Ufafanuzi wa CUF kuhusiana na taarifa ya CAG juu ya ukaguzi wa hesabu za vyama vya siasa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
UFAFANUZI WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) KUHUSIANA NA TAARIFA YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI JUU YA UKAGUZI WA HESABU ZA VYAMA VYA SIASA:

Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha sheria ya Vyama vya siasa sura 258 iliyorekebishwa mwaka 2015, kila Chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kinatakiwa kuandaa taarifa nzuri ya fedha na taarifa za mali za za Chama. Aidha kila chama kinatakiwa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa taarifa ya mwaka ya hesabu za chama iliyokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na taarifa ya hesabu na tamko la kila mwaka la mali yote inayomilikiwa na Chama. Wajibu wa maandalizi na uwasilishaji wa taarifa za kifedha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa ajili ya ukaguzi upo kwa Katibu Mkuu wa Chama.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2016/2017 (iliyoishia tarehe 30 Juni, 2017), vyama tisa kikiwemo The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi), havikuwasilisha taarifa ya hesabu kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya ukaguzi.

The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi), kinapenda kutoa ufafanuzi ufuatao kwa umma wa Watanzania wazalendo na wapenda demokrasia.

The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi), ni Chama makini kinachozingatia sheria na taratibu za nchi. Kwa suala la fedha na rasilimali za Chama na nchi kwa ujumla,Katiba ya The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi) ya mwaka 1992 (Toleo la 2014) imebainisha katika ibara ya 7(5) kuwa lengo na madhumuni ya kuanzishwa Chama cha hiki; ni kuondoa mambo yote yanayohusu rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa aina yoyote.

Kwa msingi huo, Katibu Mkuu wa Chama amekuwa akitekeleza wajibu wake kwa kuhakikisha kuwa taarifa ya hesabu za Chama inaandaliwa na kukabidhiwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya ukaguzi na kisha kuwasilisha taarifa iliyokaguliwa kwa msajili wa vyama vya siasa kila mwaka. Wajibu huo licha ya kuwa takwa la kisheria, umebainishwa katika Kanuni za Fedha za Chama (Toleo la mwaka 2014) ambapo Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa Chama wana wajibu wa kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ajili ya kulitaarifu Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, ambalo lina wajibu wa kuhakikisha utekelezaji bora na wa dhati wa masharti yote ya sheria za nchi zinazohusu usajili na uendeshaji wa vyama vya siasa, mapato na matumizi ya fedha na mali nyingine za Chama kama ilivyoainishwa katika ibara ya 82(2)(h) ya Katiba ya The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi) ya mwaka 1992 (Toleo la mwaka 2014).

Tangu kuanzishwa kwa ukaguzi wa hesabu za vyama vya siasa mwaka 2010/2011, The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi), hakijapatapo kushindwa kuwasilisha hesabu zake kwa ajili ya ukaguzi. Itakumbukwa kwamba katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka wa fedha 2014/2015, The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi) kiliibuka kuwa Chama cha kupigiwa mfano. Mapungufu yaliyoainishwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka wa fedha 2016/2017 ya kutokuwa na rejista ya mali za Chama, kutofanyika kwa usuluhishi wa kibenki (Bank reconciliation) n.k. yalikwisha zungumzwa katika vikao vya exit meeting na kuwekewa utaratibu wa kufanyiwa kazi. Aidha kwa kuwa mwaka wa fedha wa Chama ulikuwa unakwenda Januari – Desemba na hivyo kupishana na mwaka wa serikali wa Julai - Juni, makubaliano yalifikiwa na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kubadilisha mwaka wa fedha wa Chama. Makubaliano hayo yaliafikiwa na vikao vya Bodi ya Wadhamini na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na hivyo ukaguzi wa nusu mwaka wa 2014/2015 (ulioishia tarehe 30 Juni 2015) ulifanywa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ilibakia kikao cha exit meeting ambacho kilipangwa kufanyika Jumatatu ya tarehe 26/9/2016 Ofisi Kuu ya Chama Buguruni Dar es salaam. Hata hivyo kikao hicho hakikuweza kufanyika kutokana na Ofisi Kuu kuvamiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Prof. Ibrahimu Haruna Lipumba akishirikiana na msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Katabazi Mutungi Jumamosi ya Tarehe 24/9/2016. Taarifa ya uvamizi huo ilipelekwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupitia barua Kumb.Na.CUF/AKM/003/016/051 ya tarehe 14/10/2016. Barua hiyo, ilitaarifu juu ya kushindikana kufanyika kikao cha exit meeting na uwasilishaji taarifa ya hesabu za Chama zilizofungwa za mwaka 2015/2016 tarehe 30/9/2016 kama yalivyo matakwa ya sheria kutokana na ofisi ya Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi kuvunjwa na nyaraka zote za fedha zilizoandaliwa pamoja na kompyuta ya kumbukumbu hizo kuhodhiwa na genge la wavamizi.

