri kukusanya michango. Aisee pesa ni pesa haina rafiki hata iwe ya rambirambi.
 
Back
Top Bottom