Tangu wakati huo, msajili wa vyama vya siasa na mshirika wake Lipumba, wamekuwa na kazi ya kufisidi fedha na mali za The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi), na jukumu la kuandaa taarifa ya hesabu za Chama na kuikabidhi kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya ukaguzi limekuwa si kipaumbele kwao.

Kwa taarifa ya uhakika tuliyonayo, Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Katabazi Mutungi mpaka tarehe 20/1/2018 amekwapua Jumla ya Tshs. 1,076,982,032.12 kupitia akaunti Na. 2072300456 ya NMB tawi la Temeke ambayo haikufunguliwa na Bodi ya Wadhamini kama inavyoelekezwa na sheria ya vyama vya siasa sura 258 kifungu cha 15.

Kwa hali hiyo na kwa kuwa si akaunti inayotambuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hakuna namna ambayo msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Katabazi Mtungi na genge lake wanaweza kandaa hesabu za akaunti hiyo na kuiwasilisha kwa ajili ya ukaguzi. Akaunti hiyo imekuwa kichaka cha wizi wa fedha ya ruzuku ya The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi).

Aidha kama alivyosema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali katika taarifa yake, wajibu wa maandalizi na uwasilishaji wa taarifa za fedha kwa ajili ya ukaguzi upo kwa Katibu Mkuu wa Chama. Kutokana na msajili wa vyama vya siasa jaji Francis Katabazi Mutungi, kutomtambua Katibu Mkuu Mheshimiwa Seif Sharif Hamad na badala yake kuanzisha cheo kipya kisichokuwa cha kikatiba cha kaimu katibu mkuu na kumteua Magdalena Hamisi Sakaya kwa nafasi hiyo; ambaye si mwanachama na hana mamlaka na akaunti za Chama zinazofahamika na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kumekuwa na kigugumizi katika mawasiliano na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Kupitia taarifa hii, The Civic United Front (CUF-Chama cha Wananchi), kinapenda kuutarifu umma kuwa kukosekana kwa taarifa ya fedha ya Chama si tatizo la Chama chenyewe bali ufisadi unaoendeshwa na msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Katabazi Mutungi na mshirika wake Prof. Ibrahim Haruna Lipumba chini ya mpango mpana unaoratibiwa na dola ili kuua upinzani makini nchini.

HAKI SAWA KWA WOTE

Seif Sharif Hamad
KATIBU MKUU
 
Msajili kala pesa ya CUF, zaidi ya Bilioni Moja?!! Kunahitajika maelezo hapa, si bure!
 
Ila jiwe kwenye kupiga pesa lina akili sana....Kumbe lengo ni kumlazimisha msajili amtambue lipumba na kumpa ruzuku ili lipumba na jiwe wagawane pesa...Hapo msajili ni zuga tu...Hawez kupiga hela za ruzuku...Jiwe ndio limepiga hizo

Awamu hii kiboko
 
Back
Top Bottom